Asante Field Marshall1,
Aisee, una macho makali sana. Nimeona, kwanza aliingiza mkono wake mfukoni, akautoa akiwa amefumba viganja, halafu kwa ujanja ukajifanya anamsukuma Mosha huku mkono ule uliofumbwa akiuingiza mfukoni mwa Mosha. Hakika huyu jamaa ni yule yule aliyemtolea Nappe bastola.
Mh. Sana Rais Magufuli, haya mambo yaendeko siko. Inawezekana unampenda sana Makonda, lakini mambo anayoyafanya kwa raia wako, yanaharibu kabisa sifa njema uliyo nayo na bidii yako ya kuwakomboa watanzania.
Pamoja na kuwa huyu umpendae anatumi watu wasiojulikana au usalama wa taifa, mwiso wa yote wewe ndiye amiri jeshi wa majeshi yote hapa nchini. Haiwezekani ukampenda sana mtu mmoja na kumwacha aangamize watanzania wengi namna hiyo kwa faida yake binafsi. Naamini watu wako wanasoma jamii forum na hivyo watakufikishia ujumbe huu.
Naandika haya kwa uchungu na kwa nia njema, lakini kama utaamua kuniangamiza na mimi pia, sina la kufanya kwani uamuzi ni wako. Lakini mwisho wa yote, sote tutakufa na kuiacha dunia hii. EE MUNGU NISAIDIE! Kilangila.