Askofu Bagonza ajiepushe na upindifu wa kimantiki unaoweza kuzaa taharuki ya kijamii bila uhalali

Swali kwa mama amoni ; Katika kueleza na bainisha Hoja ya msingi katika andiko lako hili , unatumia methodolojia gani ambayo ,kwanza inakubalika katika muktadha wa kifalsafa na hata dhana za kitaaluma ili kufikia hitimisho uliloweka ?!
Samahani, hebu weka vizuri swali lako ili nijibu kitu ninachokielewa.

Naona kama kuna skips katika aya yako. Naona umeandika hivi:

"Swali kwa mama amoni: Katika kueleza na (ku)bainisha hoja ya msingi katika andiko lako hili kwamba ............................................., unatumia methodolojia gani ambayo , kwanza inakubalika katika muktadha wa kifalsafa na hata dhana za kitaaluma ili kufikia hitimisho uliloweka kwamba ...........................................?"

Nitajibu baada ya wewe kukamilisha swali lako.

Karibu
 
Mama Amon mbona wewe unafaa kuwa mke kabisa, nilete mahari?
 
Too much

Paragraph mbili zingetosha
 
Umeelewa nini kati kati ya equivocations hizo?
Mimi ni Mfuasi wa Yesu Ambae Amefundisha!
[emoji116][emoji116]
Mark 2:17
[17]Yesu aliposikia aliwaambia, Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio hawawezi; sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi. Swali kuhusu Kufunga

Yesu Amefafanua kuhusu hilo!
[emoji116][emoji2534][emoji116][emoji2534]
Matthew 19:12
Maana wako matowashi waliozaliwa hali hiyo toka matumboni mwa mama zao; tena wako matowashi waliofanywa na watu kuwa matowashi; tena wako matowashi waliojifanya kuwa matowashi kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Awezaye kulipokea neno hili, na alipokee.

Yesu Ametuagiza!
[emoji116][emoji2534][emoji116][emoji2534]
Matthew 7:1-5
[1]Msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi.

[2]Kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa; na kipimo kile mpimiacho, ndicho mtakachopimiwa.

[3]Basi, mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe huiangalii?

[4]Au utamwambiaje nduguyo, Niache nikitoe kibanzi katika jicho lako; na kumbe! Mna boriti ndani ya jicho lako mwenyewe?

[5Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe; ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi katika jicho la ndugu yako. Kutweza Kitakatifu

Paulo Mtume wa Yesu Anakazia!
[emoji116][emoji2534][emoji116][emoji2534]
1 Corinthians 4:1,3-5
[1]Mtu na atuhesabu hivi, kuwa tu watumishi wa Kristo, na mawakili wa siri za Mungu.

[3]Lakini, kwangu mimi, si kitu kabisa nihukumiwe na ninyi, wala kwa hukumu ya kibinadamu, wala sijihukumu hata nafsi yangu.

[4] Maana sijui sababu ya kujishitaki nafsi yangu, lakini sihesabiwi haki kwa ajili hiyo; ila anihukumuye mimi ni Bwana.
[5]Basi ninyi msihukumu neno kabla ya wakati wake, hata ajapo Bwana; ambaye atayamulikisha yaliyositirika ya giza, na kuyadhihirisha mashauri ya mioyo; ndipo kila mtu atakapoipata sifa yake kwa Mungu.
 
Mkono wa kulia wa Mh.Bagonza umeshikana na mkono wa kulia wa Mh. Tundu.Lissu.
Ni ishara ya kusalimiana.
Mkono wa kushoto wa Mh.Lissu umeshika bega la kushoto la Mh.Bagonza.
Mkono ulioshika bega la kulia la Mh.Lissu ni mkono wa nani?
Mh.Bagonza ana mikono ya kulia mingapi?
 
Kwa hiyo Mungu aliumba vidole vyenye ishara ya ushoga?kwamba Mungu anaenda ushoga!je' Kwa Nini Mungu aliangamiza sodoma na gomora?
 
Nashauri serikali iwe na special task force ya kufanya operation angamiza mashoga,viroba ufukweni vitumike
 
Nadhan ifike wakat tuache kuzungumzia haya mambo mana kuzidi kuyaongelea ni kama tunayahubiri tunawatangaza tena bila hata malipo
 
Hii hoja yako ya vidole kuwa na ratio ya 2D : 4D unaonekana hata nawe ulikuwa huijui na kuiamini, kama unaijua, jiweke miongoni mwa hao wanaoamini hayo mambo, ili nijue naezungumza nae analiamini jambo analosemea, isije kuwa unatuletea hisia za wengine halafu unalazimisha na wengine tuziamini kama nyie.

