Askari Shahidi ashindwa kueleza maana ya Kahaba na Malaya katika Kesi ya Wanawake waliokamatwa Riverside wakidaiwa kujiuza

Shahidi wa pili katika kesi ya ukahaba inayowakabili washtakiwa watano katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Sokoine Drive, ameileza mahakama hiyo kuwa waliwakamata washtakiwa hao kwa tuhuma za ukahaba kutokana na viashiria vya aina ya mavazi waliyokuwa wameyavaa na muda na mahali walikokutwa na polisi.

Hata hivyo, shahidi huyo ambaye ni askari kutoka Kituo cha Polisi Mburahati, WP Konstebo wa Polisi (PC), Tunusuru Malungula, alijikuta katika wakati mgumu alipotakiwa kueleza maana ya umalaya au ukahaba kutokana na viashiria hivyo alivyovitaja.

Ilikuwa ni wakati wa maswali ya dodoso aliyoulizwa na mawakili wa utetezi katika kesi hiyo, Peter Madeleka, Jebra Kambole na Maria Mushi, leo Alhamisi Juni 27, 2024, mpaka akasema kuwa hajui maana ya ukahaba.

Pia, amesema hajui kama kuna sheria inayobainisha sifa za mavazi yanayoashiria ukahaba wala inayoweka muda ambao mtu akikutwa barabarani anakuwa anajihusisha na ukahaba.

Shahidi huyo pia alitakiwa kueleza kama washtakiwa walikuwa wakiuza miili yao, wao walibaki na nini na wateja walioinunua wako wapi.

Washtakiwa katika kesi hiyo inayosikilizwa na Hakimu Mfawidhi Rachael Kasebele ni Mariam Yusufu Mkinde (25) mkazi wa Magomeni, Mwazani Nassoro (25) mkazi wa Kigogo, Mwanaidi Salum (25) mkazi wa Mabibo, Faudhia Hassan (35) mkazi wa Ubungo na Tatu Omary (40) mkazi wa Ubungo.

Katika kesi hiyo ya jinai namba 17277/2024, washtakiwa hao wanakabiliwa na shtaka moja la kufanya vitendo vya aibu mbele ya hadhara kwa ajili ya kufanya umalaya, kinyume na kifungu cha 176 (a) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16, marejeo ya mwaka 2022.
Hivi kweli, Hawa tuwaite ni wachuuzi, wanunuzi wako wapi? (Asie na dhambi na awe wakwanza kumtupia jiwe)
 
Kwangu mimi sijaona watu wajinga kama hawa wanao itwa Mawakili. Shida hata hao maaskari wana shida. Unamuulizaje mtu kuhusu maana ya kahaba au malaya au ukahaba au umalaya ? Wakili kwanza anaonekana hajielewi. Ni sawa leo hii umuulize maji ni nini ? Sio kila kitu kinahitaji kiarifisho (taarifu), kuna vitu kwa kujulikana kwake havihitaji kutolewa maana mfano wa hivyo vitu ni ukahaba au umalaya.

Hapo wakili kiuhalisia ndio kilaza sababu ameuliza swali la kipuuzi sana, shida aliye ulizwa nae hajui.

Kingine hizi sheria za kibidamu zina ujinga na madhaifu mengi sana. Yaani leo hii kuna watu wanaitwa wasomi wanawatetea watu wanao fanya uovu wa wazi namna ile. Watu hawa hawakupaswa kuwepo katika mgongo wa ardhi.
 
Hata hivyo, shahidi huyo ambaye ni askari kutoka Kituo cha Polisi Mburahati, WP Konstebo wa Polisi (PC), Tunusuru Malungula, alijikuta katika wakati mgumu alipotakiwa kueleza maana ya umalaya au ukahaba kutokana na viashiria hivyo alivyovitaja.

Ningekuwa mimi kwanza, ningemuomba anipe maana ya maana ya maana, kisha anipe ukamilifu wa maana anayoiujua yeye.
 
Muuza mayai wa ubungo mjini hapo atasumbua sana , ukishaona wakili kambole hiyo imeisha
 
Uonevu tu, hakuna under 18 hapo. Ni ngumu kuthibitisha ni wauza miili yao
 
Askari wengi hizi kesi zinawasumbua katika kazi inayowaumiza hawa jamaa zetu ni kwenda kusimama na Wakili upande wa utetezi huwa wanaona kama wapo kwenye kikaango ila ndio hivyo hakuna namna inabidi waende tu...
 
Hata hiyo ikija kisheria kabisa mkuu kahaba anachomoka.
Atasema umemtongoza ili awe mpenzi wako na amekubali, ukaamua mwenyewe umpatie hela ya vocha.
Naona bora waachwe tu au litafutwe kosa lingine.
Kwa hiyo kiufupi tukubali walishashindikana! Waachachwe tu wafanye watakavyo as long haina direct effect kwa wengine unless umechagua kujipeleka kwa utashi wako mwenyewe.
 
Back
Top Bottom