Askari mstaafu: Walichofanya Mdee na wenzake pale Segerea ni sawa na Gari kugonga Treni kwenye "Railway cross Road"

Mm huwa narudia rudia kila siku humu, ikiwa akili na tabia za viongozi wa CHADEMA ndio kama za akina Halima, Bulaya, ujue wafuasi/followers wao ni nusu mfu, haiwezekani kabisa uwe kiongozi tena mbunge ambaye anajua kabisa sheria alafu unaenda kuleta vurugu, fujo na kuvamia geti la magereza huku ukijua hilo ni kosa kubwa sana. Je wangewashinda Askari magereza nguvu sbb walikuwa wengi na wafungwa wa magereza wangetoka na kukimbia ingekuwaje? Hili ni kosa kubwa sana haihitaji hata mtu kuwa mwanasheria kujua hili. Hii ni sawa kuvamia kituo cha polisi ukiwa na wafuasi 27 na kuanza kupambana na maskari walioko kituoni. Upumbavu usio na mfano huu, wamedekezwa sana akina Halima, ingekuwa mm ndio IGP, hiiiiii, haiwezekani mtu utoke huko na wafuasi hadi 27 alafu unavamia magereza lenye wafungwa kadhaa, haiwezekani, kisa unajiona mwanamke unatumia gender kama kinga labda usipigwe, nasema mm ningepiga hadi namdandia mgongoni, pumbaf Halima ww, umeonyesha hufai hata kidogo kuwa kiongozi, adhabu yao najua itakuwa kali sana, tusubiri 😡😡
 
Nimekuelewa sana bwashee!
Shia ya wanasiasa wengi wanadhani wao ndiyo wenye akili ya kuongoza wananchi wote badala ya kusikiliza kwetu pia.

Binafsi nashauri sana chadema ila hawasikii kutegemea public sympathy bila kujua namna ya kuitumia hasa kwenye mazingira genuine itawaumiza na kuwaangusha sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lawama zinaenda kwa watu wa Chadema. Ingawa hatujasikia upande wa pili wa wahanga naogopa kusema viongozi wa chadema walipaswa kusoma alama za nyakati na kumpisha mwanaharamu. Umeenda nyumbani kwa jirani na fujo ikatokea vyo vyote wewe uliyekuja ndio utaonekana kufanya fujo. Magereza ni hiyo hiyo lakini wengine walitoka kwa amani, kwanini safari hii ya kumtoa Mbowe kutokee vurugu?
Wakati mwingine tujifunze kufanya tathmini ya kila matukio na kuyajadili kama chama ili tuonyane tunapokosea kwani tayari tunamjua adui yetu. Wakati mwingine ni kupisha mihemuko ili twende salama sio kila siku tuonekane tunalia lia kwani itafika mahali hata sympathisers wetu watachoka na kutupuuza. Hakukuwa na sababu ya makamnda kuumizwa vile. Tungeweza kuchukua tahadhari.
 
Nimekwambia si kila jambo limetungiwa sheria, wala nchi haiongozwi na sheria pekee usipotambua hili ujue bado una kibarua cha kujifunza mengi kuhusu uongozi na utawala.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya mambo uki tazama kishabiki Huwezi kuona Nani ame kosea
Ila Ukitazama kwa mtazamo bila kufunga maana na upande unaweza kuwa na vitu muhimu Sana.

Na ishia hapa



Sent using Jamii Forums mobile app
 
 

Attachments

  • 2020-03-15-17-12-25-431878677.jpg
    9.7 KB · Views: 14
Hawana cha kusema zaidi kutambua makosa too late.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
johnthebaptist ,

..mimi naamini umati uliokwenda kumchukua Mh.Mbowe ulikuwa umati wenye FURAHA.

..sidhani kama walikwenda Magereza kuleta shari, kumpiga mtu, au kuharibu mali.

..that was a happy and jubilant crowd.

..huenda askari wetu wametumwa, au wana CHUKI fulani dhidi ya CDM.

..haiwezekani CDM wawe ktk hali ya FURAHA halafu atokee askari aanze kuwapiga karibia kuwauwa.
 
Mkuu hata unapo kuja kwangu unakuwa una amri wala sheria uzitakazo wewe...
Ukizingua kama walivyo zingua naku tandika haswa..
 
Jeshini hawafanyi kazi kwa hisia ni Kanuni, Taratibu na Amri, ukishindwa kufuata kanuni na taratibu unapewa amri usipotii ni kukusurutisha na kipigo juu kufuata amri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kina Halima walikosa intelligensia ya kung’amua madhara. Pole zao, tunawaombea wapone ili waendelee na kesi ya uvamizi na kuchana sare ya askari
waliingizwa chaka, nasikia geti la kwanza lilifunguliwa la pili wakagoma hivyo wakawa ndani ya Himaya ya Segerea. Mdee ajue hii ni Nchi nyingine sio enzi zile za Dhaifu
 
Magari ndio huchakazwa!
Huyo ni mbumbumbu wa sheria. Hajui hata anachosema!
Hawezi hata kusema ni kifungu kipi cha sheria kilichovunjwa! Isitoshe hata kama walifanya ghasia kama Magereza wanavyojaribu kujitetea, jukumu lao lilikuwa kuwadhibiti, kuwaweka chini ya ulinzi na kuwashtaki, si kuwapiga, kuwadhalilisha na kuwajeruhi vibaya!
Kufananisha tukio hilo na vivuko vya Reli ambapo Operetta hana uono wa kilicho mbele yake ni sawa na kusema maaskari wetu hawana uwezo wa kufikiri na kupambanua hatua stahiki kwa tukio husika! Huo ni ukosefu mkubwa wa weledi (unprofessional) na ni 'mechanical thinking'! Mahali hapo hapo Polepole alikwenda na kundi la watu wakiwemo waandishi na hakufanywa lolote. Yeye yuko juu ya sheria? Au ndiyo matumizi ya dola aliyotuambia Bashiru?
Maaskari wafahamu kuwa wanasiasa hawa wanaojaribu kuwafurahisha watawaruka siku mambo yakienda kombo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uzuri tabia zao zinajulikana kuanzia bungeni kwa kupenda kulazimisha mambo.

Sugu aliwahi kubebwa msobe msobe na askari kumtoa ndani ya ukumbi wa bunge na walipofika nje walimtupa kama gunia na kumtimbatimba

Askari hafundishwi kazi na raia bwashee!
 
Jeshi linatenda kwa mujibu wa sheria, kanuni, utaratibu na amri.

Wanajua wanachofanya pale gerezani siyo sawa na mitaani manzese na Tandale bwashee!
Wapuuzi tu,wanakuwa driven kisiasa!Awamu hii hakuna weledi wowote katika majeshi yetu!Sio ajabu kuona hata CDF akizungumzia maandamano,shame!
 
nchi ambayo think-tanks wake ni Bashite & Musiba mambo yake ndiyo yanakuwa hivi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…