Askari wawili JWTZ wafa ajalini, wanne wajeruhiwa

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
ajali-pic.jpg

Askari wawili wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wa kikosi cha 825 KJ kambi ya Mtabila iliyopo wilayani Kasulu mkoani Kigoma, wamefariki dunia na wengine wanne kujeruhiwa baada ya gari walilokuwa wamepakia kuacha njia na kupinduka.

Kaimua Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Menrad Sindano amesema tukio hilo limetokea Julai 8, 2022, majira ya saa sita mchana katika eneo la Kidahwe, Wilaya ya Kigoma, Mkoani Kigoma.

Amesema gari aina ya Toyota Land Cruiser mali ya Jeshi la Wananchi ambalo lilikuwa likiendeshwa na askari is Ramadhani George, gari hiyo iliacha njia na kupinduka na kusababisha vifo vya askari wawili ambao ni Advent Peter (31) na Nicholaus Lonjino (31).

“Majeruhi ni askari wa nne ambao wamejeruhiwa sehemu mbalimbali za miili yao ambao ni Andrea Augustino, Ramadhani George, Manyama Fredrick na Ngongolima Misungwi ambapo kwasasa wote wanapatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa ya mkoa Maweni,” amesema.

Amesema majira ya mchana siku ya leo majeruhi wote wanatarajiwa kusafirishwa kwa njia ya ndege kwenda hospitali ya kijeshi Lugalo jijini Dar es Salaam kwa matibabu na uchunguzi zaidi.

Amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi na kwamba jeshi hilo limetoa wito kwa madereva wote kuendesha magari kwa kuchukua tahadhari hasa katika maeneo yenye kona na kufata sheria za usalama barabarani.
 
Inaonekana walikuwa 120+KPH. Wajifunze kuheshimu vyombo vya moto na watumiaji wengine.
 
Kiujumla askari wa jeshi wengi pamoja na polisi, ikiwa ni pamoja na madereva wa serikali, hawaheshimu KABISA usalama barabarani.
Askari kufa kizembe namna hii ni uhujumu uchumi.
Tumeonya humu mtandaoni mara nyingi bila kuona hatua zozote kuchukuliwa, na hii ni indiscpline ambayo CDF mpya Geberali Makunda analaswa kushughulikia.

Tulionya hapo nyuma.
 
Poleni kwa wafiwa wote na waliojeruhiwa wapate quick recovery, naona macho yangu hayaoni vema,paragraph ya mwisho imeandikwa majeruhi watapelekwa kwa ndege Lugalo Hospital?sio kwa gari au nimekua over sensitive hapa?
 
“majeruhi wote wanatarajiwa kusafirishwa kwa njia ya ndege kwenda hospitali ya kijeshi Lugalo jijini Dar es Salaam kwa matibabu na uchunguzi zaidi.”

Hii ndio Tanzania.
RIP Kid.
Ohooo mkuu kumbe nawe umesoma kama mimi, paragraph hiyo kuna watu wataungua sana kwa moto wa jehanamu ,yule mtoto angekua ni w DC wa kigoma, naamini asingefanya maamuzi yale ya kikatili,ila yule mtoto hana Jina kwa hiyo tupia huko kwenye another statistics, waliokufa njiani!
 
Inasikitisha sana Mkuu, hata week haijapita.
 
Tunasema kifo kinapangwa na Mungu mmmh wakati mwingine tunamtwisha Mungu mizigo.....
Wanajeshi polisi gari za serikali sijui mnaziita st ni waharibifu wanavunja sheria barabarani kuliko raia wa kawaida... Wanatumia kodi zetu vibaya mno hawana heshima wakatili wadhulumaji wajeuri na kikubwa zaidi ni ignorant... wamejigeuza miungu watu lakini Mungu naye huwa anawajibu kwa style hii kuwa yeye ni Mungu hakuna miungu wengine...
Jifunzeni kumwogopa Mungu ninyi mnaopewa mamlaka
 
Ila yule mtoto aliekatwa mapanga mkaona ndio akafie Morogoro Ila kweli alieshiba hamjui mwenye njaa
 
Kwa hyo yule mtoto waliamua kumuua makusudi

Kama Hawa wanapanda ndege lakn mtoto Tena malaika mkaamua kumpa shurba mateso ili afe mkifurahi

Hamna hata haya viongozi wa mkoa wa kigoma nikiwakuta paradiso nitashangaaa
 
Tunasema kifo kinapangwa na Mungu mmmh wakati mwingine tunamtwisha Mungu mizigo.....
Wanajeshi polisi gari za serikali sijui mnaziita st ni waharibifu wanavunja sheria barabarani kuliko raia wa kawaida... Wanatumia kodi zetu vibaya mno hawana heshima wakatili wadhulumaji wajeuri na kikubwa zaidi ni ignorant... wamejigeuza miungu watu lakini Mungu naye huwa anawajibu kwa style hii kuwa yeye ni Mungu hakuna miungu wengine...
Jifunzeni kumwogopa Mungu ninyi mnaopewa mamlaka
Wafe kwa wingi ndio watajirekesha, wanaonaga sifa kumbia speed wakati hawana dharula yeyote.
 