Maneno uliyotumia kama "wafitini wa mambo" "kwa maoni yao" na "wakabeba hoja hiyo mitandaoni" yanaonesha umejitenga nao, wakati nawe umeibeba toka huko ulipoiona ukaileta hapa hivyo sioni tofauti yako nao, vyema utuambie wewe msimamo wako ni upi kuhusu hili suala, sababu unaonekana hujiamini, wala hukiamini unachozungumzia.

Kwangu mimi, sababu ya tofauti za kimaumbile haiwezi kuhusianishwa moja kwa moja na tabia za mtu, wanadamu tupo wengi wenye maumbile tofauti, na tabia tofauti, hivyo, kuzungumzia hiyo ratio ya vidole sioni uzito wa hoja yenu.
 
Bila-samahani, sasa nauliza vizuri swali langu . Katika kueleza na (ku) bainisha hoja ya msingi katika andiko hili kwamba " Upindifu wa kimantiki ni kosa la kimantiki ambapo mwongeaji hutunga hoja inayokiuka misingi bora ya usanifu wa hoja na uendeshaji wa mijadala."


Swali : Je unatumia methodolojia gani ,ambayo kwanza inakubalika katika muktadha wa kifalsafa na hata muktadha wa dhana za kitaaluma , ili kufikia hitimisho uliloliweka kwamba " Upindifu wa kimantiki ni kosa la kimantiki ambapo mwongeaji hutunga hoja inayokiuka misingi bora ya usanifu wa hoja na uendeshaji wa mijadala.".
 
Kifalsafa, methodolojia ya udadavuzi wa kimantiki inazingatia kanuni tano:

1. Law of noncontradiction
2. Law of excluded middle
3. Law of identity
4. Law of sufficient reason
5. Law of sound inference

Bagonza alivunja kanuni namba 4 kwa sababu ya ushahidi haba

Pia alivunja kanuni namba 5 kwa sababu ya equivocations
 
Nini maana ya usanifu bora wa hoja ?! Pia katika lugha ya kiswahili au kiingereza unatumia nadharia gani inayothibitisha usanifu wa hoja kujitosheleza kimaana na kimantiki
 
Nini maana ya usanifu bora wa hoja ?! Pia katika lugha ya kiswahili au kiingereza unatumia nadharia gani inayothibitisha usanifu wa hoja kujitosheleza kimaana na kimantiki
Umeuliza: "Nini maana ya usanifu bora wa hoja ?!"

Jawabu: Kwanza, maneno "usanifu bora wa hoja" yasomeke "usanifu wa hoja bora." Na "usanifu wa hoja bora" yana sehemu mbili. Kwanza ni "usanifu" na pili ni "hoja bora". Kusanifu kitu ni kuunda kitu kwa kukipa umbo fulani, yaani "designing a thing."

Hivyo, "usanifu wa hoja bora" ni uundaji wa hoja bora. Na "hoja bora" ni hoja yenye muundo bora, yaani muundo unaokubaliana na anatomia ya hoja, kama tukiongozwa na nadharia mamboleo za kimawazo kuhusu usanifu wa hoja. Ziko nadharia mbili, kuna nadharia ya Aristotle na nadharia ya Toulmin. Najadili hizi shule mbili katika kujibu swali lako la pili.

Umeuliza tena: "... unatumia nadharia gani inayothibitisha usanifu wa hoja kujitosheleza kimaana na kimantiki?"

Jawabu: Nadharia ya Aristotle wa Ugriki ya Kale inasema kuwa hoja bora inapaswa kuwa na muundo wenye sehemu tatu: dokezo kuu, dokezo dogo, na hitimisho. Mfano:

(1) Cheti cha kuzaliwa cha Bagonza kinasema alizaliwa Tanzania,

(2) Wazazi wa Bagonza wanasema kuwa alizaliwa Tanzania,

(3) Hivyo, Bagonza ni Raia wa Tanzania.

Na nadharia ya Stephen Toulmin wa Uingereza, ilibuniwa miaka ya 1960, na inaboresha nadharia ya Aristotle.

Inasme akuwa hoja bora inapaswa kuwa, sio na sehemu tatu kama alivyofundisha Aristotle, bali sehemu angalau sita zifuatazo:

(1) Tamko (claim),

(2) Uthibitisho wa kuunga mkoni tamko (ground),

(3) Utetezi wa kuunga mkoni uthibitisho (warrant),

(4) Msingi wa kuimarisha utetezi (backing),

(5) Pingamizi dhidi ya tamko (objection),

(6) Majibu ya pingamizi (rebuttal), na

(7) Mipaka ya tamko linalopendekezwa (qualifier/concession).

Mfano:

(1) Bagonza ni Raia wa Tanzania.

(2) Wazazi wa Bagonza wanasema kuwa alizaliwa Tanzania.

(3) Cheti cha kuzaliwa cha Bagonza kinasema alizaliwa Tanzania.

