Kimeumana....... waliona sifa kukiweka chama cha magundu madarakani, sasa wanajipukutisha tu wenyewe.
Anaandika Ndugu MalisaGJ
TATIZO LA KUJIUA KATIKA JAMII
"Kwako mke wangu
(Mama Derick). Naomba nisamehe sana kwa maamuzi haya. Maisha kwangu hayana maana tena, nisamehe sana. Nimejitahidi nimeshindwa naomba uwatunze watoto wetu” sms ya mwisho ambayo Sajenti William Giriango Chacha (40) askari wa JWTZ alituma kwa mkewe, dakika chache kabla ya kujinyonga kwa mkanda wa suruali huko Dodoma.
#MyTake:
1. Tatizo la afya ya akili ni kubwa sana kwenye jamii zetu kuliko tunavyofikiri. Kuna haja ya serikali, wadau mbalimbali (NGOs) na jamii kwa ujumla kuchukua hatua za makusudi za kukabiliana na tatizo hili.
2. Ukipata tatizo hata liwe kubwa kiasi gani jitahidi kuzingumza, usikae kimya. Kuzungumza kunapunguza risk ya kufanya maamuzi mabaya ikiwemo kujidhuru.
3. Hakuna binadamu ambaye ni bingwa wa matatizo. Uwe tajiri, maskini, mnene, mwembamba shida haichagui. Hakuna watu majasiri kama wanajeshi. Lakini pamoja na ujasiri wake, Sajenti Chacha ameshindwa kuonesha ujasiri huo kwenye matatizo, hatimaye ameruhusu matatizo yamshinde.
4. Kujiua kwa sababu ya matatizo ni kuwaachia matatizo makubwa zaidi uliowaacha. Mke na watoto wa Chacha wanaenda kukabiliana na changamoto nyingi za maisha baada ya baba yao kujiua, kuliko changamoto walizokua nazo baba yao akiwa hai.
5. Kama unaipenda familia yako, mkeo, watoto, na ndugu zako, usijiue. Kujiua ni ubinafsi. Kujiua ni njia rahisi ya kumaliza matatizo yako lakini kuacha matatizo makubwa zaidi kwa ndugu zako na marafiki. Kujiua ni kuacha alama ya maumivu isiyofutika kwa familia yako.
6. Matatizo yakikuzidi hakikisha huwi peke yako. Hakikisha unaye wa kumwambia hata kama una uhakika hawezi kukusaidia, we mwambie tu. Kushare matatizo yako ni sehemu ya healing process. Ni psychosocial therapy.!