HOJA Askari Polisi Wastaafu tulipwe stahiki zinazoendana na uhalisia, kiasi tunachopewa ni kidogo sana

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
A

Anonymous

Guest
Sisi Askari Wastaafu tunaeleza haya kwa uchungu mkubwa sana, hivi karibuni kuna Viongozi walisema sisi tunaolalamika kwamba tulishindwa "kujiandaa" kabla ya kustaafu!

Wanasema eti tulipostaafu tulishindwa kujiandaa wakati tulipokuwa tukikaribia kuingia uraiani. Hiyo kauli ina maana gani? Kujiandaa wanamaanisha nini kuchukua rushwa au? Kwa mshahara upi? Wanataka askari ashindwe kutenda ukweli na uaminifu kazini kwake sababu tu anaambiwa "alishindwa kujiandaa"?

Kuna waliofanya kazi Serikalini kwa zaidi ya miaka 30 lakini wanakuja kupewa shilingi milioni 29! Kisha nyingine wanasema watatupa taratibu, badala ya kutulipa fedha zetu zote kwa pamoja baada ya kulitumikia taifa hili kwa miaka zaidi yote hiyo, wanatupa fedha hizo kidogo kidogo, wanakata na kukokotoa wanavyotaka wao!

Wenzetu huo Dar es Salaam walilalamika mara kadhaa kuhusu hili lakini hakuna hatua zilizochukuliwa. Wengi wetu wanasita kujitokeza kuzungumza hadharani sababu kuna matukio ya watu kupote ambayo tunayasikia, hivyo tunanun'gunika tu chinichini.

Wanatupa labda laki tatu na nusu au laki mbili, tena kwa kusuasua kila mwezi. Hivi hizo pesa ndogondogo zinasaidia nini kwa mtu aliyestaafu ambaye bado ana watoto wanaosoma na wanahitaji ada na mahitaji mengine?

Mtu amepambana na kulitumikia Taifa miaka 34 au zaidi, halafu leo anapewa Shilingi Milioni 29 kidogo kidogo kana kwamba wanatufanyia biashara na fedha zetu!

Hali hii inatufanya wastaafu wengi tuishi kwa shida na dhiki kubwa, na wengine wanajikuta wanakufa kwa mawazo na shinikizo la damu, au hata kujinyonga kwa sababu ya maisha magumu huku haki zao zikiwa zimeshikiliwa.

Tena ukitaka kujitokeza kuongea na kulalamika, unakabiliwa na vitisho au kufanyiwa mambo mabaya! Ndiyo maana askari wengi wadogo wanaumia na kulia kimya kimya lakini viongozi wetu wa juu (Askari) hawajali kwa sababu wao wana mifuko mikubwa.

Wito wangu na ombi letu kubwa kwa Serikali na uongozi wa Jeshi la Polisi na Jeshi la Magereza kote nchini (ikiwemo Mkoani Manyara na Tanzania nzima): Tulipeni stahiki zetu zote kwa mkupuo mmoja bila kutukata wala kutulipa kidogo kidogo!

Tulipeni pesa zetu zote tulizozifanyia kazi kwa jasho na uaminifu wetu ili tukazitumie kujikimu na kusomesha familia zetu.
 
3d0e6208-cc73-463e-9898-8717896d48d1-1_all_10001.jpg
 
Sisi askari wastaafu tunaeleza haya kwa uchungu mkubwa sana kero na dhuluma inayotupata wastaafu kutoka kwa viongozi wetu.

Hivi karibuni kuna Viongozi walisema kwamba sisi tunaolalamika kwamba tulishindwa "kujiandaa" kabla ya kustaafu!

Wanasema eti tulipostafu tulishindwa kujiandaa wakati tulipoingia uraiani. Hiyo kauli ina maana gani? Kujiandaa wanamaanisha nini kuchukua rushwa au? Wanataka askari ashindwe kutenda ukweli na uaminifu kazini kwake kwa sababu tu anaambiwa "alishindwa kujiandaa"?

