Askari anayenyanyasa wananchi kuhamishwa kituo cha kazi, kunajenga picha gani?

Askari anayenyanyasa wananchi kuhamishwa kituo cha kazi, kunajenga picha gani?

benzemah

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2014
Posts
1,533
Reaction score
3,187
Jumatatu 20 Februari 2023, Jeshi la Polisi lilitoa taarifa kuwa limewafukuza kazi Askari wake sita mkoani Arusha (ambao hawajatajwa majina yao) katika kipindi cha miezi sita, kutokana na makosa mbalimbali ya utovu wa nidhamu yasiyoendana na maadili ya Jeshi hilo.

Siku moja baadae, Jumanne 21 Februari 2023, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamadi Masauni ametangaza kumsimamisha kazi Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kilombero (OCD) Shedrack Kigobanya huku "AKIMHAMISHA" kituo cha kazi Mkuu wa Upelelezi Wilaya hiyo (OC-CID), Daud Mshana kwa kushindwa kuwasimamia Askari wake na kudaiwa kunyanyasa Wananchi na kuwabambikia kesi.

Hoja hapa ni kama jeshi hili limeweza kuwafukuza kazi Askari huko Arusha limeshindwa nini kufanya hivyo kwa hawa wa Kilombero ambapo mmoja kasimamishwa lakini mwingine (OC-CID) amehamishwa kituo cha kazi.

Askari ambaye wananchi wamelalamika hadharani kuwa kuna baadhi ya Askari Polisi wa Wilaya hiyo ya Kilombero wanatumia nafasi zao vibaya na kunyanyasa Wananchi anahamishwa ili akaendeleze unyanyasaji sehemu nyingine au tuelewe vipi?​
 
Jeshi la Polisi limeoza!!! OCDs wa Wilaya za Bonde la Kilombero ni wanyanyasaji na wala Rushwa wakubwa.

Badala ya kuwa Walinzi wa Amani wamekuwa WAHALIFU
 
Jeshi la Polisi limeoza!!! OCDs wa Wilaya za Bonde la Kilombero ni wanyanyasaji na wala Rushwa wakubwa.

Badala ya kuwa Walinzi wa Amani wamekuwa WAHALIFU
Ngoja tuone ile Tume ya haki ya Rais Samia itakuja na majawabu gani
 
Back
Top Bottom