Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Mbali na askari wa jeshi la Israel wanaouliwa vitani na Hamas kuna adui wao wengine wanaowatesa kichini chini .Maabadui hao wengine ni viumbe visivyoonekana ambavyo huwakumba wale wanaopata majeraha katika vita hivyo vinavyoendelea kwa mwezi wa tatu sasa.
Viungo vya askari hao huathiriwa na aina za bakteria wasiotibika kwa dawa za kawaid zinazotibu majeraha kama hayo.Wadudu hao ni kama vile Klebsiella ,Escherichia coli, naAspergillus fungi.
Mwanzoni mwa mwezi huu askari hao vile vile walipatwa na maradhi ya kuhara na maumivu makali ya matumbo yaliyopelekea baadhi yao kuhamishwa kutoka uwanja wa vita.
Maambukizi ya namna hii si mara ya mwanzo kutokea katika uwanja wa vita.Hata askari wa Marekani waliokuwa wakipigana Iraq na Afghanistan baadhi yao walirudi makwao Marekani baada ya kuambukizwa na bakteria waliopewa majina ya Iraqibacter superbug na Acinetobacter Baumannii.