Ukiangalia kwa makini huyo mwenye shati la kijivu ametoa kitu mfukoni kwake akamsogelea Davis Mosha (Akajiweka upande kwa upande au kwa kiingereza "side by side" Kwa mkono wa kulia ambao aliufunga/aliukunja alipoutoa mfukoni mwake akaingiza kwenye mfuko wa suruali wa kushoto wa suruali wa Davis Mosha wakati huo akitumia mkono wa kushoto kumsukuma Mosha. Ukiangalia kwa makini mkono wa kulia wa huyo "askari"baada ya kuuingiza mfukoni kwa Davis Mosha akautoa ukiwa hauna kitu (Tofauti na mwanzo) halafu akatumia mikono yake miwili kumsukuma Mosha. Angalia kwa makini alichokuwa akifanya...kuwa "Detail oriented" Suruali kubana siyo tatizo kwa sababu si lazima alichowekewa siyo lazima kiwe kikubwa pia kumbuka hiyo suruali Davis Mosha anatumia hiyo mifuko ya suruali aidha kuwekea walet au inatosha pia kuweka mikono yake, hivyo suruali kubana siyo tija. Hapo yeyote mwenye macho na akili timamu anaona kilichotokea. Hapo ni simply kubambikiza....Hiyo system ya kubambikiza siyo ngeni hapa Tanzania hao polisi uchwara na polisi wa kawaida ni kitu wanachofanya siku zote. LINI HUU UONEVU UTAKWISHA?