Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,067
- 10,938
Nakumbuka mwaka 2020 aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamis Kigwangalla alimtuhumu aliyekuwa Meya wa Iringa kuwa ametenda kosa la ujangili baada ya kupakia picha kwenye mtandao wa Twitter akiwa amemuua nyoka aina ya chatu. Zaidi soma Dtk. Kigwangalla amtuhumu Alex Kimbe kwa ujangili baada ya kuua chatu
Leo nimekutana na video ikimuonesha Askari wa JWTZ akiwa anajinadi kwa kumuua nyoka mkubwa aina ya chatu. Ukimsikiliza vizuri utagundua kwamba nyoka huyo hakuwa katika mazingira ya kuleta madhara yoyote kwa binadamu, ni kwamba alikuwa katika mazingira yake ya maisha ya kila siku. Kitendo cha Askari huyo kumuua bila sababu za msingi si kitu cha kufumbia macho.
Nyoka mkubwa kama yule anachukua muda mrefu kufikia ukubwa ule, na pia anapitia katika mazingira hatari tokea kuanguliwa ikiwa pamoja na kuwindwa na wanyama wengine hatari. Anapoweza kukabiliana na hatari zote mpaka kufikia ukubwa ule ni suala la kushukuru.
Huyu Askari angetumia busara hata kuwaita maafisa wanyama pori waje kumchukua, mnyama kama huyu ni kivutio kikubwa sana cha utalii, anaweza akaleta mapato makubwa sana akiwekwa kwa snake park