Askari wa Marekani waliorudi nchini kwao baada ya kushiriki vita nchini Iraq na Afghanistan wanajiua kwa viwango vya juu

Wanajeshi wa marekani 40% yao huishia kuwa homeless au kuwa mateja, wengine huishia kufanya kazi viwandani na truck driver.

Kuna msela nilisoma nae kule hivi sasa akili yake haipo poa anapiga kelele burebure au anatafuta ugomvi tu.

Wengi wao ukiwauliza kwanini alijiunga na jeshi husema walitaka kuishi free life( mbali na wazee wao) au husema walidhani vita kama ile kwenye movie na video game's.
Duh huyo nae asije kujiua maana hizo dalili sio nzuri
 
Ripoti zinasema, tangu uvamizi wa Marekani nchini Afghanistan na Iraq uliotokea baada ya Shambulio la September 11:

1. Zaidi ya askari 30,000 walioshiriki uvamizi huo wamejiua. Hii ni mara nne zaidi ya askari waliokufa vitani/ kwenye mapigano.

2. Mwaka 2019 pekee askari 6261 walijiua ikiwa ni ongezeko la asilimia saba kulinganishwa na takwimu za mwaka 2018.

3. Kwa wastani kwa siku askari 17 walioshiriki uvamizi nchini Iraq/ Afghanistan hujiua.

4. Visa vya kujiua miongoni mwa askari hao ni mara mbili zaidi ikilinganishwa na visa vya kujiua vinavyotokea miongoni mwa raia wa kawaida

5. Askari wengi wanaojiua wako kwenye kundi la umri kati ya miaka 18-34. Visa vya kujiua miongoni mwa kundi hili ni mara tatú zaidi ikilinganishwa na visa vya kujiua miongoni mwa askari walio na umri zaidi ya miaka 34.

CHANZO CHA TAKWIMU/ SOURCE:
"More Veterans Die By Suicide Than In Combat. But It's Preventable | Cognoscenti" More Veterans Die By Suicide Than In Combat. But It's Preventable

FUNZO: TATIZO LA AFYA YA AKILI LINAWEZA KUMKUTA MTU YOYOTE. USIOGOPE WALA USISITE KUOMBA MSAADA PALE UNAPOPATWA NA MAWAZO YA KUJIUA.
Itakuwa majini ya kitaliban na kiarabu waliyoo doka nayo huko vitani
 
Siyo mara ya kwanza hii mada na comments kwa bahati mbaya ni zile zile albadir, karma, msongo, nk nk

Sikilizeni nyinyi msiojua lolote, ni kwamba hao jamaa wanauawa wala usidanganywe kuwa wanajiua!
 
Ripoti zinasema, tangu uvamizi wa Marekani nchini Afghanistan na Iraq uliotokea baada ya Shambulio la September 11:

1. Zaidi ya askari 30,000 walioshiriki uvamizi huo wamejiua. Hii ni mara nne zaidi ya askari waliokufa vitani/ kwenye mapigano.

2. Mwaka 2019 pekee askari 6261 walijiua ikiwa ni ongezeko la asilimia saba kulinganishwa na takwimu za mwaka 2018.

3. Kwa wastani kwa siku askari 17 walioshiriki uvamizi nchini Iraq/ Afghanistan hujiua.

4. Visa vya kujiua miongoni mwa askari hao ni mara mbili zaidi ikilinganishwa na visa vya kujiua vinavyotokea miongoni mwa raia wa kawaida

5. Askari wengi wanaojiua wako kwenye kundi la umri kati ya miaka 18-34. Visa vya kujiua miongoni mwa kundi hili ni mara tatú zaidi ikilinganishwa na visa vya kujiua miongoni mwa askari walio na umri zaidi ya miaka 34.

CHANZO CHA TAKWIMU/ SOURCE:
"More Veterans Die By Suicide Than In Combat. But It's Preventable | Cognoscenti" More Veterans Die By Suicide Than In Combat. But It's Preventable

FUNZO: TATIZO LA AFYA YA AKILI LINAWEZA KUMKUTA MTU YOYOTE. USIOGOPE WALA USISITE KUOMBA MSAADA PALE UNAPOPATWA NA MAWAZO YA KUJIUA.
Naomba msaada wa connection ya kazi ndugu yangu hii kitu inanisumbua
 
Vita ni upumbavu.

Yani mnauana kisa wanasiasa wawili wenye bifu. Wenyewe wamekaa ofisini kwao kwenye viti vya kuzunguka wakiwacheki mnavyo uana.

Halafu nyie mna miminiana risasi maporini.

Ndio maana wanajeshi wakikaaga chini na kutafakari wanajiona walivyokuwa mafala.

Mwisho wa siku wanajiua.
Hapa kuna la kujifunza.
 