(4) Sheria ya uraia inasema kuwa kila mtu aliyezaliwa nchini Tanzania anakuwa na sifa ya uraia wa kuzaliwa.

(5) Huenda Bagonza ameshakana uraia wa Tanzania na kuchukua uraia wa nchi nyingine au ameshakufa.

(6) Hakuna ushahidi wowote wa kuthibitisho pingamizi hilo.

(7) Kama Bagonza hajakana uraia wa Tanzania na kuchukua uraia wa nchi nyingine na hajafa, basi tamko kuu hapo juu linasimama. Lakini, litaanguka kama ameshakana uraia wa Tanzania na kuchukua uraia wa nchi nyingine au ameshakufa.

Katika uwasilishaji wa mawazo kupitia maongezi ya kawaida pointi hizi saba zitaunganishwa hivi:

Kuna uwezekano mkubwa kwamba, (1) Bagonza ni Raia wa Tanzania, kwa sababu (2) Wazazi wa Bagonza wanasema kuwa alizaliwa Tanzania; na kwa kuzingatia kwamba, (3) Cheti cha kuzaliwa cha Bagonza kinasema alizaliwa Tanzania; na kutokana na ukweli kuwa, (4) Sheria ya uraia inasema kuwa kila mtu aliyezaliwa nchini Tanzania anakuwa na sifa ya uraia wa kuzaliwa; isipokuwa kama itathibitika kwamba, Bagonza ameshakana uraia wa Tanzania na kuchukua uraia wa nchi nyingine au ameshakufa, mapingamizi ambayo hayana ushahidi wa kuyaunga mkono kwa sasa.

Nawasilisha.

Kuna swali jingine?
 
Kanuni za usanifu wa hoja zinatutaka kutofautisha hoja na mleta hoja. Tujielekeze kwenye hoja. Nimesema kuwa, ni jukumu la Lissu na Bagonza kujitetea kuhusu tuhuma hizo mbili. Hakuna mtu mwingine anayeweza kuwatetea vizuri. Sababu ni mbili.

Mosi, mosi, Lissu ndiye anavijua vidole vyake vizuri. Anapaswa kutokea mbele ya kamera ya TV na kuweka bayana anatomia yake ili watu tuone vidole vyake vina muundo gani. Mojawapo ya picha hizi mbili, hapa chini, itajitokeza, nasi tutapata ushahidi wa awali kuhusu tuhuma hizo:



Pili, uwiano wa urefu wa kidole cha pili na cha nne (2D:4D ratio) sio confirmatory test ya ushoga wala kinyume chake.

Kuna tafiti zinaonyesha mashoga wenye vidole vyenye 2D:4D ratio ya kike, wapo mashoga wenye vidole vyenye 2D:4D ratio ya kiume, wapo wanaume wa kawaida wenye vidole vyenye 2D:4D ratio ya kike, wapo wanawake wa kawaida wenye vidole vyenye 2D:4D ratio ya kiume.

Ni kama ambavyo wako wanaume wenye sura za kike, na wanawake wenye sura za kiume, na maisha yanasonga mbele.

Confirmatory tests za ushoga ni mbili: hormone test pamoja na sexual orientation test. Kuhusu hili la pili, hakuna mtu mwingine anayeweza kutupa taarifa sahihi isipokuwa mtuhumiwa mwenyewe.

Maana yeye pekee ndiye anayeweza kujichunguza na kujifahamu vizuri kuanzia kwenye mtazamo wa nafsi ya kwanza, yaani from the first person perspective (introspection).

Mbali na hapo sisi watazamaji wa nje tutatambua mbetuko wa kimapenzi wa mtu kwa kuangalia tabia yake, yaani anapenda kutiana na kina nani.
 
Mleta hoja kusema ukweli ebu mtake radhi Mh.Lissu na Askofu Bagonza. Yaani umechukua vidole vya mkono wa mlinzi na msaidizi wa Mh.Lissu na kusema ni mkona wa Mh.Askofu Bagonza. Ili ni kosa kubwa sana,unataka kusema Askofu Bagonza ana mikono mitatu? Moderators ebu mkue makini na watu kama huyu
 
Ndugu, huwa sifanyi ujinga huo. Picha hiyo ipo kwenye ukurasa wa wanachadema wenyewe. Tazama hapa: Chadema in Blood. Ilibandikwa hapo 15 Desemba 2020. Naiposti tena hapa chini bila labels zangu, lakini kwa kuonyesha context ya mtandaoni ...



Picha zingine zilizo kwenye ukurasa wao hizi hapa:


Na hii....

Na hii....

Na hii....


Kwa ajili ya kukuondolea shaka kuhusu anatomia ya vidole vya Lissu, picha hii hapa inamaliza utata (iangalie vizuri):


Hii nayo nimeichakachua?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…