View attachment 2285457
Askari wawili wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wa kikosi cha 825 KJ kambi ya Mtabila iliyopo wilayani Kasulu mkoani Kigoma, wamefariki dunia na wengine wanne kujeruhiwa baada ya gari walilokuwa wamepakia kuacha njia na kupinduka.

Kaimua Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Menrad Sindano amesema tukio hilo limetokea Julai 8, 2022, majira ya saa sita mchana katika eneo la Kidahwe, Wilaya ya Kigoma, Mkoani Kigoma.

Amesema gari aina ya Toyota Land Cruiser mali ya Jeshi la Wananchi ambalo lilikuwa likiendeshwa na askari is Ramadhani George, gari hiyo iliacha njia na kupinduka na kusababisha vifo vya askari wawili ambao ni Advent Peter (31) na Nicholaus Lonjino (31).

“Majeruhi ni askari wa nne ambao wamejeruhiwa sehemu mbalimbali za miili yao ambao ni Andrea Augustino, Ramadhani George, Manyama Fredrick na Ngongolima Misungwi ambapo kwasasa wote wanapatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa ya mkoa Maweni,” amesema.

Amesema majira ya mchana siku ya leo majeruhi wote wanatarajiwa kusafirishwa kwa njia ya ndege kwenda hospitali ya kijeshi Lugalo jijini Dar es Salaam kwa matibabu na uchunguzi zaidi.

Amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi na kwamba jeshi hilo limetoa wito kwa madereva wote kuendesha magari kwa kuchukua tahadhari hasa katika maeneo yenye kona na kufata sheria za usalama barabarani.
Hapa najua 98% ya Watu watawalaumu hawa Wajeda kuwa Jeuri ya mwendo Kasi yao ndiyo imewaua.

Kwa tunaojua ya ndani hasa katika hizi Taasisi kwa jinsi Wanavyochukiana wakikosona Kuuana kwa Kurogana basi Mbinu mpya ya Siku hizi inayotumika ni wale wenye Nia mbaya nawe Kukulegezea Nati za Gari yako hasa wakijua kuwa una Safari ndefu na utasafiri na Watu wengine ambao Kwao wanaonekana ni Kikwazo cha Maslahi yao hapo Kazini.

Mtindo huu wa Kimafia umeshaua Wakubwa fulani barabarani ( Nawahifadhi ) Miaka ya hivi karibuni na nina Watu Wawili walinihakikishia kabisa kuwa tabia hii ipo na kuna Watu Maalum wamepelekwa Kusomeshwa Israel, Uingereza na Urusi ambao ndiyo Wabobezi Wakuu wa Uuaji huu ili wawe nao na Wautumie kwa wale Wanaohitajika na kuonekana ni Kero kwa Mamlaka.

Ninaomba niishie hapa tu tafadhali.
 
View attachment 2285457
Askari wawili wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wa kikosi cha 825 KJ kambi ya Mtabila iliyopo wilayani Kasulu mkoani Kigoma, wamefariki dunia na wengine wanne kujeruhiwa baada ya gari walilokuwa wamepakia kuacha njia na kupinduka.

Kaimua Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Menrad Sindano amesema tukio hilo limetokea Julai 8, 2022, majira ya saa sita mchana katika eneo la Kidahwe, Wilaya ya Kigoma, Mkoani Kigoma.

Amesema gari aina ya Toyota Land Cruiser mali ya Jeshi la Wananchi ambalo lilikuwa likiendeshwa na askari is Ramadhani George, gari hiyo iliacha njia na kupinduka na kusababisha vifo vya askari wawili ambao ni Advent Peter (31) na Nicholaus Lonjino (31).

“Majeruhi ni askari wa nne ambao wamejeruhiwa sehemu mbalimbali za miili yao ambao ni Andrea Augustino, Ramadhani George, Manyama Fredrick na Ngongolima Misungwi ambapo kwasasa wote wanapatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa ya mkoa Maweni,” amesema.

Amesema majira ya mchana siku ya leo majeruhi wote wanatarajiwa kusafirishwa kwa njia ya ndege kwenda hospitali ya kijeshi Lugalo jijini Dar es Salaam kwa matibabu na uchunguzi zaidi.

Amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi na kwamba jeshi hilo limetoa wito kwa madereva wote kuendesha magari kwa kuchukua tahadhari hasa katika maeneo yenye kona na kufata sheria za usalama barabarani.

Bora amesema chanjo cha ajali ni nini ningeshangaa sana
 
Back
Top Bottom