Askari wa Ukraine waliopelekwa Kursk wahoji sababu ya kupelekwa huko wakati Urusi ikifunga njia za kutokea.

Askari wa Ukraine waliopelekwa Kursk wahoji sababu ya kupelekwa huko wakati Urusi ikifunga njia za kutokea.

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
8,870
Reaction score
14,258
Askari kadhaa wa Ukraine wameonesha dalili za wazi za kujuta na kulaumu uamuzi wa kupelekwa huko wakati wakianza kuzingirwa na majeshi ya Urusi.

Kwa mujibu wa askari hao ambao hata majina yao hawakupenda kuwekwa hadharani ni kuwa maangamizi kwao yalianza tangu siku ya mwanzo ya jaribio lao na kwa sasa hali imekuwa ni ngumu zaidi.

Dalili za hatma zao kuwa ziko mashakani wamesema tayari wamewaona wapiganaji wa Wagner wakimwagwa kwenye jimbo hilo la Kursk ambao wamesema wanahisi wana mafunzo na silaha zaidi kuliko wao na hata jeshi la Urusi.

Ukraine’s Kursk offensive was seen as a major success, but it came at a huge cost

Hizo ni propaganda, kila jeshi lina war engineers hawa wao kazi yao ni kupima maji na unga, mpaka Ukraine wanaingia kule tayari walikuwa wameshajiridhisha namna ya kupigana wakiwa Kursk , pia ingekuwa ni rahisi tayari jeshi la Ukraine lingekuwa limeshusha, kila siku tunasikia Rusia afyeka jeshi la Ukraine sasa mbona hamalizi vita?
 
Naomba kuuliza nyie watalamu wa vita. Hivi askari wa Ukrain wanapokuwa wanasonga mbele huko Kursk maana yake nyuma yao si inakuwa ndio sehemu waliyoichukua? Sasa wakiona mambo ni magumu mbele yao si ina maana wanarudi nyuma? Sasa wanasubiri nini mpaka wazingirwe yaani nyuma yao? ina maana wanakuwa wamefanya makusudi kuzingirwa sasa ikiwa njia waliyoijia ndio wanatakiwa warudie
 
Sijui Zeleboy aliwaambia waelekee wapi baada ya kursk maana nasikia Wanazurula tu kwenye mapori kama nguruwe😁
 
Back
Top Bottom