Askari mstaafu: Walichofanya Mdee na wenzake pale Segerea ni sawa na Gari kugonga Treni kwenye "Railway cross Road"

Askari mstaafu: Walichofanya Mdee na wenzake pale Segerea ni sawa na Gari kugonga Treni kwenye "Railway cross Road"

Nj
Huyo ni mbumbumbu wa sheria. Hajui hata anachosema!
Hawezi hata kusema ni kifungu kipi cha sheria kilichovunjwa! Isitoshe hata kama walifanya ghasia kama Magereza wanavyojaribu kujitetea, jukumu lao lilikuwa kuwadhibiti, kuwaweka chini ya ulinzi na kuwashtaki, si kuwapiga, kuwadhalilisha na kuwajeruhi vibaya!
Kufananisha tukio hilo na vivuko vya Reli ambapo Operetta hana uono wa kilicho mbele yake ni sawa na kusema maaskari wetu hawana uwezo wa kufikiri na kupambanua hatua stahiki kwa tukio husika! Huo ni ukosefu mkubwa wa weledi (unprofessional) na ni 'mechanical thinking'! Mahali hapo hapo Polepole alikwenda na kundi la watu wakiwemo waandishi na hakufanywa lolote. Yeye yuko juu ya sheria? Au ndiyo matumizi ya dola aliyotuambia Bashiru?
Maaskari wafahamu kuwa wanasiasa hawa wanaojaribu kuwafurahisha watawaruka siku mambo yakienda kombo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli Polepole alikwenda pale na watu je alikiuka taratibu za kuingia gerezani? Alitumia mabavu? Kusema ni kifungu kipi kimevunjwa subiri hati ya mashitaka itoke kwa mwanasheria. Ila usimpuuze huyu mzee maana gari moshi ligongwa na gari...Pia usimdharau maana humjui.
 
Jeshini hawafanyi kazi kwa hisia ni Kanuni, Taratibu na Amri, ukishindwa kufuata kanuni na taratibu unapewa amri usipotii ni kukusurutisha na kipigo juu kufuata amri.

Sent using Jamii Forums mobile app

..Nakubaliana na wewe.

..lakini Magereza hawakutumia kanuni na taratibu wakati ccm wanamtoa Dr.Mashinji na walipojaribu kumtoa Mch.Msigwa.

..Magereza wangewaruhusu CDM kumtoa mwenyekiti wao kwa utaratibu uliotumiwa na CCM kumtoa Dr.Mashinji tabu yote hii isingetokea.

..Zoezi hili lilikwenda vizuri kwa vyama vyote kwanini liharibiwe dakika za mwisho, wakati mfungwa wa mwisho, Mh.Mbowe, anatolewa?
 
Wee mjing### unahangaika sana
Afisa mstaafu wa jeshi la magereza ndugu Mwakibinga amenieleza kuwa kilichotokea pale Segerea kati ya akina Halima Mdee na askari walinzi wa gereza ni sawa kabisa na Gari kugongana na Treni kwenye eneo ambalo Reli imevuka barabara " Railway cross Road"

Vyovyote itakavyokuwa tafsiri ni moja tu uwapo eneo la gereza raia unapaswa kuheshimu na kutii maelekezo yote unayopewa na askari au maofisa magereza na si vinginevyo anasema Mwakibinga.

Hata upelelezi wa matukio ya namna hauwezi kuchukua zaidi ya dakika 30 kwa sababu utaratibu wa Magereza kwa wageni uko wazi kabisa, amemalizia Mwakibinga.

Binafsi bado natafakari hii ya " Railway cross Road" mara nyingi magari ndio huchakazwa chakari na kesi hubebeshwa wao, kweli mwenye nguvu mpishe.

Maendeleo hayana vyama!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bwashee mtu akikusimulia jambo usimuache bila kumuuliza hivyo vifungu, ukimuacha na kukimbilia kutundika uzi huku na sisi wasomaji tutakuuliza wewe juu ya vifungu hivyo.
Kifungu cha Railway cross Road mbona kinajulikana bwashee!
 
Uzuri tabia zao zinajulikana kuanzia bungeni kwa kupenda kulazimisha mambo.

Sugu aliwahi kubebwa msobe msobe na askari kumtoa ndani ya ukumbi wa bunge na walipofika nje walimtupa kama gunia na kumtimbatimba

Askari hafundishwi kazi na raia bwashee!

..chanzo cha yote haya ni UPENDELEO kwa ccm.

..kukumbushia ya bungeni unazidi kutetea hoja yangu.

..rejea tukio la Mh.Mnyika kutolewa bungeni na askari na baadae kuadhibiwa na Spika.

..Mh.Mnyika alikuwa anamlalamikia Spika kwa kutomchukulia hatua mbunge wa ccm aliyemtukana.

..lakini kilichotokea ni Spika kumuadhibu Mnyika.

..Again, tatizo na chanzo cha yote haya ni UPENDELEO kwa chama cha mapinduzi.
 
..tatizo Magereza na Polisi waliruhusu msafara wa Polepole kuingia ndani ya gereza na kumchukua Dr.Mashinji. wakarudia tena walipojaribu kumchukua / kumtorosha Mch.Msigwa.

