Uzalendo wa Kitanzania
JF-Expert Member
- Mar 8, 2020
- 3,585
- 8,106
Askari huyo wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) anayeenda kwa jina la Daniel Warioba alijaribu kujiua kwa kunywa sumu baada ya tukio hilo lakini hakufanikiwa.
Uchunguzi wa tukio hilo la kutisha lililotokea Mlandizi Mkoani Pwani bado unaendelea na taarifa kamili itatolewa na mamlaka husika ambayo ni Jeshi la Polisi
Inadaiwa Kuwa chanzo cha tukio la kikatili ni mfarakano uliochangiwa pamoja na mambo mengine wivu wa kimapenzi baina ya wanandoa hao
Mtuhumiwa huyo kwa Sasa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano zaidi ya tukio hilo.
Tunatoa pole kwa familia ya Mwendazake aliyehudumu kama Mwalimu Katika uhai wake
=====
Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linamshikilia Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Koplo Daniel Warioba (43) kutoka Kikosi cha 92 TJ kwa tuhuma za kumuua Mke wake Joyce Ismail (35) ambaye ni Mwalimu wa Shule ya Msingi Ruvu Darajani
Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa, aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana huu katika eneo la Janga, Wilaya ya Kipolisi Mlandizi.
Kamanda Wankyo alisema askari huyo anadaiwa kumchoma mke wake na kitu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili na kumsababishia kifo.
Kwa mujibu wa Kamanda Wankyo, baada ya kutekeleza mauaji hayo, mtuhumiwa anadaiwa alitaka kunywa sumu kwa lengo la kujiua.
Wankyo alisema polisi wamemkamata mtuhumiwa huyo na anaendelea kupata matibabu katika Hospitali ya Rufani ya Mkoa ya Tumbi, huku chanzo cha tukio hilo kikiendelea kuchunguzwa.