Askari wa Marekani waliorudi nchini kwao baada ya kushiriki vita nchini Iraq na Afghanistan wanajiua kwa viwango vya juu

Strong ladg

Senior Member
Joined
Jul 15, 2021
Posts
170
Reaction score
445
Ripoti zinasema, tangu uvamizi wa Marekani nchini Afghanistan na Iraq uliotokea baada ya Shambulio la September 11:

1. Zaidi ya askari 30,000 walioshiriki uvamizi huo wamejiua. Hii ni mara nne zaidi ya askari waliokufa vitani/ kwenye mapigano.

2. Mwaka 2019 pekee askari 6261 walijiua ikiwa ni ongezeko la asilimia saba kulinganishwa na takwimu za mwaka 2018.

3. Kwa wastani kwa siku askari 17 walioshiriki uvamizi nchini Iraq/ Afghanistan hujiua.

4. Visa vya kujiua miongoni mwa askari hao ni mara mbili zaidi ikilinganishwa na visa vya kujiua vinavyotokea miongoni mwa raia wa kawaida

5. Askari wengi wanaojiua wako kwenye kundi la umri kati ya miaka 18-34. Visa vya kujiua miongoni mwa kundi hili ni mara tatú zaidi ikilinganishwa na visa vya kujiua miongoni mwa askari walio na umri zaidi ya miaka 34.

CHANZO CHA TAKWIMU/ SOURCE:
"More Veterans Die By Suicide Than In Combat. But It's Preventable | Cognoscenti" More Veterans Die By Suicide Than In Combat. But It's Preventable

FUNZO: TATIZO LA AFYA YA AKILI LINAWEZA KUMKUTA MTU YOYOTE. USIOGOPE WALA USISITE KUOMBA MSAADA PALE UNAPOPATWA NA MAWAZO YA KUJIUA.
 
Vita ni upumbavu.

Yani mnauana kisa wanasiasa wawili wenye bifu. Wenyewe wamekaa ofisini kwao kwenye viti vya kuzunguka wakiwacheki mnavyo uana.

Halafu nyie mna miminiana risasi maporini.

Ndio maana wanajeshi wakikaaga chini na kutafakari wanajiona walivyokuwa mafala.

Mwisho wa siku wanajiua.
 
Japo sina uhakika na taarifa ila sikatai kuhusu kufa kwao huenda taarifa ipo sahihi...

Ila kwa wewe unahisi kwamba ni kweli wanajiua?

Politics ni mchezo mchafu sana.

Kuna Siri watu wanazibeba wanatakiwa kufa nazo kwa namna yoyote ile ni either wametaka or wamelazimishwa.
 
Hizi ni ripoti za kutoka Uarabuni na kufika mpaka Masjid za Tandale
Nimeweka chanzo cha ripoti na walioitoa ni Marekani. Kingine mimi sio Muislam nimeiona tu hii ripoti mahali nikaitafsiri nikaileta ili watu wajue haya matukio ya kujiua yanaweza kumkuta mtu yoyote maana mwanzo sikuwahi kudhani mwanajeshi anaweza kujiua. Kama huamini unaweza kwenda Google ukajitafutia mwenyewe habari.
 
Japo sina uhakika na taarifa ila sikatai kuhusu kufa kwao huenda taarifa ipo sahihi...

Ila kwa wewe unahisi kwamba ni kweli wanajiua?

Politics ni mchezo mchafu sana.

Kuna Siri watu wanazibeba wanatakiwa kufa nazo kwa namna yoyote ile ni either wametaka or wamelazimishwa.
According tu sources nilizotumia ambazo ni media za Magharibi kama BBC, media za kujitegemea na documentary nilizoangalia ni kweli wanajiua. Kuna documentary inaitwa the heart of a soldier ndo inaelezea vizuri na hao wanajeshi walioenda huko wanahojiwa . Kama nimeingia kingi basi iko nje ya uwezo wangu kuelezea maana mimi sio mtaalamu
 
Ripoti zinasema, tangu uvamizi wa Marekani nchini Afghanistan na Iraq uliotokea baada ya Shambulio la September 11:

1. Zaidi ya askari 30,000 walioshiriki uvamizi huo wamejiua. Hii ni mara nne zaidi ya askari waliokufa vitani/ kwenye mapigano.

2. Mwaka 2019 pekee askari 6261 walijiua ikiwa ni ongezeko la asilimia saba kulinganishwa na takwimu za mwaka 2018.

3. Kwa wastani kwa siku askari 17 walioshiriki uvamizi nchini Iraq/ Afghanistan hujiua.

4. Visa vya kujiua miongoni mwa askari hao ni mara mbili zaidi ikilinganishwa na visa vya kujiua vinavyotokea miongoni mwa raia wa kawaida

5. Askari wengi wanaojiua wako kwenye kundi la umri kati ya miaka 18-34. Visa vya kujiua miongoni mwa kundi hili ni mara tatú zaidi ikilinganishwa na visa vya kujiua miongoni mwa askari walio na umri zaidi ya miaka 34.

