Askari Polisi kutumia silaha za moto za Automatiki (SMG, ASSAULT RIFLES) siyo sahihi, ni silaha za Kivita

Askari Polisi kutumia silaha za moto za Automatiki (SMG, ASSAULT RIFLES) siyo sahihi, ni silaha za Kivita

Majambazi yanahitaji kupelekewa moto mkali.

Ukimchapa moja haamki, au akiamka anajikuta yuko kwa Yesu.
 
The late mwangosi aliuawa kwa bunduki ya bomu la machozi tu.

Sijui unafahamu nini kuhusu silaha za kivita,ila hiyo silaha vitani inamhusu askari mmoja tu,ambaye matumizi yake hayatofautiani na haya ya askari wa polisi, labda siku ukiwaona na kifaru bank utahoji, hiyo ni silaha ndogo sana ya kivita. Lakini silaha bora sana kwa matumizi yasiyo ya kivita.ndio maana ili kuizatiti zaidi sheria ikakataa kabisa umiliki wa silaha yoyote auto kwa taasisi isiyo ya kulinda usalama na ya kiserikali.

Polisi hawawezi kuwa na vipistol peke yake ambavyo hata watu wenye hela ya kununua iphones wanavyo.
Nadhan Hujaelewa, Dhumuni sio Kumiliki Silaha bali Matumizi yake ni nn? hizi AK47 zinanguvu sana huwez pigwa nayo mwilini ukapona,.. Je nambie Wewe unayeelewa Dhumuni ni kuuwa au Ku neutralize kikwazo?
 
Wazo zuri.

Maana ni amani pale ambapo watu uwezo wa kudhuriana ni mdogo.

Hata kama ni amani zaidi pale hatudhuriani hata kidogo. Lakini tuwe wakweli tufanye kinachowezekana tupunguze uwezo wa kudhuriana

Majambazi wasimiliki auto machines, na mapolisi wasimiliki auto machines✌. Nnajitolea kuwa mwenyekiti wa hii nationwide disarmament ya majambazi na polisi 😂😂
Siraha za Auto watumie pale ambapo panahitaj nguvu ya Kadri, ila kwa ulinzi wa raisa na Doria tutumie tu Pistol
 
Hizo ni nchi za wenzetu na hizo ni tamaduni zao. Nasi kama taifa tunaonesha utofauti wetu, kuwa inawezekana askari polisi kutumia AK 47 na SMG na mambo yakawa Sawa tu.

Pia mfano lile tukio la Hamza imagine wawe saba, utaweza kuwatuliza kwa pistol?
Tukio kama ni kubwa waweza tumia Auto Guns
 
Ukiwa ni mtu ambaye hujawahi kukutana na majambazi wenye SMG na AK47 utatoa ushauri kama huu. Lakini ukikutana na changamoto kubwa ya kukabiliana na jambazi mwenye zana za kisasa na silaha za kivita naamini utatoa ushauri wa kutumia silaha Kali zaidi ya hizi wanazotumia askari polisi za Sasa. Cha msingi ni kuangalia katika kupunguza pengo la maskini na tajiri ndipo watu kujitoa mhanga wa kununua silaha za kivita na kutoka nchi zenye makundi ya waasi na kuja kuzitumia kutafuta fedha kwa nguvu na kutumia silaha! Endelea kuomba mungu siku Moja usishuhudie tukio Hilo na wewe uwe ni miongoni mwa watu waliokuwa wanalengwa kuibiwa na hao wenye silaha maana utaomba kwa lugha zote, dini zote na utakumbuka yote mabaya na mazuri ulofanya, familia yako,mkeo,watoto,mali zako, na mengi ulofanya mpaka wa huo tukio hilo linakutokea maana hutaamini kama watafanikiwa kuwaua wote ili wewe na wenzako mpone maana umetoka kutafuta kihalali na wenzako wanatumia njia ya mkato!!
SMG siyo jina la bunduki ni sifa ya bunduki, AK47 pia ina sifa za bunduki zenye sifa ya SMG na ndo jina la bunduki wanazobeba polisi zinaitwa Ak47 kwahiyo usiseme Ak47 na SMG inakua haileti maana, ni sawa na useme mtu na mrefu , mtu ni kiumbe na mrefu ni sifa
 
Nadhan Hujaelewa, Dhumuni sio Kumiliki Silaha bali Matumizi yake ni nn? hizi AK47 zinanguvu sana huwez pigwa nayo mwilini ukapona,.. Je nambie Wewe unayeelewa Dhumuni ni kuuwa au Ku neutralize kikwazo?
aliyekwambia kwamba inaua popote itakapopiga hakuwa na lengo zuri kwako kielimu.

Maeneo ambayo silaha hii inaweza kuua punde ni kichwani,shingoni,na kifuani.maeneo yaliyobaki yote kuna uwezekano 90% mtu akapona akipigwa hata tumboni.
Wakati wa matumizi askari ameagizwa kuzingatia maeneo chini ya goti ili kuwa na uhakika wa dhana(ku neutralize)
Sasa taja silaha ambayo ni sahihi kwa zoezi hilo la kurenga miguu kati ya hizo unazozifikiria
Shotgun kama za SA haitaki umbali mrefu na ukiitumia umbali mfupi inaondoka mguu kabisa,pistol si tu inataka umbali mfupi lakini na utulivu pia maana sio nzuri ktk shabaha.
 
Hizi bunduki za Automatiki zenye risasi nyingi kama 30+ ni silaha mahususi za Kivita sio za kulinda Raia au Kupigia Doria


Ukiangalia Nchi za wenzetu Police wanatumia Hand Gun kama Pistol ndogo kama Bereta na Glock kwasababu hizi hazina Impact kubwa ukipigwa katika mwili. Ila hizi Mashine Gun ni ngumu kuishi baada ya kupigwa kwasababu ina Impact kubwa sana unapopigwa nayo. Tujikumbushe kwa yaliowahi tokea


Naomba Mamlaka Husika iangazie hili na kulipa uzito ili kuepusha athari za hapa na pale
Wewe jambazi nini ?! Unataka Askari wapewe gobore ili ukija na SMG yako polisi washindwe kupambana na wewe ?!
 
Back
Top Bottom