Askofu anamiliki HAMMER ya 250million!

Status
Not open for further replies.
Kiby, Hivi kumtetea askofu kuna kosa gani? maana si wote kwamba tutakuwa na mawazo yaliyo sawa. Najua leo kuna wengine wanaona iwe hivi na wengine tunaona tuwe hivi.
Namshangaa sana huyo anayekuomba nauli wewe kwenda kule kanisani maana maandiko yanatuzuia. Hata hivyo kuna kosa gani mtu kuomba msaada kwa jamii yake?
Leo hii wewe unatanua kwenye internet lakini kuna watu wanatamani hawawezi, sijui umewasaidia nini. Wengine wanatumia hata net za maofisini bure wakati kuna watu wanatamani hawawezi.
Jaribu kuelewa kuwa hapa duniani haitakuja kuwezekana watu wote tukawa sawa. Tunaishi mtaa mmoja na wote tunalipa same tax to the government lakini uwezo wetu na hata huduma kwetu huko huko mitaani inatofautiana. Hatuwezi kuwa sawa hata siku moja watu wote. Bado wahitaji wataendelea kuwapo na wenye uwezo wataendelea kuwepo. Na wote tunaishi mtaa mmoja huo huo.
Sijui kama umeelewa nini hasa point yangu.
 

Nyie mteteeni tu wakati yeye anaishi maisha ya kifahari kwa michango ya kila Jumapili kupitia waumini wakati waumini wakiwa na maisha ya kutisha halafu wanalalamika maisha magumu bei za vitu zimepanda wakati kila Jumapili wanamchangia askofu aendelee kutanua kupitia migongo yao! Hii michango yao ya kila Jumapili wangeielekeza SACCOS wangeweza kufanya mambo makubwa kuinua viwango vya maisha yao. Kweli wajinga ndiyo waliwao!
 

sijajaribu kumhukumu hatia rafiki yangu na jirani yangu kwa uhitaji wa nauli la hasha! Mimi sii wa tabia hiyo, nampenda kwa dhati na ni mmoja wa watu tunaobadilishana mawazo, yeye ni mchanga katika imani hajafikia bado hata miaka miwili ya wokovu. Nimekuwa nikimutia moyo na kumpa matumaini ya njia hiyo aliyoichagua, inayochukiwa na wengi bali hata hivyo ikiwa ndiyo njia nyoofu ya mbinguni. Nayadhamini maneno ya bwana yesu asemapo 'msiogope enyi kundi dogo, kwa kkuwa imempendeza baba yenu kuwapa huo ufalme. Amewaficha wenye hekima na maarifa wa dunia hii na amewafunulia watoto wachanga. Sasa nilichokuwa nataka kuonyesha pale ni tofauti kubwa iliyopo kati ya mtumishi na kondoo kwa sadaka zile zile za kondoo au kwa misaada itokanayo na kivuli cha kundi analoliongoza.
 
Wandugu kama mna Mjua Mungu kweli, ni bora mkamuona Mungu ndani ya wale Mafukara wanaoteseka bila msaada mkawape hayo mafungu ya 10/mbegu mkimwomba Mungu naye atawasaidia kuliko kwenda kuwapa hao jaa ambao wamesoma ujasiriamali na saikolojia wawekee mafuta ya laki3 kutanulia mjini. Imani huleta upofu tusipo kuwa makini ya Kibwetele yatajirudia Tz na yatakuwa makali zaidi.
 
Kweli hawa ni watu wa Mungu kweli?

MaxShibe hata ukifanyaje, ujanja au elimu ya kutapeli mpaka kupata hammer huwezi. Sijui kama utakwenda kupata Degree ya utapeli katika chuo cha injili huko massachust Marekani.
 
Kweli hawa ni watu wa Mungu kweli?

MaxShibe hata ukifanyaje, ujanja au elimu ya kutapeli mpaka kupata hammer huwezi. Sijui kama utakwenda kupata Degree ya utapeli katika chuo cha injili huko massachust Marekani.

Yesu anagawa Mahammer. Nashukuru kuwa umeelewa kuwa mimi sina elimu ya ujanja ujanja, kazi yangu ni elimu iliyo hai, na kupata kiuhalali.

Zaidi ya hapo, hakuna hata sehemu moja, kwenye Biblia inayo mkataza Mchungaji au Mwinjilisti kuwa na vitu vya kifahari.
 
Mwandishi wa hii habari naweza kumwita kuwa ni mzushi, wa kuokota taarifa toka gazeti la ajabu RISASI. Kama ulikuwa na taarifa nzuri ungefanya ufafiti kidogo kuhusu gari la Hammer na bei yake. Bei ya 250millioni ni uzushi mtupu usiokuwa na mwanzo wala mwisho.

