Askari wa Marekani waliorudi nchini kwao baada ya kushiriki vita nchini Iraq na Afghanistan wanajiua kwa viwango vya juu

Askari wa Marekani waliorudi nchini kwao baada ya kushiriki vita nchini Iraq na Afghanistan wanajiua kwa viwango vya juu

Hiyo article ni ya miaka 3 iliyopita.

Ni article ya NGO inayotaka michango ya kusaidia watu afya akili.

Article haikuweka wazi kuwa hao wanadai wanajiua walipigana vita Afghanistan

Hii sio authentic Source
 
5. Askari wengi wanaojiua wako kwenye kundi la umri kati ya miaka 18-34. Visa vya kujiua miongoni mwa kundi hili ni mara tatú zaidi ikilinganishwa na visa vya kujiua miongoni mwa askari walio na umri zaidi ya miaka 34.
Huu uzi umeandikwa jana. Lakini hii habari ni ya mwaka gani? Kama ni habari ya jana pia basi hilo kundi tajwa hapo juu halikuwa jeshini wakati wa uvamizi wa iran.
 
U.S. military suicides increased in 2023, continuing long-term trend​

By — Lolita C. Baldor, Associated Press
Nation Nov 14, 2024 2:02 PM EST
WASHINGTON (AP) — Suicides in the U.S. military increased in 2023, continuing a long-term trend that the Pentagon has struggled to abate, according to a Defense Department report released on Thursday. The increase is a bit of a setback after the deaths dipped slightly the previous year.
The number of suicides and the rate per 100,000 active-duty service members went up, but that the rise was not statistically significant. The number also went up among members of the Reserves, while it decreased a bit for the National Guard.

Ni kweli wanajeshi wa Marekani wanaijua sana
Watu wanaweza kuunganisha doti Kwa sababu hakuna vita ambayo wanajeshi wa Marekani wameua watu wengi kama vita ya Iraqi na Afghanistan
 
Huu uzi umeandikwa jana. Lakini hii habari ni ya mwaka gani? Kama ni habari ya jana pia basi hilo kundi tajwa hapo juu halikuwa jeshini wakati wa uvamizi wa iran.
Wanajeshi wa Marekani wameondoka Afghanistan mwaka 2021. Iraq hadi leo bado wapo ila sio active sana kwenye opearations kama miaka hiyo.Uvamizi haukuchukua mwaka mmoja tu
 
We unadhani ukatili walioufanya ni mdogo?
Jullian Assange si alitoa ushahidi wa ukatili wa askari wa Marekani Iraq!?
Nimekumbuka videos za Assange. Kuna hiyo moja wanajeshi wapo kwenye ndege wanaona watoto wanaenda shule wanapewa amri "fire" wanamimina risasi. Baadae gari la wagonjwa linakuja kubeba wale watoto, wanajeshi wanaambiwa tena" fire" wanamiminia risasi lile gari la wagonjwa. Waliomo mule wanakufa ila ananusurika mtoto mmoja. Huyo mtoto alivyokua mkubwa picha yake ikasambaa. Mwanajeshi mmojawapo wa Marekani aliewamiminia risasi siku ile akaenda kumtafuta kumuomba msamaha maana na yéyé alikuwa anaelekea kujiua akikumbuka ukatili alioufanya . Sio poa.
 
Vita ni upumbavu.

Yani mnauana kisa wanasiasa wawili wenye bifu. Wenyewe wamekaa ofisini kwao kwenye viti vya kuzunguka wakiwacheki mnavyo uana.

Halafu nyie mna miminiana risasi maporini.

Ndio maana wanajeshi wakikaaga chini na kutafakari wanajiona walivyokuwa mafala.

Mwisho wa siku wanajiua.
Kazi ya hovyo sitaki mtoto wangu aje kufanya asee,labda mi niwe sipo duniani,Yani usulubukie maslahi ya mwana siasa
 
Vita ni upumbavu.

Yani mnauana kisa wanasiasa wawili wenye bifu. Wenyewe wamekaa ofisini kwao kwenye viti vya kuzunguka wakiwacheki mnavyo uana.

Halafu nyie mna miminiana risasi maporini.

Ndio maana wanajeshi wakikaaga chini na kutafakari wanajiona walivyokuwa mafala.

