Askofu Bagonza ajiepushe na upindifu wa kimantiki unaoweza kuzaa taharuki ya kijamii bila uhalali

Swali kwa mama amoni ; Katika kueleza na bainisha Hoja ya msingi katika andiko lako hili , unatumia methodolojia gani ambayo ,kwanza inakubalika katika muktadha wa kifalsafa na hata dhana za kitaaluma ili kufikia hitimisho uliloweka ?!
Samahani, hebu weka vizuri swali lako ili nijibu kitu ninachokielewa.

Naona kama kuna skips katika aya yako. Naona umeandika hivi:

"Swali kwa mama amoni: Katika kueleza na (ku)bainisha hoja ya msingi katika andiko lako hili kwamba ............................................., unatumia methodolojia gani ambayo , kwanza inakubalika katika muktadha wa kifalsafa na hata dhana za kitaaluma ili kufikia hitimisho uliloweka kwamba ...........................................?"

Nitajibu baada ya wewe kukamilisha swali lako.

Karibu
 
View attachment 2515878
Bagonza akiwa amemkumbatia Lissu Kwenye Uwanja wa Kayanga, Karagwe, 2020. Kuhusu sababu mojawapo ya uzushi angalia tofauti kati ya urefu wa kidole cha pili na kidole cha nne, ambapo duara A ni vidole vya Bagonza (kidole cha pili kifupi kuliko kidole cha nne) na duara B ni vidole vya Lissu (kidole cha pili kirefu kuliko kidole cha nne).

Mwaka 2020 Bagonza alizushiwa zengwe kwamba ni rafki wa mashoga kwa sababu mbili.

Kwanzani ni kutokana na kujitokeza hadharani kwenye uwanja wa Kayanga, Karagwe, na kumsalimia Tundu Lissu, kwa kumkumbatia kama wafanyavyo wanyarwanda (kuhobherana).

Na pili, ni kutokana na tofauti za urefu wa vidole vya Lissu na Bagonza kwenye picha yao.

Vidole vya Bagonza (duara A) vinaonyesha kuwa kidole cha pili ni kifupi kuliko kidole cha nne.

Yaani, ukitafuta uwiano wa urefu wa kidole cha pili dhidi ya urefu wa kidole cha nne (2D:4D ratio) utapata namba iliyo ndogo kuliko moja.

Lakini, vidole vya Lissu (duara B) vinaonyesha kuwa kidole cha pili ni kirefu kuliko kidole cha nne.

Yaani, ukitafuta uwiano wa urefu wa kidole cha pili dhidi ya urefu wa kidole cha nne (2D:4D ratio) utapata namba iliyo kubwa kuliko moja.

Kwa mujibu wa maoni ya watu kwenye mitandao ya kijamii, wakati huo, kama mtu anakuwa na kidole cha pili ambacho ni kirefu kuliko kidole cha nne anakuwa na vidole vya kishoga, na hivyo ishara kwmaba yeye ni shoga.

Hivyo, watu hao walitumia mitandao ya kijamii kumvisha Lissu joho la ushoga kwa sababu hizi mbili.

Picha hiyo hapo juu, Bagonza anapoonekana kumkumbatia Lissu ilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii ikiwa na bandiko "acheni ushoga."

Kwa ajili ya kunusuru hali, jamaa asiyejulikana aitwaye "Kigogo2014" alitafuta picha za viongozi wa CCM wakiwa wanasalimiana kwa kukumbatiana kama alivyofanya Bagonza. Zengwe lililoanzishwa na kamati ya ufundi ya CCM likatulia.

Kigogo2014

Lissu aliondoka nchini bila kujibu tuhuma hizi. Na bagonza amekuwepo nchini muda wote bila kujibu tuhuma hizi.

Yaani, mpaka naandika uzi huu, hakuna majibu ya kukanusha ama tuhuma kwamba Lissu ni shoga au tuhuma kwamba ana vidole vya kishoga.
Lakini, mimi kama mwanasayansi, mtafiti na mwanafalsafa makini, ninao msimamo kwamba, "nadharia ya vidole vya kishoga" ni sayansi-koko, yaani "pseudo-science."

Lakini, linabaki jukumu ya Bagonza na Tundu Lissu kujibu tuhuma mbili zinazoelekezwa kwao.

Bagonza ni mwanazuoni ngazi ya uzamivu. Hivyo, naamini kwamba anapaswa kuwa na mawazo kama yangu kuhusu utata juu ya "nadharia ya vidole vya kishoga."

Hivyo, binafsi nilitarajia kwamba, Bagonza atakuwa miongoni mwa watu watakaopinga tabia ya watu kuvishwa "joho la ushoga" pasipo ushahidi unaokubalika kisayansi. Lakini, naona anafanya kinyume.