According tu sources nilizotumia ambazo ni media za Magharibi kama BBC, media za kujitegemea na documentary nilizoangalia ni kweli wanajiua. Kuna documentary inaitwa the heart of a soldier ndo inaelezea vizuri na hao wanajeshi walioenda huko wanahojiwa . Kama nimeingia kingi basi iko nje ya uwezo wangu kuelezea maana mimi sio mtaalamu
Hizo operation haijalishi ni media zipi zimeelezea.....

Kama huwa inadaiwa ni watu wa propaganda basi wanaweza kutengeneza habari yoyote ambayo wanaitaka wao...

Wasililize kwa ukaribu Former Soldiers& CIA agents ambao wamewahi kwenda field moja kwa moja utajua kwamba kuna mengi tunafichwa na hayatakiwi kuja hadharani....

Haiwezi kuwa by coincidence kwamba over 30k soldiers wajiue kwa sababu tu ya kujifeel guilty kwa waliyo yafanya under the order ya kutimiza wajibu wao japo sipingi kwamba wapo baadhi ambao wanaweza kujiua kutokana na tatizo la akili na sometimes kwa kujifeel guilty kwa ambayo wameyafanya....

Ndiyo maana these people sometimes are trained to kill.... Ingekuwa hivyo basi wangefika hata mamilioni kwa sababu daily wapo vitani kwenye mataifa mbali mbali.....

Hizo ni mission ambazo zinatengenezwa tu na wakubwa kwa ajili ya kutekeleza lengo au jambo Fulani bila kuacha trace....

Baadae ukifanyika uchunguzi inaonekana kwamba mtu amecommit suicide.......

Kuna movies kama BLACKLIST, FBI n.k Zina mengi sana kuhusu aina ya hizo cases .. Directors walijitahidi sana kwenda na uhalisia japo Haina maana kwamba kila kitu ni ukweli.... Ila hao jamaa sometimes huwa wanaweza kuwadedisha watu wao kulinda siri au kutafuta wa kumsingizia Incase wanataka kumtengenezea tatizo.... Ndiyo maana ni rare cases sana kukuta taifa Fulani linaua raia wa US hata kwa bahati mbaya na ikajulikana kwa Sababu they'll come for you kama ambavyo huwa wanatafuta uhalali wa kumpoteza Iran kwenye map ila Iran anaplay smart.

Binafsi siwezi kuamini kwamba ni coincidence tu... Kama kweli wamekufa kwa hiyo idadi basi sio mental illness bali Kuna kitu nyuma ya hayo mambo na ndiyo maana hata hizo operation za huko Afghanistan zilikuja kusimama.

They are US mkuu, they can tell whatever they want......

Tangu siku ambayo nilimuona Director wa FBI akilalamika bungeni kwamba DG wa CIA hamshirikishi kwenye taarifa za mhimu za nchi na ananyimwa access za ndani sana kuhusu security ya nchi yao na mwamba akamjibu hadharani kwamba kuna taarifa hata viongozi wakubwa hawatakiwi kujua....

Since then I knew these people live in lies, siri kubwa na ngumu sana...

Imagine Director wa FBI analalamika hivyo ambaye ni mkuu wa shirika la pili (la kwanza kwa ndani) la kijasusi kwa ukubwa US kati ya zaidi ya mashirika 17....

Binafsi naweza kuiamini taarifa yako vizuri ila kuhusu chanzo cha vifo binafsi siwezi kukiamini mkuu.
 
Naona War veterans mnachambua Mambo ya ughaibuni.
 
Vita si nzuri!

Kuna mwanajeshi mmoja alikuwa ananiambia wale waliyoenda kwenye mission tofauti tofauti wapo wanaodata.

Hao wamewekwa kambini ili wasilete madhara na wapo watu wanawafuatilia muda wote wasije kuleta madhara kwa wengine.
 
Kun movie inaitwq ghost of war ya 2020 inaelezea sababu za hawa watu kujiuaga wakirudi vitani. Mzee sio poa mawenge yake muarabu sio mtu kabisa
Screenshot_20241229_064746_Chrome.jpg
 
Ripoti zinasema, tangu uvamizi wa Marekani nchini Afghanistan na Iraq uliotokea baada ya Shambulio la September 11:

1. Zaidi ya askari 30,000 walioshiriki uvamizi huo wamejiua. Hii ni mara nne zaidi ya askari waliokufa vitani/ kwenye mapigano.

2. Mwaka 2019 pekee askari 6261 walijiua ikiwa ni ongezeko la asilimia saba kulinganishwa na takwimu za mwaka 2018.

3. Kwa wastani kwa siku askari 17 walioshiriki uvamizi nchini Iraq/ Afghanistan hujiua.

4. Visa vya kujiua miongoni mwa askari hao ni mara mbili zaidi ikilinganishwa na visa vya kujiua vinavyotokea miongoni mwa raia wa kawaida

5. Askari wengi wanaojiua wako kwenye kundi la umri kati ya miaka 18-34. Visa vya kujiua miongoni mwa kundi hili ni mara tatú zaidi ikilinganishwa na visa vya kujiua miongoni mwa askari walio na umri zaidi ya miaka 34.

