Askari Polisi Mwita Milumbe adaiwa kuteswa na kuuwawa, Ndugu waomba msaada

Askari Polisi Mwita Milumbe adaiwa kuteswa na kuuwawa, Ndugu waomba msaada

Anaitwa Mwita Mecky Mirumbe halafu Force Number yake inaanzia na H...!? HAIWEZEKANI!
Nitaeleza; Force Number ya askari wa Tanzania inatakiwa ianze na herufi ya kwanza ya jina la ukoo (Surname). Mfano mimi naitwa Mtoto wa Shule" hivyo kama ningelikuwa askari Force Number yangu ingelianza na "S.....". Kwa huyu, ilitakiwa Force Number yake ianze na "M..."!

Ebu jipangeni kabla ya kuucheza huu mchezo!!
Sasa wewe na polic nani anajua zaidi?kwamba washindwe kusema kuwa si askar wa jesh polic?
 
Malisa Godlisten Leo alikuwa safarini kutoka Marekani ambapo amekuwa kwa zaidi ya miezi tisa (9), tangu alipoenda kuiwakilisha nchi yetu kama mtanzania pekee aliyechaguliwa na Wizara ya Mambo ya nje ya Marekani kwenda kupata mafunzo ya uongozi. Fursa ambayo hujitokeza kwa watanzania wachache sana kama ilivyowahi kutokea kwa aliyekuwa Rais wa awamu ya nne Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.

Alipofika Nairobi- Kenya asubuhi ya leo, alishindwa kuendelea na safari kutokana na kuwepo kwa mgomo wa wafanyakazi unaondelea katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta. Hivyo aliamua kusafiri kwa usafiri binafsi mpaka Namanga ambao ni mpaka kati ya nchi yetu na Kenya ili kuingia nchini kupitia Arusha.

Aliwasili Namanga majira ya saa tisa(9) mchana na kwenda kwa maafisa uhamiaji ili kugongewa hati ya kusafiria (Passport) na hatimaye kuingia nchini kama utaratibu unavyotaka.

Baada ya kufika kwa maafisa uhamiaji hao, walichukua hati yake ya kusafiria na kumwambia kuwa haisomeki kwenye mfumo (system) hivyo wao hawana namna ya kufanya mpaka mkuu wao (in- charge) aje ndio anaweza kuona kwenye mfumo.

Kutokana na kadhia hiyo, na kwa kuwa aliambiwa Mkuu huyo hayupo kwa muda Malisa GJ aliendelea kukaa katika ofisi hizo za uhamiaji akisubiri Mkuu huyo kuja na kuhakikisha tatizo hilo linapatiwa ufumbuzi.

Cha kushangaza ilipofika saa moja jioni, alichukuliwa na gari ambalo si la Polisi jeupe Double Cabin na kupelekwa kituo cha Polisi Longido. Hata hivyo gari hilo halikukaa sana likaondoka kuelekea uelekeo wa Arusha.

Mpaka natoa taarifa hii hakuna taarifa kamili za aliko Malisa GJ na nini ni sababu ya kukamatwa kwake. Aidha simu zake zote zimezimwa tangu alipokuwa anatolewa Namanga.

Nitoe rai kwa Polisi na Uhamiaji kumwachia huru mara moja au kuhakikisha wanatoa taarifa kwa umma za aliko Malisa GJ na sababu ya kukamatwa kwake. Kama haitoshi kuhakikisha anapewa haki zake za kisheria ikiwemo kuonana na mawakili wake na haki ya Mawasiliano.

Dickson Matata (Wakili)
31/8/2026
Arusha-Tanzania.
 

Attachments

  • e773c1bd-d6de-4bec-acb8-a6f6b8fa6d72.jpeg
    e773c1bd-d6de-4bec-acb8-a6f6b8fa6d72.jpeg
    72.3 KB · Views: 8
  • Screenshot_2026-08-27-04-59-50-43_40deb401b9ffe8e1df2f1cc5ba480b12.jpg
    Screenshot_2026-08-27-04-59-50-43_40deb401b9ffe8e1df2f1cc5ba480b12.jpg
    145.9 KB · Views: 6
  • IMG-20260824-WA0073.jpg
    IMG-20260824-WA0073.jpg
    38.2 KB · Views: 6
Huyu naye alikuwa hajielewi,kama kitu unapinga na wenzio hawakuungi mkono na wewe una misimamo yako,si bora tu uache kazi uendelee na maisha mengine,kuna ulazima gani unapinga kitu halafu unabaki humohumo kwenye system wakati unajua fika kuwa huwezi kumshinda bosi wako kwa chochote...?
unafikiri angeacha kazi ndio wangemuacha?
 
Ni kwanini wasio julikana wanapenda kutumia mlango was nyuma was wahanga ktk udhalilishaji n utesaji wao??
Kuuwa Character yako.
Kama huyo spesho fosi ana mazoezi ( PT) zile za kifo unakiona hiki hapa wanaita Kifo sio kitu.

Kumdogosha usugu ili kazi iishe haraka udhalilishaji ( Huzuni ) ni kimbilio lao.
 
Mimi mwenyewe nikionaga askari kapanda ana mibavu ntakuwa ninamashaka na wale watekaji, haiwe

Mkuu mimi likija suala la polisi kuumizana wao kwa wao hata sishtuki aiseeee kwa sababu Mwanza mdogo wangu alikuwa ni mmoja ya waliokuwa kwenye Banda la mpira waliomiminiwa risasi na hao polisi bila huruma ni Bora wangemchukua wakamfunga maisha tukawa tunamtembelea hata Kila mwisho wa mwaka


Loh! Pole sana kwa kumpoteza ndugu yako. Damu yake ikawe laana kwa wauaji. Tunaomba Mungu amjalie pumziko jema marehemu ndugu yako.
 
Back
Top Bottom