..siyo busara kuruhusu CCM kufanya jambo fulani, halafu CDM wakifanya jambo hilohilo wanapigwa karibia ya kuuwawa.

..chanzo cha yote haya ni vyombo vya dola / ulinzi na usalama kupendelea waziwazi chama cha mapinduzi.
Mimi sijawahi kuwaita CHADEMA nyumbu! Lakini kwa hoja yako hii ya CCM walienda kumlaki Mashinji hivyo lazima CHADEMA wamwendee Mbowe basi sisemi kama ni nyumbu au siyo!
 
Wakati mwingine mtambue kuwa si sheria tu zinazoongoza nchi..! Kuna amri, maelekezo si kila jambo hapa nchini limetungiwa sheria.

Katika hili Chadema walichemka jeshini wanatumia zaidi amri si sheria kwenda kubishania gerezani kuliko fanywa na akina Mdee na yaliwapata ni haki yao.

Lakini pia waneshindwa kujitathimini na kuwa na mikakati mipya ya kufanya siasa shindani ndani ya mazingira kinzani.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hizo amri wanazo toa wanatoa bila kuwepo sheria inayowaruhusu kutoa amri zao hizo?.
 
tulishawajua tangu zamani,serekali ya CCM mkosaji ni mpinzani siku zote,hata kama atafanya kilekile ambacho CCM wanakifanya, wapinzani ndiowataonekana kuwa wamevunja sheria wakati wamepita njia ileile na kufanya kilekile kilichofanywa na CCM.
 
Hii tabia ya kupenda kukandamizana ni moja ya sababu kubwa hatuendelei.

Na mkiendelea kusifia ujinga hivi mtakuwa masikini wajinga daima.

Sent from my typewriter using Tapatalk

Exactly,

Mkuu Kiranga bila kujali itikadi yoyote miaka ya karibuni kumeibuka aina ya reasoning ya “kimbayuwayu” ambapo huwa tunadhani maendeleo na usawa/ustawi wa binafamu vinahawanyika.
 
Exactly,

Mkuu Kiranga bila kujali itikadi yoyote miaka ya karibuni kumeibuka aina ya reasoning ya “kimbayuwayu” ambapo huwa tunadhani maendeleo na usawa/ustawi wa binafamu vinahawanyika.
Kuna wajinga wanasifia kuvunjwa kwa haki magerezani leo.

Kama vile wanajua kesho yao itakuwa vipi.

Sent from my typewriter using Tapatalk
 
Hayo ni matumizi mabaya ya dola aliyosema bashiru. Waliochana sare ya askari ni mapandikizi ya ccm.
Toka lini au ulisikia wapi siasa zinaenda kufanywa gerezani tatizo la upinzani wanataka sana watanzania na dunia nzima iwaonee huruma au wahalalishe uvunjaji wa sheria kisa tu ni wanasiasa wana haki ya kufanya demokrasia !
 
Wakati mwingine mtambue kuwa si sheria tu zinazoongoza nchi..! Kuna amri, maelekezo si kila jambo hapa nchini limetungiwa sheria.

Katika hili Chadema walichemka jeshini wanatumia zaidi amri si sheria kwenda kubishania gerezani kuliko fanywa na akina Mdee na yaliwapata ni haki yao.

Lakini pia waneshindwa kujitathimini na kuwa na mikakati mipya ya kufanya siasa shindani ndani ya mazingira kinzani.

Sent using Jamii Forums mobile app
Eti hawana mikakati, kama watu wananyimwa haki yao ya kikatiba kufanya kazi za kisiasa jaribu kutumia akili hata kwa asilimia moja
 
Afisa mstaafu wa jeshi la magereza ndugu Mwakibinga amenieleza kuwa kilichotokea pale Segerea kati ya akina Halima Mdee na askari walinzi wa gereza ni sawa kabisa na Gari kugongana na Treni kwenye eneo ambalo Reli imevuka barabara " Railway cross Road"

Vyovyote itakavyokuwa tafsiri ni moja tu uwapo eneo la gereza raia unapaswa kuheshimu na kutii maelekezo yote unayopewa na askari au maofisa magereza na si vinginevyo anasema Mwakibinga.

Hata upelelezi wa matukio ya namna hauwezi kuchukua zaidi ya dakika 30 kwa sababu utaratibu wa Magereza kwa wageni uko wazi kabisa, amemalizia Mwakibinga.

Binafsi bado natafakari hii ya " Railway cross Road" mara nyingi magari ndio huchakazwa chakari na kesi hubebeshwa wao, kweli mwenye nguvu mpishe.

Maendeleo hayana vyama!
Na pole pole je?
 
I wish i could be ofisa magereza, kuna mtu angekatwa kiuno, maana hawa nyumbu hawishagi matusi, na mara nyingi wanafanyaga kwa masifa waonekane kua makamanda na hawaogopi, ndio maana walivtoka gerezan walikua wanajigamba wamekiwasha na wanaogopeka, SIFA ZA KIJINGA, sasa dawa yao ni kuwavunja meno na viuno ili kila wakiona majeraha watambue walikosa kutafuta misifa mbele ya askari

Sent using Jamii Forums mobile app
Akili za kiafrika katika ubora wake
 
Back
Top Bottom