"Askari" aonekana akimwekea Davis Mosha kitu mfukoni

"Askari" aonekana akimwekea Davis Mosha kitu mfukoni

Hivi sheria zinasemaje!? Hawatakiwi wawe na vitambulisho hawa,!? Hawatakiwi wavioneshe kabla ya kufanya chochote!? Hwatakiwi wawe na search warranty!? Au mimi ndo sielewi!? Kama walikuwa navyo vyote hivyo imekuaje kuaje mpaka wakaanza kushikana mashati na huyo Mosha!?
 
Mosha kaleta ubabe wa kipumbavu sana. Somtym kuwa na Vijisenti ukakosa busara na hekima ndio matokeo yake. Hizo dhahania za kuwekewa vitu mfukoni ndio matokeo ya jazba zake alipaswa aonyeshe busar si upimbi huo. Vijana watamnyonyoa mpaka wapate vibanda vyao sasa.
 
Asante Field Marshall1,

Aisee, una macho makali sana. Nimeona, kwanza aliingiza mkono wake mfukoni, akautoa akiwa amefumba viganja, halafu kwa ujanja ukajifanya anamsukuma Mosha huku mkono ule uliofumbwa akiuingiza mfukoni mwa Mosha. Hakika huyu jamaa ni yule yule aliyemtolea Nappe bastola.

Mh. Sana Rais Magufuli, haya mambo yaendeko siko. Inawezekana unampenda sana Makonda, lakini mambo anayoyafanya kwa raia wako, yanaharibu kabisa sifa njema uliyo nayo na bidii yako ya kuwakomboa watanzania.

Pamoja na kuwa huyu umpendae anatumi watu wasiojulikana au usalama wa taifa, mwiso wa yote wewe ndiye amiri jeshi wa majeshi yote hapa nchini. Haiwezekani ukampenda sana mtu mmoja na kumwacha aangamize watanzania wengi namna hiyo kwa faida yake binafsi. Naamini watu wako wanasoma jamii forum na hivyo watakufikishia ujumbe huu.

Naandika haya kwa uchungu na kwa nia njema, lakini kama utaamua kuniangamiza na mimi pia, sina la kufanya kwani uamuzi ni wako. Lakini mwisho wa yote, sote tutakufa na kuiacha dunia hii. EE MUNGU NISAIDIE! Kilangila.
Mbona unasema vzri ila kwa uoga wa hari ya juu.....kunahaja yakua tayari kujitoa sadaka kwa kukemea mahovu.....wa tanzania tuache kulialia hatuta nshi milele.
 
Kupitia huyu tunapata picha kwamba wapo watanzania wengi wanateseka kwa kesi za kubambikiwa kama hizi. Ikigundulika ukweli kwenye hili, itakua vyema mahakama ikachukua hatua kali dhidi ya hao maafisa na mkuu wao wa operation ili iwe fundisho.
 
Tanzania ipo zaidi ya miaka million ijayo tuache uonevu na ubinafsi tufanye mambo kwa wakati
 
Kwanini uzuie Maafisa Uhamiaji kufanya kazi zao Kama huna tatizo?
Mosha kaleta ubabe wa kipumbavu sana. Somtym kuwa na Vijisenti ukakosa busara na hekima ndio matokeo yake. Hizo dhahania za kuwekewa vitu mfukoni ndio matokeo ya jazba zake alipaswa aonyeshe busar si upimbi huo. Vijana watamnyonyoa mpaka wapate vibanda vyao sasa.
Sawa Mosha ana ubabe wa kipumbavu na kwanini azuie Maafisa Uhamiaji kufanya kazi zao, lakini je mna maoni gani na mashaka ya mleta mada kwamba huyo jamaa kaweka kitu mfukoni mwa Mosha?

Ukiangalia, unaona wazi jinsi huyo askari anavyoingiza mkono mfukoni mwake kisha anaenda kumbana Mosha upande wa kushoto!!
 
Tumesikia kuwa Davis Mosha alipelekwa polisi.....Ninahisi kuwa aidha walimtilia bangi au Dawa za kulevya au simu waliyosema aliwanyang'anya wao. Aliyevaa shati la kijivu anafanana na yule aliyemtolea Nape Nnauye bastola mwaka jana.



Hivi huo mtalaala wa askari wetu kujenga uhasama na raia ulitungwa na nani na kwa faida ya nani?
 
Ukiangalia, unaona wazi jinsi huyo askari anavyoingiza mkono mfukoni mwake kisha anaenda kumbana Mosha upande wa kushoto!!


Hizo mbinu walisoma zamani kabla ya tekinolojia na wao wanaendelea kuzitumia ka kukariri bila kujua teknolojia inawaumbua, kwa mwendo huo kamwe hatutafika maana ni full mawazo mgando
 
Back
Top Bottom