Kuna waliofanya kazi Serikalini kwa zaidi ya miaka 30 lakini wanakuja kupewa shilingi milioni 29! Kisha nyingine wanasema watatupa taratibu, badala ya kutulipa fedha zetu zote kwa pamoja baada ya kulitumikia taifa hili kwa miaka zaidi yote hiyo, wanatupa fedha hizo kidogo kidogo, wanakata na kukokotoa wanavyotaka wao!

Wanatupa labda laki tatu na nusu au laki mbili, tena kwa kusuasua kila mwezi. Hivi hizo pesa ndogondogo zinasaidia nini kwa mtu aliyestaafu ambaye bado ana watoto wanaosoma na wanahitaji ada na mahitaji mengine?

Mtu amepambana na kulitumikia taifa miaka 34 au zaidi, halafu leo anapewa shilingi milioni 29 kidogo kidogo kana kwamba wanatufanyia biashara na fedha zetu!

Hali hii inatufanya wastaafu wengi tuishi kwa shida na dhiki kubwa, na wengine wanajikuta wanakufa kwa mawazo na shinikizo la damu, au hata kujinyonga kwa sababu ya maisha magumu huku haki zao zikiwa zimeshikiliwa.

Tena ukitaka kujitokeza kuongea na kulalamika, unakabiliwa na vitisho na hofu ya kutekwa au kufanyiwa mambo mabaya! Ndio maana askari wengi wadogo wanaumia na kulia kimya kimya lakini viongozi wa juu hawajali kwa sababu wao wana mifuko mikubwa.

Wito wangu na ombi letu kubwa kwa serikali na uongozi wa Jeshi la Polisi na Jeshi la Magereza kote nchini (ikiwemo Mkoani Manyara na Tanzania nzima): Tulipeni stahiki zetu zote kwa mkupuo mmoja bila kutukata wala kutulipa kidogo kidogo!

Tulipeni pesa zetu zote tulizozifanyia kazi kwa jasho na uaminifu wetu ili tukazitumie kujikimu na kusomesha familia zetu.
Askari wastaafu,Kumbukeni, mnacholipwa ni size yenu,tena mmezidishiwa sana,nyie ni MALI YA CCM
 
Attachments

  • 6405238-eae1ceee959bf6fd97d9fb2eab102cc4.mp4
    9.2 MB
MAlipo ya kupiga watuu ndio.hayoo soo tulieni dawa iwaingiee na hatutaki kelele

Kama mlivyokuwa mkijipigia watuu
Endeleeni kupigwa nanyi soo usumbufuu hatutaki huku jukwaani.

Na hata hivyo moja wa ya watu wa ccm
Amesema nynyi ni Ccm
Soo.nendeni ofii si za chama chenu kinachodai MAMBO YA UTUU
 
Askari? Mapolisi? Nyinyi mnaotupiga marisasi na kutuua kama wanyama? Wala rushwa nyinyi! Waonevu! Na nyinyi mnalia lia mtendewe haki? Haki gani? Ningekuwa mimi hata hicho kidogo mnachopata msingekipata wallahi! Kwani hela za rushwa, uonevu na michongo hazikuwatosha? Nyinyi si WanaCCM nyinyi?

Umenichefua sana.

Tesekeni!
Tesekeni!
Tesekeni!
Tesekeniiiiiiiiiiiiiii! 📣📣📣📣📣📣📣📣

Na damu zote zisizo na hatia mlizomwaga. Rushwa zote mlizokula. Uonevu wote mliofanya. Hebu na vikawaandame nyinyi pamoja na uzao wenu wote. Laana ya haki na ikawapige. Muwe na mwisho mbaya. Muaibike mileleeeeeeeee wajaa laana nyinyi! 📌📌📌🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿
 
Sisi askari wastaafu tunaeleza haya kwa uchungu mkubwa sana kero na dhuluma inayotupata wastaafu kutoka kwa viongozi wetu.

Hivi karibuni kuna Viongozi walisema kwamba sisi tunaolalamika kwamba tulishindwa "kujiandaa" kabla ya kustaafu!