Mwisho wa siku wanajiua.
Kwa nini wasigome kuenda vitani,ni mafala sana!
 
Ripoti zinasema, tangu uvamizi wa Marekani nchini Afghanistan na Iraq uliotokea baada ya Shambulio la September 11:

1. Zaidi ya askari 30,000 walioshiriki uvamizi huo wamejiua. Hii ni mara nne zaidi ya askari waliokufa vitani/ kwenye mapigano.

2. Mwaka 2019 pekee askari 6261 walijiua ikiwa ni ongezeko la asilimia saba kulinganishwa na takwimu za mwaka 2018.

3. Kwa wastani kwa siku askari 17 walioshiriki uvamizi nchini Iraq/ Afghanistan hujiua.

4. Visa vya kujiua miongoni mwa askari hao ni mara mbili zaidi ikilinganishwa na visa vya kujiua vinavyotokea miongoni mwa raia wa kawaida

5. Askari wengi wanaojiua wako kwenye kundi la umri kati ya miaka 18-34. Visa vya kujiua miongoni mwa kundi hili ni mara tatú zaidi ikilinganishwa na visa vya kujiua miongoni mwa askari walio na umri zaidi ya miaka 34.

CHANZO CHA TAKWIMU/ SOURCE:
"More Veterans Die By Suicide Than In Combat. But It's Preventable | Cognoscenti" More Veterans Die By Suicide Than In Combat. But It's Preventable

FUNZO: TATIZO LA AFYA YA AKILI LINAWEZA KUMKUTA MTU YOYOTE. USIOGOPE WALA USISITE KUOMBA MSAADA PALE UNAPOPATWA NA MAWAZO YA KUJIUA.
Kwa kiingereza wanaita "POST-TRAUMATIC STRESS DISORDER"

Yaani kiwewe anachokuwa nacho mtu punde baada ya kupitia kipindi fulani kigumu na cha kutisha..
 
Ata apo Gaza IDF wamefanya ukatili sana kwawatoto kwa watu wasio naatia washaanza kujiuwa wenyewe lkn idadi wanaficha chuki zao za DINI ya wengine ndio zinawaponza vita inamisingi yake sio mnavamia tu vijiji mnakuta Arusi mnawauwa watu wakiwemo bibi na bwana afu unaenda kwenu unajiuliza kosa Lao lipi mmewakuta watu wapo kwenye maisha yao wamama wabibi wasichana watoto ,,, tena wale Teleban mwanamke ashiki mtutu. Uwo ndio UGAID lkn wamiliki wa MEDIA niwao sasa wanajiuwa ovyo na wanawatibu sana lkn kuuwa ndugu kugumu. Asa wanawake na watoto wazee unaondoka na donda kubwa kwenye akili yko.
 
Mambo ya vitani sio mchezo hata vita ya Ukraine wengi wanajiua
 
Nimekumbuka videos za Assange. Kuna hiyo moja wanajeshi wapo kwenye ndege wanaona watoto wanaenda shule wanapewa amri "fire" wanamimina risasi. Baadae gari la wagonjwa linakuja kubeba wale watoto, wanajeshi wanaambiwa tena" fire" wanamiminia risasi lile gari la wagonjwa. Waliomo mule wanakufa ila ananusurika mtoto mmoja. Huyo mtoto alivyokua mkubwa picha yake ikasambaa. Mwanajeshi mmojawapo wa Marekani aliewamiminia risasi siku ile akaenda kumtafuta kumuomba msamaha maana na yéyé alikuwa anaelekea kujiua akikumbuka ukatili alioufanya . Sio poa.
Hata Israel pia askari wengi wana matatizo ya afya ya akili toka watoke Gaza.
Inaripotiwa zaidi ya askari 12k wapo rehab.
Damu ya mtu haswa ukiimwaga kikatili haiwezi kukuacha salama.
 
Hao sio inshu ya Afya ya Akili... Itakua kuna siri wamebeba hawatakiwi kuzisema.

Kwahyo wakiona wanashindwa kuvumilia kuzibeba wanajiua.
kubalina na wanaosema ni afya ya Akili, si uzima huo.
Kwanini ajihakishie kifo kwa asilimia 100 badala aitaje hiyo síri ili kuwepo na asilimia 50 za kunusurika kifo ikiwa haitajulikana kama yeye ndie alitevujisha Siri?
 
Back
Top Bottom