Pre GE2025 Askari wa Jeshi la Polisi athibitisha jinsi wanavyosaidia kuiba kura ili CCM ibaki madarakani, ni aibu!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ngoja kwanza, kwani raisi SSH alichaguliwa kwa kura?, mwaka gani huo?.

Uliyasikiliza mazungumzo ya CDF Mabeyo vizuri kweli kuhusu nyakati za mwisho za JPM?

Uliisikiliza hotuba/salamu za CDF Mabeyo katika hafla ya kuapishwa kwa raisi SSH?.

Hii kauli ilikuwa ni kauli za mwanzo sana kusema yaliyojiri zile nyakati.
 
hii clip ni enzi ya jk, wame edit sauti, na hiyo sauti sio ya afande kyondo, haya mambo ya kijinga hayawasaidii
Hatari sana !!
Kweli kupakazia Watu kwa mambo mabaya ambayo hawayafanyi au hawakuyafanya ni Ushetani wa hali ya juu sana !!
Na ni Hatari sana kwa mustakabali wa Umoja wetu Nchini !!

Ila ikumbukwe mambo haya ya kupakaziana Upuuzi Upuuzi yanatumiwa sana na Vijana wa sare za kijani tangu kitambo sana !
Hao wengine wa sasa wanaiga tu !!

Law of the Universe sayings -:
What goes around comes around !

Bandugu Acheni huo Ujinga !!
 
Rais Samia alichaguliwa kwa Kura akiwa Mgombea mwenza wa Hayati JPM,
Kisha akawa Rais kwa mujibu wa Takwa la Kikatiba linavyoelekeza pindi Rais aliyepo madarakani anapofariki !
Anayepaswa kuapishwa kuwa Rais ni Makamu wa Rais !
 
Rais Samia alichaguliwa kwa Kura akiwa Mgombea mwenza wa Hayati JPM,
Kisha akawa Rais kwa mujibu wa Takwa la Kikatiba linavyoelekeza pindi Rais aliyepo madarakani anapofariki !
Anayepaswa kuapishwa kuwa Rais ni Makamu wa Rais !
Ni lini mgombea mwenza anapigiwa kura kwenye uchaguzi Mkuu?. Tunapiga kura ya uraisi sio ugombea wenza.

Soma iyo fomu vizuri hakuna neno Makamo wa Raisi au Mgombea mwenza halo juu kwenye neno uchaguzi ni raisi tu na ndie tunayemchagua.

Na hapa ndipo marekebisho yanahitajika pia ili kuweka uhalali pale mambo yanapotokea kama yaliyotokea.
 

Attachments

  • images (22).jpeg
    32.9 KB · Views: 1
Hakuna mgombea URais anayeruhusiwa kugombea kiti hicho akiwa pekee !
Ni lazima awe na mgombea mwenza Hiyo ni kwa vyama vyote !

Kwahiyo tunapompigia kura Rais uliyeamua kumpa kura yako umempa kura hiyo na mgombea mwenza wake πŸ‘
Na ndio maana Kwa vyama vyote mgombea URais akitokea upande mmoja wa muungano ni lazima mgombea mwenza atokee upande wa pili wa Muungano,
Na kipindi cha kampeni wote wanazunguka kwa Wananchi kuomba kura !
 
Mgeni wa Jiji angalia vizuri hiyo karatasi ya mfano wa kupigia kura utaona kila Chama kwenye kisanduku chao zipo picha za Wagombea Wawili πŸ˜…πŸ‘
 
Bado yanakuja makubwa zaidi, nimwanzo wa kuanguka, na wataanguka kwa KISHINDO KIKUBWA SANA.....2024 to 2025....
 
Sasa mkuu kama polisi anaweza kuchukua rushwa mchana peupe akiwa na macho makavu anawezaje kuona aibu kuiibia kura CCM ishinde iendelee kumpa mshahara mfupi kama akili yake.

Tatizo ni somo la uraia. Watumishi wa umma huwa wanafikiri nchi ikiongozwa na chama tofauti na CCM kazi zao zitakoma au hawataingiziwa mshahara, pia wananchi wanalishwa propaganda kuwa CCM ndio inalinda amani tofauti na hapo tutaingia kwenye machafuko.
 
Jamani tuende mbele turudi nyuma kwa upinzani tulionao nii bora tu ccm wakaendelea kutawala maana angalau mule kuna wazalendo. Huku upinzani ukifuatilia kwa makini hakuna uzalendo, yaani akitokea kiongozi wa chama tawala anafanya vizuri na wakatokea wapinzani wakawa tayari kufanya naye kazi wanawaita wasaliti, wao tafsri ya upinzani ni kuwa na hasira muda wote dhidi ya kiongozi au mtu yeyote wa chama tawala na kufoko foka hii tabia wanayo hasa chadema.
 
Namna pekee ya polisi kuacha kuisaidia serekali iliyopo madarakani ni kwanza Rais asiwe Amir jesh mkuu pili wakuu wa mikoa na wilaya wasiwe wenyeviti wa kamati ya ulinzi na usalama za mikoa na wilaya.
Vinginevyo hamna njia nyingine
Wazo zuri, tunafika je huko?, (how do we go about)
 
EPISODE 1: Nape Naye.
EPISODE 2: Fairs Buruhan
EPISODE 3: DC Longido
EPISODE4: Afande wa Polisi
Endelea kufutilia "Full Movie to 2025".
 
Unaumwa wewe Sio bure
 
Kijana wa Lema Jamaa alishastaafu πŸ˜‚πŸ˜‚
Nani kastaafu huyo? Afande πŸ˜„ 🀣 πŸ˜‚ πŸ˜† alafu aanze kulia lia kiunua mgongo hakitoshi akiwa kazini alikubali kutumika kama mpira
 
Kauli haina utata wowote ule
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…