Askari Polisi kutumia silaha za moto za Automatiki (SMG, ASSAULT RIFLES) siyo sahihi, ni silaha za Kivita

Majambazi yanahitaji kupelekewa moto mkali.

Ukimchapa moja haamki, au akiamka anajikuta yuko kwa Yesu.
 
Nadhan Hujaelewa, Dhumuni sio Kumiliki Silaha bali Matumizi yake ni nn? hizi AK47 zinanguvu sana huwez pigwa nayo mwilini ukapona,.. Je nambie Wewe unayeelewa Dhumuni ni kuuwa au Ku neutralize kikwazo?
 
Siraha za Auto watumie pale ambapo panahitaj nguvu ya Kadri, ila kwa ulinzi wa raisa na Doria tutumie tu Pistol
 
Hizo ni nchi za wenzetu na hizo ni tamaduni zao. Nasi kama taifa tunaonesha utofauti wetu, kuwa inawezekana askari polisi kutumia AK 47 na SMG na mambo yakawa Sawa tu.

Pia mfano lile tukio la Hamza imagine wawe saba, utaweza kuwatuliza kwa pistol?
Tukio kama ni kubwa waweza tumia Auto Guns
 
SMG siyo jina la bunduki ni sifa ya bunduki, AK47 pia ina sifa za bunduki zenye sifa ya SMG na ndo jina la bunduki wanazobeba polisi zinaitwa Ak47 kwahiyo usiseme Ak47 na SMG inakua haileti maana, ni sawa na useme mtu na mrefu , mtu ni kiumbe na mrefu ni sifa
 
Nadhan Hujaelewa, Dhumuni sio Kumiliki Silaha bali Matumizi yake ni nn? hizi AK47 zinanguvu sana huwez pigwa nayo mwilini ukapona,.. Je nambie Wewe unayeelewa Dhumuni ni kuuwa au Ku neutralize kikwazo?
aliyekwambia kwamba inaua popote itakapopiga hakuwa na lengo zuri kwako kielimu.

Maeneo ambayo silaha hii inaweza kuua punde ni kichwani,shingoni,na kifuani.maeneo yaliyobaki yote kuna uwezekano 90% mtu akapona akipigwa hata tumboni.
Wakati wa matumizi askari ameagizwa kuzingatia maeneo chini ya goti ili kuwa na uhakika wa dhana(ku neutralize)
Sasa taja silaha ambayo ni sahihi kwa zoezi hilo la kurenga miguu kati ya hizo unazozifikiria
Shotgun kama za SA haitaki umbali mrefu na ukiitumia umbali mfupi inaondoka mguu kabisa,pistol si tu inataka umbali mfupi lakini na utulivu pia maana sio nzuri ktk shabaha.
 
Wewe jambazi nini ?! Unataka Askari wapewe gobore ili ukija na SMG yako polisi washindwe kupambana na wewe ?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…