Askari waliopambana na Hamza wapewa zawadi

Askari waliopambana na Hamza wapewa zawadi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
1632156977851.png

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, ametoa zawadi ikiwemo fedha na vyeti kwa maaskari polisi walioshiriki katika tukio la kupambana na Hamza aliyezua taharuki karibu na zilipo ofisi za ubalozi wa Ufaransa Dar es Salaam Agosti 25 mwaka huu.

Taarifa hiyo imetolewa leo Septemba 20, 2021, na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Muliro Jumanne Muliro.

"Askari hawa (Waliopambana na Hamza) miongoni mwao walikuwa ni Askari 11, ambao kwa mamlaka za kisheria za uendeshaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP amewapa zawadi ya vyeti vya ujasiri na zawadi ya pesa kwa kadri alivyoona inafaa," amesema Kamanda Muliro
 
Hilo gaidi lilioua askari sijui kwann lilipewa heshima ya kuzikwa
 
Kamanda muliro mchana huu amewatunukia zawadi za vyeti na pesa kwa mashujaa wetu wa jeshi la polisi waliojitoa mhanga kupambana na Hamnza wakafanikiwa kumuuwa

Katika ukurasa wa instagram wa millard ayo ameripoti tukio hilo lakini chakushangaza badala ya wananchi kupongeza jeshi letu wameonekana kuweka emoji za kucheka na kuwadhihaki mashujaa wetu kuwa hawakustahili kupewa zawadi eti walikuwa hawana shabaha
 
Back
Top Bottom