Unajua USA ni nchi ambayo haina mwenyewe...Wote ni wahamiaji...wenye nchi ni wahindi wekundu ' Red Indians' ambao waliuawa katika mauaji ya kikatili mno...waliobaki hivi Sasa wanaishi kwenye 'zones' zilizotengwa..yaani wahindi wekundu wako kwenye maeneo Kama zoo ...sitaki kuingia kwa undani kwani ni historia inayotisha., Wamarekani wenyewe huwa hawataki kulizungumzia hili kwani walifanya ukatili wa kutisha ...kwa hiyo Marekani kuna whites kwa maana ya wazungu kutoka England, Ujdrmani, Ireland, Italy, Spaniards, Eastern Europe, na kadhalika...wako pia kutoka Latin America...Wapo waasia Kama wahindi, wachina na kadhalika...Halafu Wapo blacks...makundi yote Yana watu in millions...Trump mwenyewe inasemekana asili yake ni Ujerumani, Clinton nadhani asili yake ni Irish Kama sijakosea..Obama tunajua asili yake ni Kenya kwa maana ya Afrika...Sasa swali lako lilikuwa je civil war itakuwa baina ya makundi yapi? Binafsi Sijui...wako wachambuzi wanaosema kuwa inaweza ikawa baina ya states...kwa mfano inaelezwa kuwa California wako wanaotaka ijitenge...wengine wanasema inaweza ikawa Kati ya masikini na matajiri..wengine wanasema Kati ya 'ethnic groups'...Tusisahau kuwa iliwahi kutokea civil war huko USA miaka kadhaa ya nyuma Kati ya North na South...Sina jibu rshisi kwa swali lako zuri...