CHANZO CHA TAKWIMU/ SOURCE:
"More Veterans Die By Suicide Than In Combat. But It's Preventable | Cognoscenti" More Veterans Die By Suicide Than In Combat. But It's Preventable

FUNZO: TATIZO LA AFYA YA AKILI LINAWEZA KUMKUTA MTU YOYOTE. USIOGOPE WALA USISITE KUOMBA MSAADA PALE UNAPOPATWA NA MAWAZO YA KUJIUA.
Wengi wao wana trauma kwa kiasi kikubwa hadi wengine walikuwa wanafuatiliwa wakihisiwa kuja kutenda uhalifu.
Kuna mmoja alirudi aliposikia ISIS imeanza kuchukua miji yani solo bila serikali kuwa na taarifa akazama Iraq na kujiunga ni kikundi cha kutoa misaada, baadaye alishuhudia ISIS wameua maiti zimetapakaa akaamua kushika abunduki na kuingia front line akisaidiana na majeshi ya Iraq pasipo hata nchi yake kujua. Walikuja kumwona kwenye footage jamaa akipigana na kuokoa raia.
Anasema alifanya hivyo kutokana na kwamba alikuwa anaona kusaidia raia ndicho kitu kitakachomsaidia kupunguza jinsi alivyokuwa akijisikia baada ya kutoka Iraq.
 
Hao sio inshu ya Afya ya Akili... Itakua kuna siri wamebeba hawatakiwi kuzisema.

Kwahyo wakiona wanashindwa kuvumilia kuzibeba wanajiua.
We unadhani ukatili walioufanya ni mdogo?
Jullian Assange si alitoa ushahidi wa ukatili wa askari wa Marekani Iraq!?
 
Hii habari umeinukuu wapi, mbona haina uhalisia?

Watu wapigane vita miaka ya 90 huko, halafu wagandishe umri wao, mpaka leo wabakie kuwa na miaka 34?
Duuuh vita za Iraq hazikutoa miaka ya 90 aisee umekosea.
Ni miaka ya 2000 kuja hadi 2008.
 
Tatizo majeneral wa USA na UK wate wanawafundisha ukatili kwenye atua mwisho wanaelekweza kuuwa watu atakama awana tatizo ili wapate uzoefu wakuuwa wanawaona wale wakulima uko Iraq na Afghanistan lkn wanaambiwa wauweni wote adi watoto wao nawao wanauwa mwisho nafsi zao zinakataa wanajilaumu wanatamani wasingewauwa au wawarudishe wawe hai kitu akiwezekani wanasafa sana na nafsi zao kuzulum nafsi bola pesa unaweza mrejeshea siku yoyote lkn kumpoka uhai wake iyo itakusumbua sana. Kila mala inakujia akilini ile picha au tukio lote. So wanaona bora wafe kuepukana na mchafukoge wa akili. Hii nitafaut na Soviet au Russia zaid wao miaka na miaka wanapigana kujilinda sio kuvamia hiii ya Ukraine ndio yakwanza kutuma majesh kuvamia japo tunajua msingi wake ni ule ule kuondosha kitisho jilan yake.
 
Ripoti zinasema, tangu uvamizi wa Marekani nchini Afghanistan na Iraq uliotokea baada ya Shambulio la September 11:

1. Zaidi ya askari 30,000 walioshiriki uvamizi huo wamejiua. Hii ni mara nne zaidi ya askari waliokufa vitani/ kwenye mapigano.

2. Mwaka 2019 pekee askari 6261 walijiua ikiwa ni ongezeko la asilimia saba kulinganishwa na takwimu za mwaka 2018.

3. Kwa wastani kwa siku askari 17 walioshiriki uvamizi nchini Iraq/ Afghanistan hujiua.

4. Visa vya kujiua miongoni mwa askari hao ni mara mbili zaidi ikilinganishwa na visa vya kujiua vinavyotokea miongoni mwa raia wa kawaida

5. Askari wengi wanaojiua wako kwenye kundi la umri kati ya miaka 18-34. Visa vya kujiua miongoni mwa kundi hili ni mara tatú zaidi ikilinganishwa na visa vya kujiua miongoni mwa askari walio na umri zaidi ya miaka 34.

CHANZO CHA TAKWIMU/ SOURCE:
"More Veterans Die By Suicide Than In Combat. But It's Preventable | Cognoscenti" More Veterans Die By Suicide Than In Combat. But It's Preventable

FUNZO: TATIZO LA AFYA YA AKILI LINAWEZA KUMKUTA MTU YOYOTE. USIOGOPE WALA USISITE KUOMBA MSAADA PALE UNAPOPATWA NA MAWAZO YA KUJIUA.
Kawaida inaitwa Podt war syndrome
 
Back
Top Bottom