Askari wa Marekani waliorudi nchini kwao baada ya kushiriki vita nchini Iraq na Afghanistan wanajiua kwa viwango vya juu

Askari wa Marekani waliorudi nchini kwao baada ya kushiriki vita nchini Iraq na Afghanistan wanajiua kwa viwango vya juu

Hata kama 2000+ umri wa miaka 18-34 kiuhalisia hawapo, watakuwa washavuka.
Piga hesabu kwa kutumia min age ya, 18 yrs.
Aliyeenda Iraq mfano mwaka 2008 akiwa na miaka 20 akajiua mwaka 2010 alifariki akiwa na miaka mingapi? Hii report inahusisha idadi ya waliojiua kuanzia miaka hiyo sio waliojiua mwaka huu
 
Ripoti zinasema, tangu uvamizi wa Marekani nchini Afghanistan na Iraq uliotokea baada ya Shambulio la September 11:

1. Zaidi ya askari 30,000 walioshiriki uvamizi huo wamejiua. Hii ni mara nne zaidi ya askari waliokufa vitani/ kwenye mapigano.

2. Mwaka 2019 pekee askari 6261 walijiua ikiwa ni ongezeko la asilimia saba kulinganishwa na takwimu za mwaka 2018.

3. Kwa wastani kwa siku askari 17 walioshiriki uvamizi nchini Iraq/ Afghanistan hujiua.

4. Visa vya kujiua miongoni mwa askari hao ni mara mbili zaidi ikilinganishwa na visa vya kujiua vinavyotokea miongoni mwa raia wa kawaida

5. Askari wengi wanaojiua wako kwenye kundi la umri kati ya miaka 18-34. Visa vya kujiua miongoni mwa kundi hili ni mara tatú zaidi ikilinganishwa na visa vya kujiua miongoni mwa askari walio na umri zaidi ya miaka 34.

CHANZO CHA TAKWIMU/ SOURCE:
"More Veterans Die By Suicide Than In Combat. But It's Preventable | Cognoscenti" More Veterans Die By Suicide Than In Combat. But It's Preventable

FUNZO: TATIZO LA AFYA YA AKILI LINAWEZA KUMKUTA MTU YOYOTE. USIOGOPE WALA USISITE KUOMBA MSAADA PALE UNAPOPATWA NA MAWAZO YA KUJIUA.
Kihoro
 
Vita ni upumbavu.

Yani mnauana kisa wanasiasa wawili wenye bifu. Wenyewe wamekaa ofisini kwao kwenye viti vya kuzunguka wakiwacheki mnavyo uana.

Halafu nyie mna miminiana risasi maporini.

Ndio maana wanajeshi wakikaaga chini na kutafakari wanajiona walivyokuwa mafala.

Mwisho wa siku wanajiua.
Well done brother, hakika unaona mbali sana sana. Sio tu Marekani wala Ulaya, check hawa wenzetu wa hapa Bongofleva/askarii, wanavyogawa dose kwa washiriki wa upande ule hata kutoa uhai kama sio kusababisha ulemawavu wa kudumu. Cha kushangaza, wanafanya hivyo kwa ndugu zao, marafiki zao, watanzania wenzao watoto wa ndugu zao. Kisa wanasiasa waendelee kuwa majukwaani na kula mema ya nchi. Nilishafanya hitimisho langu kuwa; PENGINE NDIO MAANA WANAWACHUKUWA F4 FAILURE, WANAOGOPA KUWACHUKUWA WATU WENYE AKILI ZAO KICHWANI, MAANA WANAWEZA WAGEUZIA KIBA MUDA WOWOTE. I stand to be corrected though.
 
Kazi ya watu wenye akili ndogo kabisa.
Yaani ule kwa kumbania makalio mwanadamu mwenzako.
Ufala sana
 
Post Traumatic Stress Disorder siyo hao tu hata wana waliopigana sana NAM iliwakuta sana... Achilia mbali hii ya UG mfano baada ya kupigwa ma saba saba yale ushawahi kuona nini mnakikuta kudata pia imo.
 
kubalina na wanaosema ni afya ya Akili, si uzima huo.
Kwanini ajihakishie kifo kwa asilimia 100 badala aitaje hiyo síri ili kuwepo na asilimia 50 za kunusurika kifo ikiwa haitajulikana kama yeye ndie alitevujisha Siri?
Kweli lakini. Mbona waliofanya kazi CIA wanatoa siri live YouTube interviews zao zipo na wengine hadi vitabu wanaandika . Ingawa ndo hivyo unajitoa kufa maana lazima wakufuatilie. Kuna huyo ex CIA agent niliona interview yake anadai alivyoanza kutoa siri walimuwekea sumu nyumbani kwake kwenye paa bila yéyé kujua. Kuja kushtuka,mke na watoto wanaumwa vibaya. Yéyé alinusurika maana alikuwa kasafiri wakati hiyo sumu imewekwa nyumbani kwake.
 
Hao askari wa miaka 18 wanaojiuwa vita walipigana huko Iraq lini. Au wakiwa na miaka 10
 
Vita ya Iraq na US iliyopigwa wakati wa Rais Bush (baba) ilikuwa miaka ya 90. Punguza ujuaji
Naona umevamia mada kichwa kichwa kenge wewe.
Mimi nazungumzia vita za USA VS Iraq zilizopelekea anguko la Saddam Hussein.
Zilizanzia miaka ya 2000 sio 1990.
Unakurupuka tu kujibu.
 
Back
Top Bottom