Wanasema eti tulipostafu tulishindwa kujiandaa wakati tulipoingia uraiani. Hiyo kauli ina maana gani? Kujiandaa wanamaanisha nini kuchukua rushwa au? Wanataka askari ashindwe kutenda ukweli na uaminifu kazini kwake kwa sababu tu anaambiwa "alishindwa kujiandaa"?

Kuna waliofanya kazi Serikalini kwa zaidi ya miaka 30 lakini wanakuja kupewa shilingi milioni 29! Kisha nyingine wanasema watatupa taratibu, badala ya kutulipa fedha zetu zote kwa pamoja baada ya kulitumikia taifa hili kwa miaka zaidi yote hiyo, wanatupa fedha hizo kidogo kidogo, wanakata na kukokotoa wanavyotaka wao!

Wanatupa labda laki tatu na nusu au laki mbili, tena kwa kusuasua kila mwezi. Hivi hizo pesa ndogondogo zinasaidia nini kwa mtu aliyestaafu ambaye bado ana watoto wanaosoma na wanahitaji ada na mahitaji mengine?

Mtu amepambana na kulitumikia taifa miaka 34 au zaidi, halafu leo anapewa shilingi milioni 29 kidogo kidogo kana kwamba wanatufanyia biashara na fedha zetu!

Hali hii inatufanya wastaafu wengi tuishi kwa shida na dhiki kubwa, na wengine wanajikuta wanakufa kwa mawazo na shinikizo la damu, au hata kujinyonga kwa sababu ya maisha magumu huku haki zao zikiwa zimeshikiliwa.

Tena ukitaka kujitokeza kuongea na kulalamika, unakabiliwa na vitisho na hofu ya kutekwa au kufanyiwa mambo mabaya! Ndio maana askari wengi wadogo wanaumia na kulia kimya kimya lakini viongozi wa juu hawajali kwa sababu wao wana mifuko mikubwa.

Wito wangu na ombi letu kubwa kwa serikali na uongozi wa Jeshi la Polisi na Jeshi la Magereza kote nchini (ikiwemo Mkoani Manyara na Tanzania nzima): Tulipeni stahiki zetu zote kwa mkupuo mmoja bila kutukata wala kutulipa kidogo kidogo!

Tulipeni pesa zetu zote tulizozifanyia kazi kwa jasho na uaminifu wetu ili tukazitumie kujikimu na kusomesha familia zetu.
Kwa kweli inaumiza sana. Mtu ametumikia Taifa miaka 30+ kwa uaminifu, halafu akistaafu anapewa kiasi ambacho hata kwa maisha ya sasa ni kidogo sana.

Na hili si tatizo la askari tu, ni la wastaafu wengi; isipokuwa wanasiasa na baadhi ya senior officers ndio wanaonekana kufaidika zaidi.
Milioni 29 leo huwezi hata kujenga nyumba nzuri na kupata kiwanja sehemu nzuri. Hata ukinunua Bajaj kwa kujiajiri, unaweza kubakiwa na milioni 10 hivi tu.

Hiyo ndiyo heshima tunayompa mtu aliyelitumikia Taifa miaka 30?
Serikali inahitaji kuangalia upya kabisa kikokotoo cha mafao.

Ni aibu na fedheha mtu atumike miaka 30+ halafu anastaafu na posho/mafao yasiyolingana na uhalisia wa maisha.

Mfumo huu pia unashusha sana morali ya watumishi na unaweza kumweka mstaafu kwenye msongo mkubwa wa mawazo na hata depression.
 
Ungemfikishia Paulo Chacha na yule mwenezi wa Chama bwana Kenani Kihongosi na Makamu Mwenyekiti Mzee Wasira maana wao wanasema nyinyi ni mali yao ndani ya Chama na mnafanya kazi kwa ajili ya Chama kubaki madarakani, sasa unatulalamikia sisi badala ufikishe kwenye ngazi za uongozi wa Chama mnachokifanyia kazi, umechukua hatua hio kabla?
 
Back
Top Bottom