CHANZO CHA TAKWIMU/ SOURCE:
"More Veterans Die By Suicide Than In Combat. But It's Preventable | Cognoscenti" More Veterans Die By Suicide Than In Combat. But It's Preventable

FUNZO: TATIZO LA AFYA YA AKILI LINAWEZA KUMKUTA MTU YOYOTE. USIOGOPE WALA USISITE KUOMBA MSAADA PALE UNAPOPATWA NA MAWAZO YA KUJIUA.
Laana ya maovu waliyoyatenda,fikiria wale wa Israeli watakao rudi kutoka gaza,Lebanon,na kwingineko wanao ua watu kama majani,au panya au mende au chawa?Na hiyo laana haipiti kando na mwana mboga mboga yeyote na lile mbeleko lao policccemu,bila kuwasahau waenguaji wasimamizi wasaidizi.
 
Veterans wengi wao ni homeless utawaona kwenye traffic stop au grocery store wanaomba hela. Tatizo maisha ya kambini kula,kulala na usafiri bure. Wakiingia uraiani baada ya 2yr contract kuisha hawana walicho wekeza.

Majeshi wa marekani wengi wao ni fresh out of high school hawana college/university education sasa huishia viwandani au homeless.
 
Vita ni upumbavu.

Yani mnauana kisa wanasiasa wawili wenye bifu. Wenyewe wamekaa ofisini kwao kwenye viti vya kuzunguka wakiwacheki mnavyo uana.

Halafu nyie mna miminiana risasi maporini.

Ndio maana wanajeshi wakikaaga chini na kutafakari wanajiona walivyokuwa mafala.

Mwisho wa siku wanajiua.
Kweli vita ni kitendo cha watu wasiofahamiana kuuana kwa ajili ya watu wanaofahamiana .
 
Veterans wengi wao ni homeless utawaona kwenye traffic stop au grocery store wanaomba hela. Tatizo maisha ya kambini kula,kulala na usafiri bure. Wakiingia uraiani baada ya 2yr contract kuisha hawana walicho wekeza.

Majeshi wa marekani wengi wao ni fresh out of high school hawana college/university education sasa huishia viwandani au homeless.
Duh yaani veterans ni homeless? Mmmh makubwa haya.
 
Ripoti zinasema, tangu uvamizi wa Marekani nchini Afghanistan na Iraq uliotokea baada ya Shambulio la September 11:

1. Zaidi ya askari 30,000 walioshiriki uvamizi huo wamejiua. Hii ni mara nne zaidi ya askari waliokufa vitani/ kwenye mapigano.

2. Mwaka 2019 pekee askari 6261 walijiua ikiwa ni ongezeko la asilimia saba kulinganishwa na takwimu za mwaka 2018.

3. Kwa wastani kwa siku askari 17 walioshiriki uvamizi nchini Iraq/ Afghanistan hujiua.

4. Visa vya kujiua miongoni mwa askari hao ni mara mbili zaidi ikilinganishwa na visa vya kujiua vinavyotokea miongoni mwa raia wa kawaida

5. Askari wengi wanaojiua wako kwenye kundi la umri kati ya miaka 18-34. Visa vya kujiua miongoni mwa kundi hili ni mara tatú zaidi ikilinganishwa na visa vya kujiua miongoni mwa askari walio na umri zaidi ya miaka 34.

CHANZO CHA TAKWIMU/ SOURCE:
"More Veterans Die By Suicide Than In Combat. But It's Preventable | Cognoscenti" More Veterans Die By Suicide Than In Combat. But It's Preventable

FUNZO: TATIZO LA AFYA YA AKILI LINAWEZA KUMKUTA MTU YOYOTE. USIOGOPE WALA USISITE KUOMBA MSAADA PALE UNAPOPATWA NA MAWAZO YA KUJIUA.
Hii habari umeinukuu wapi, mbona haina uhalisia?

Watu wapigane vita miaka ya 90 huko, halafu wagandishe umri wao, mpaka leo wabakie kuwa na miaka 34?
 
Duh yaani veterans ni homeless? Mmmh makubwa haya.
Wanajeshi wa marekani 40% yao huishia kuwa homeless au kuwa mateja, wengine huishia kufanya kazi viwandani na truck driver.

Kuna msela nilisoma nae kule hivi sasa akili yake haipo poa anapiga kelele burebure au anatafuta ugomvi tu.

Wengi wao ukiwauliza kwanini alijiunga na jeshi husema walitaka kuishi free life( mbali na wazee wao) au husema walidhani vita kama ile kwenye movie na video game's.
 
Hii habari umeinukuu wapi, mbona haina uhalisia?

Watu wapigane vita miaka ya 90 huko, halafu wagandishe umri wao, mpaka wabakie kuwa na miaka 34?
Nimeweka source ya habari ( kuna link) na source ni ya wamarekani wenyewe sijaitoa taarifa hewani. Halafu Afghanistan hawajapigana miaka ya 90 ni miaka ya 2000+ maana aliyeidhinisha Marekani kwenda Iraq na Afghanistan ni Rais Bush aliyemuachia kijiti Obama. Kwahiyo unaweza kuona sio miaka mingi iliyopita. Na wanavyoenda huko wanapishana unakaa kwa muda unarudi nyumbani mwenzio anaenda.
 
Back
Top Bottom