Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Ajali imetokea leo alfajiri katika eneo la Mavi ya Ng'ombe kwenye Kijiji cha Mboga, Kata ya Msoga baada ya gari iliyokuwa imebeba maafisa wa polisi aina ya Toyata Crester yenye namba za usajili T.323 BAL iliyokuwa ikiendeshwa na Mkaguzi msaidizi wa Polisi, Ndwanga Dastani (28) aliyekuwa akitokea Chalinze kuelekea Lugoba.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Pius Lutumo, ajali hiyo imetokea baada ya gari hilo kuacha njia na kugonga karavati na kisha kupinduka na kusababisha vifo vya watu watatu pamoja na majeruhi mmoja.
Waliofariki kwenye ajali hiyo ni pamoja na dereva wa gari hiyo Ndwanga Dastani, Polisi Konstebo Emiliana Charles (26) waliokuwa askari wa Kituo cha Polisi Chalinze na Karimu Simba (27) aliyekuwa karani wa Mahakama ya Wilaya ya Lugoba.
Aliyejaruhiwa katika ajali hiyo ni Polisi Konstebo Mwanaidi Shabani (25), askari wa Kituo cha Polisi Chalinze ambaye amejeruhiwa maneneo mbalimbali ya mwili na amepelekwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.
Aidha taarifa hiyo imesema, uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi.
Miili ya marehemu imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti katika Hospitali ya Lugoba.
Azam