Angalia bei ya magari ya Hummer kwa miundo tofauti:-

http://www.hummer.com/hummerjsp/home.jsp

Kisha bonyeza pricing & offers kwa magari mapya.

Kama unataka HUMMER iliyotumika utaipata hapa:-

http://www.tradecarview.com/used_car/japan%20car/hummer/all/?ps=25&so=1

Kama umepitia mtandao wa Hummer pia pitia mtandao wa Toyota angalia na linganisha matumizi ya mafuta ya aina hizo gari. Matumizi ya sh. 300,000/= kwa siku ni uwongo usiokuwa na kichwa wala miguu. Gari ya Hummer, Toyota Landcruiser VX, GX na Runner matumizi ya mafuta ni sawasawa.

http://www.toyotatz.com/index.php?id=46#c18
 
Nawe lako utagawiwa lini?

NB. Isome Biblia vizuri na uelewe yesu kasema nini kuhusu Matajiri yenye mahummer.

Halafu nitakuomba unukuu huo mstari hapa JF.
 
Soma maandiko ya Yesu juu ya matajiri, nafikiri wachungaji ni wanaadam vile vile na si dhani kuwa hayo hayawahusu.

Ukishamaliza kusoma inakili hapa JF hiyo mistali kwa faida ya wote.

Tatizo lenu hamsomi Biblia. Hapo sina la kuwasaidia.
 
Si wivu bali hali ya kipato cha waumini wako. Hata kama alipata msaada basi angewafikiria waumini wake kama kweli ana upendo.

Tafsiri ya UPENDO hueleweka sana kwa VITENDO.
 
wEWE UMESEMA na kwa hakika sijui kama jina lako ni Mubii au Nabii.

Nyie toeni tu, na toeni na na na ...... Usiulize pesa zako zimekwenda wapi.

Poleni ndugiu zangu. Kwani kutumia akili ni marufuku katika ukristo.
 
Kweli hawa ni watu wa Mungu kweli?

MaxShibe hata ukifanyaje, ujanja au elimu ya kutapeli mpaka kupata hammer huwezi. Sijui kama utakwenda kupata Degree ya utapeli katika chuo cha injili huko massachust Marekani.

Massachust ndiyo wapi? Hakuna sehemu Marekani kwa jina hilo. Kuna Massachusetts.
 
Ndio hao hao wakina nani??? Massachusetts ni state siyo mtu sasa ina kuaje hao?
Ndio state inayoongoza kwa ubora wa utoaji degree za utapeli katika mambo ya dini.

Ukisoma huko hiyo degree unaheshimika, kwani unakuwa na kipaji cha juu kabisa cha viini macho.
 
Ndio state inayoongoza kwa ubora wa utoaji degree za utapeli katika mambo ya dini.

Ukisoma huko hiyo degree unaheshimika, kwani unakuwa na kipaji cha juu kabisa cha viini macho.

It's hard to believe you because you couldn't even spell the place. So I doubt your words....I'm sorry.
 
Naona hapo ile kamuli ya

Ngania Vs Tundu la Sindano

ndio muda wake wa application
 
It's hard to believe you because you couldn't even spell the place. So I doubt your words....I'm sorry.
Kuspel sio taabu la msingi ni ujumbe, kwani hata mji wetu mkuu wa zamani au jiji maarufu Tanzania ni wachache wanaoweza kuspell kikamilifu.

Mwingine ataandika Daresalam, na wengine Daresalaam, hata Daresalama, na wengine Dalesalam na na na..... Na spell hizo zote si sahihi, lakini amini nakwambia utapozungumza au kuandika vyo vyote kati ya hayo juu mtanzania atakuelewa unamaanisha mji gani na hilo ndio kubwa. Japo maandiko sahihi ni Dar es salaam.

Hivyo ndugu yangu nashukuru kuwa ulinielewa sahihi toka mwanzo kuwa nilimaanisha state huko Marekani.

Mfano mwingine ni katika kichwa cha habari, ukweli Spell kamili ya Gari sahihi ni "HUMMER" na sio "HAMMER" lakini tulielewa ana maanisha nini kwa hiyo hakukuwa na haja ya kuleta gumzo lisilo na haja.
 
HAHAHAHA
kwa hiyo askofu anamiliki nyundo yenye thamani ya shs milioni miambili ushei hehehe

just kidin maana inakasirisha sana kuwakamua maskini kwa kujipa starehe duniani.

Hivi bank za mbinguni hazina money transfer ili tuwe tunatuma sadaka zetu straight halafu tunapeleka risit ktk vyombo vya sadaka?? hii itakomesha ufujaji wa hela zetu
 
We toa tu wala usiulize. Ha Ha Ha ......!!!!
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…