"Askari" aonekana akimwekea Davis Mosha kitu mfukoni

"Askari" aonekana akimwekea Davis Mosha kitu mfukoni

Swali: Hao maofisa kabla ya kwenda walijua kabisa kuwa ni lazima Mosha atafanya vurugu, na kuwasukuma sukuma hivyo watapata muda wa kumwekea kitu mfukoni wakati wa vurugu?
Kwanini wajue kwamba lazima angefanya vurugu?!

Askari anaweza kukuwekea kitu mfukoni hata usipofanya vurugu kwa sababu anaweza kutekeleza dhamira kwa mbinu mbalimbali kama vile kukunja suruali na kukulazimisha kwenda/kutembea hata kama hukufanya ukaidi kutembea pasipo na shuruti!
 
Naaminisha ya kuwa huwezi kuweka kitu kizembe na alovaa suruali asikugundue
Kwa Hiyo hata Mosha mwenyewe hawezi kuweka kitu mfukoni mwake?
Yaani akitaka kuweka Simu, funguo ya gari, pesa etc atashindwa?
 
Kuna mjuzi kanijuza ya kuwa ule ni aina ya ukaguzi wa kiasikali wanapopambana na mtu ambaye hawajui kama ana siraha au hana
Hoja sio kama alifanikiwa kuweka au hapana bali hoja ni dhamira ya huyo jamaa!! Hoja yako ni sahihi, kutokana na suruali ya Mosha kubana, inawezekana zoezi lilishindikana lakini je, si inaonesha alikuwa na hiyo nia?
 
Uko sawa kabisa, ila katika kufananisha kidogo kuna mushkeli... yule jamaa unasema alimtolea nape bastola ni mrefu kidogo kuzidi huyo lakini pia yule mwili wake ni wa mazoezi(amekaza) huyu wa hapo ana mwili wa ubonge/kitambi.
 
Kwani miongoni mwa mashitaka ya D Mosha alokamatiwa umesikia amekutwa na kitu kisichotakikana? Nimeangalia vizuri hiyo video na kwa kubana kwa suruali ile huwezi wekewa kitu na usistuke.
Wataalqm wanasema Askari alikua anamkagua aone kama ana siraha maana Davis alikua kapaniki sanaa.

NB siko hapa kumtetea Askari
Ukiangalia kwa makini huyo mwenye shati la kijivu ametoa kitu mfukoni kwake akamsogelea Davis Mosha (Akajiweka upande kwa upande au kwa kiingereza "side by side" Kwa mkono wa kulia ambao aliufunga/aliukunja alipoutoa mfukoni mwake akaingiza kwenye mfuko wa suruali wa kushoto wa suruali wa Davis Mosha wakati huo akitumia mkono wa kushoto kumsukuma Mosha. Ukiangalia kwa makini mkono wa kulia wa huyo "askari"baada ya kuuingiza mfukoni kwa Davis Mosha akautoa ukiwa hauna kitu (Tofauti na mwanzo) halafu akatumia mikono yake miwili kumsukuma Mosha. Angalia kwa makini alichokuwa akifanya...kuwa "Detail oriented" Suruali kubana siyo tatizo kwa sababu si lazima alichowekewa siyo lazima kiwe kikubwa pia kumbuka hiyo suruali Davis Mosha anatumia hiyo mifuko ya suruali aidha kuwekea walet au inatosha pia kuweka mikono yake, hivyo suruali kubana siyo tija. Hapo yeyote mwenye macho na akili timamu anaona kilichotokea. Hapo ni simply kubambikiza....Hiyo system ya kubambikiza siyo ngeni hapa Tanzania hao polisi uchwara na polisi wa kawaida ni kitu wanachofanya siku zote. LINI HUU UONEVU UTAKWISHA?
 
Davis aliingia kichwa kichwa baada ya kukutana na mtaalamu wa social media networks. Aliinvest hela nyingi kuanzisha Swahili TV. Baada ya Mitambo kufika ndipo alipogundua mtaalamu aligraduate kutoka local library of Brooklyn.
hahahaahaa nimecheka..eti local library of Brooklyn
 
Kwan hii tábua ya maafisa wanapokwenda kufanya kazi kuambatana na cameraman umeanza lin lkn
 
Swali: Hao maofisa kabla ya kwenda walijua kabisa kuwa ni lazima Mosha atafanya vurugu, na kuwasukuma sukuma hivyo watapata muda wa kumwekea kitu mfukoni wakati wa vurugu?
Hoja yako hasa nini? Tayari nimeshatoa maelezo kama third part lakini naona unataka nitoe maelezo kama miongoni mwa waliokuwa kwenye tukio! Huwezi kuniuliza ikiwa hao maofisa walijua kabisa kwamba Davis Mosha angefanya vurugu wakati mimi sio miongoni mwa hao maofisa!
 
Hizo mbinu walisoma zamani kabla ya tekinolojia na wao wanaendelea kuzitumia ka kukariri bila kujua teknolojia inawaumbua, kwa mwendo huo kamwe hatutafika maana ni full mawazo mgando

Asante digital unaumbuka mcha kweupee chezea smartphone ww.
 
Back
Top Bottom