Askari wawili JWTZ wafa ajalini, wanne wajeruhiwa

Askari wawili JWTZ wafa ajalini, wanne wajeruhiwa

View attachment 2285457
Askari wawili wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wa kikosi cha 825 KJ kambi ya Mtabila iliyopo wilayani Kasulu mkoani Kigoma, wamefariki dunia na wengine wanne kujeruhiwa baada ya gari walilokuwa wamepakia kuacha njia na kupinduka.

Kaimua Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Menrad Sindano amesema tukio hilo limetokea Julai 8, 2022, majira ya saa sita mchana katika eneo la Kidahwe, Wilaya ya Kigoma, Mkoani Kigoma.

Amesema gari aina ya Toyota Land Cruiser mali ya Jeshi la Wananchi ambalo lilikuwa likiendeshwa na askari is Ramadhani George, gari hiyo iliacha njia na kupinduka na kusababisha vifo vya askari wawili ambao ni Advent Peter (31) na Nicholaus Lonjino (31).

“Majeruhi ni askari wa nne ambao wamejeruhiwa sehemu mbalimbali za miili yao ambao ni Andrea Augustino, Ramadhani George, Manyama Fredrick na Ngongolima Misungwi ambapo kwasasa wote wanapatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa ya mkoa Maweni,” amesema.

Amesema majira ya mchana siku ya leo majeruhi wote wanatarajiwa kusafirishwa kwa njia ya ndege kwenda hospitali ya kijeshi Lugalo jijini Dar es Salaam kwa matibabu na uchunguzi zaidi.

Amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi na kwamba jeshi hilo limetoa wito kwa madereva wote kuendesha magari kwa kuchukua tahadhari hasa katika maeneo yenye kona na kufata sheria za usalama barabarani.
Yule mtoto nae angepakizwa kwenye ndege angepona ila maskin hana haki🥲
 
Bora wangekufa wote, kwann wamebaki majeruhi? Ilibidi wote walambe ardhi, dadeki zao, safi sanaaa, na bado waishe wote.
 
Ohooo mkuu kumbe nawe umesoma kama mimi, paragraph hiyo kuna watu wataungua sana kwa moto wa jehanamu ,yule mtoto angekua ni w DC wa kigoma, naamini asingefanya maamuzi yale ya kikatili,ila yule mtoto hana Jina kwa hiyo tupia huko kwenye another statistics, waliokufa njiani!
Kuna mheshimiwa alizunguka na helicopter eti anapromote anuani za makazi huku mtoto anaepigania maisha anasafirishwa kwa gari kutoka Kigoma mpaka anafia njia! Hawa watu hawana hata aibu. Mungu awalaani.
 
Bora wangekufa wote, kwann wamebaki majeruhi? Ilibidi wote walambe ardhi, dadeki zao, safi sanaaa, na bado waishe wote.
[emoji16][emoji16] wali kwambia uogelee kwenye dimbwi la maji nini..sio kwa hii hasira
 
[emoji16][emoji16] wali kwambia uogelee kwenye dimbwi la maji nini..sio kwa hii hasira
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] yaan nikisikia vifo vya hao watu, mie moyo burudaaaaaniiii, ibilisi kwann aliwaacha wengine majeruhi, ilibidi anyofoe roho za waliokuwa ndani ya gari woteee.
 
Poleni kwa wafiwa wote na waliojeruhiwa wapate quick recovery, naona macho yangu hayaoni vema,paragraph ya mwisho imeandikwa majeruhi watapelekwa kwa ndege Lugalo Hospital?sio kwa gari au nimekua over sensitive hapa?
Au wapandishwe 1Hz [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
RIP mwanangu wa dhahabu Nico...mwendo umeumaliza
31560AEF-AAD7-433D-99E3-BED8691D8B69.jpeg
 
Back
Top Bottom