Ndiyo, wanatoa waraka ili utangazwe kwenye vyombo vya habari kama huu ulivyotolewa Machi 25, 2018 wakati wa awamu ya tano.
Baraza la Maaskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), limetoa waraka mzito wa ujumbe wa Sikukuu ya Pasaka ambao mbali ya kuzungumzia masuala ya kiroho, umetaja changamoto tatu na kuzifikisha kwa waumini wake “ili ziongeze mzigo wa kuliombea taifa letu na viongozi wake.”
Huo ni waraka wa pili kutoka kwa viongozi wa dini baada ya Februari mwaka huu, Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), kutoa ujumbe wa Kwaresma uliosaniwa na maaskofu 35 uliozungumzia masuala ya kisiasa, kiuchumi na kijamii.
Wameeleza kwamba kwa umoja wao na kwa nyakati za hivi sasa kuna matukio yaliyo kinyume na tunu na misingi iliyolilea Taifa inayoshuhudiwa; “Baadhi ya matukio hayo ni hofu iliyojengwa katika matukio halisi yakiwamo utekaji, utesaji, kupotea kwa watu, mashambulizi ya silaha dhidi ya viongozi wa kisiasa, mauaji yenye mwelekeo wa kiitikadi, vitisho, ubambikiziaji wa kesi, na matumizi mabaya ya vyombo vya dola dhidi ya wananchi.”