Askari Mgambo tunaowategemea kulinda mali zetu, wamekamatwa kwa tuhuma za wizi

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
Jeshi la Polisi mkoani Lindi linawashikilia askari mgambo wawili kwa tuhuma za kuhusika na wizi wa mali mbalimbali, ikiwemo mali za raia mmoja anayeishi katika Manispaa ya Lindi.

Waliohusika ni Karimu Athuman Omari (29), askari mgambo namba MG. 512421, mkazi wa mtaa wa Raha Leo, na Zawadi Swedi Mohamed (22), askari mgambo namba MG. 624773, mkazi wa Mtanda – wote wakihudumu katika ulinzi maeneo ya Manispaa ya Lindi.

Kwa mujibu wa taarifa ya Polisi, watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa na mali zinazodaiwa kuibwa kutoka kwa Anita Patel, mkazi wa eneo la Sokoine, ambapo tukio hilo liliripotiwa kutokea majira ya saa 4 usiku.

Katika mahojiano, watuhumiwa walikiri kuhusika na wizi huo, wakieleza kuwa walitekeleza uhalifu huo katika nyumba ya mlalamikaji, iliyo jirani na makazi ya mtumishi wa TANESCO ambaye alikuwa akiwatumia kama walinzi wake binafsi.

Upekuzi uliofanywa na Polisi ulibaini si mali za Anita Patel pekee zilizopatikana, bali pia mali nyingine zinazodhaniwa kuibwa kutoka maeneo tofauti.

Kutokana na tukio hilo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Lindi limewataka wananchi waliopotelewa au kuibiwa mali kufika Kituo Kikuu cha Polisi Lindi kwa ajili ya utambuzi wa mali zilizookolewa.

Polisi wamesisitiza kuwa uchunguzi unaendelea na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wote watakaobainika kuhusika na matukio ya wizi au uhalifu mwingine.

1757507980841.png
 
Kula kwa urefu wa unapofikia
1757512065666.gif
 
Ndugu zangu wa Jeshi la akiba mmeniaibisha sana mimi mgambo mwenzenu mwaminifu.
 
Jeshi la Polisi mkoani Lindi linawashikilia askari mgambo wawili kwa tuhuma za kuhusika na wizi wa mali mbalimbali, ikiwemo mali za raia mmoja anayeishi katika Manispaa ya Lindi.

Waliohusika ni Karimu Athuman Omari (29), askari mgambo namba MG. 512421, mkazi wa mtaa wa Raha Leo, na Zawadi Swedi Mohamed (22), askari mgambo namba MG. 624773, mkazi wa Mtanda – wote wakihudumu katika ulinzi maeneo ya Manispaa ya Lindi.

Kwa mujibu wa taarifa ya Polisi, watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa na mali zinazodaiwa kuibwa kutoka kwa Anita Patel, mkazi wa eneo la Sokoine, ambapo tukio hilo liliripotiwa kutokea majira ya saa 4 usiku.

Katika mahojiano, watuhumiwa walikiri kuhusika na wizi huo, wakieleza kuwa walitekeleza uhalifu huo katika nyumba ya mlalamikaji, iliyo jirani na makazi ya mtumishi wa TANESCO ambaye alikuwa akiwatumia kama walinzi wake binafsi.

Upekuzi uliofanywa na Polisi ulibaini si mali za Anita Patel pekee zilizopatikana, bali pia mali nyingine zinazodhaniwa kuibwa kutoka maeneo tofauti.

Kutokana na tukio hilo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Lindi limewataka wananchi waliopotelewa au kuibiwa mali kufika Kituo Kikuu cha Polisi Lindi kwa ajili ya utambuzi wa mali zilizookolewa.

Polisi wamesisitiza kuwa uchunguzi unaendelea na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wote watakaobainika kuhusika na matukio ya wizi au uhalifu mwingine.

Kusini kuna shida gani?

Wale Polisi wa Mtwara waliohukumiwa juzi nao waliua ili wapoteze ushahidi wa wizi waliofanya.

Bado tusikie wazee wa karanga.
 
Back
Top Bottom