Leo, kupitia mitandai ya kijamii, Benson Bagonza ameripotiwa kutamka kauli zifuatazo:

"Sikubaliani na wanaodhani ushoga ni tatizo la Ulaya. Hapa kwetu [Tanzania] tayari hali inatisha. Imebaki kidogo mashoga wataunda umoja, watajenga nyumba zao za ibada, na serikali itaufyata. Wataunda chama chao na kuwania uongozi ... Tuamke."

Napendekeza kwamba maneno haya yanaambatana na utata mkubwa unaotokana na upindifu wa kimantiki na uhaba wa kimisamiati kwenye fikra za mwongeaji, kama nitakavyoonyesha.

Uhaba wa misamiati sahihi

Bagonza ametumia neno "ushoga" lenye maana angalu mbili, yaani "ulawiti" au "uhomofilia," bila kuzitofautisha maana hizi. Nataka kuonyesha tofauti zake kwa kina, na kisha kuonyesha kuwa neno uhomofilia lina maana nyingi pia.

Kwa upande mmoja, uhomofilia (homophilia) ni hali ya mtu kuvutiwa kimapenzi na watu wa jinsia yake.

Kuna aina mbili za uhomofilia . Kwa upande mmoja, hali ya mtu kuvutiwa kimapenzi na mwanamume inaitwa "uandrofilia," (androphilia), na uandrofilia kati ya wanaume wawili unazaa uhomofilia wa kiume (androphilia-androphilia attraction).

Homofilia wa kiume anayelawiti wenzake anaitwa basha, yaani "pedicon" kwa Kiingereza. Sio kila homofilia wa kiume ni basha.

Na homofilia wa kiume anayelawitiwa na wenzake anaitwa chicha, yaani "effeminate" kwa kimombo. Sio kila homofilia wa kiume ni chicha.

Kwa hiyo, kauli mwamba "mtu fulani anahusika na vitendo vya ulawiti wa kishoga" ni "questions begging," yaani inazalisha maswali kadhaa, yakiwemo yafuatayo: mtu huyo ni basha au chicha? kama ni chicha, basha wake nani? kama ni basha chicha wake nani?

Ni vivyo hivyo kwa tuhuma kwamba, "mtu fulani ni mwizi, mwongo, mzinzi, au mbakaji." Mwizi huiba kitu cha mtu baki, hivyo kitu na mmiliki wake lazima watajwe; mwongo hutoa tamko la uwongo dhidi ya mtu baki, hivyo tamko la uwongo na mtu aliyedanganywa lazima vitajwe; mzinzi hujamiiana na mke wa mtu baki, hivyo mke na mume wake lazima watajwe; na orodha inaendelea.

Bila kufanya hivyo, tunakuwa tunaongelea majungu, jambo ambalo ni kosa kubwa kufanywa na mwanazuoni. Kila mwanazuoni anapaswa kuheshimu kanuni ya "5W's and 1H".

Yaani, "what was done, where was it done, when was it done, who was the subject and who are the objects of the action, why was it done, and how was it done?"

Haya ni mswali kuhusu "6U's" katika Kiswahili, yaani: "unani, ulini, unini, uwapi, uvipi, usababu na utaratibu wa tukio au kitendo." Bagonza amekiuka kanuni hii.

Kwa upande mwingine, hali ya mtu kuvutiwa kimapenzi na mwanamke inaitwa "ugainefilia," (gynephilia), na ugainefilia kati ya wanawake wawili unazaa uhomofilia wa kike (gynephilia-gynephilia attraction).

Homofilia wa kike anayetumia jenitalia yake kuchua jenitalia ya mwanamke mwenzake anaitwa msagaji. Sio kila homofilia wa kike ni msagaji.

Na homofilia wa kike ambaye jenitalia yake ya kike inafanyiwa uchuaji kwa kutumia jenitalia ya mwanamke mwenzake anaitwa msagwaji. Sio kila homofilia wa kike ni msagwaji.

Kitendo cha wanawake wawili kusagana kinaitwa "tribadism" au "tribbing" au "scissooring" au "grinding," kwa Kiingereza. Msagaji anaitwa "tribber" na msagwaji anaitwa "tribbee"

Kinyume cha "uhomofilia" ni "uheterofilia" (heterophilia), yaani hali ya mtu kuvutiwa kimapenzi na watu wa jinsia tofauti na jinsia yake.

Yaani, uheterofilia hutokea pale ambapo mtu mwenye hali ya uandrofilia anapovutana kimapenzi na mtu mwenye ugainefilia (androphilia-gynephilia attraction).

Kuna maheterofilia wa aina tofauti kulingana na tabia zao.

Baadhi ya maheterofilia ni wazinzi na maheterofilia wengine sio wazinzi. Baadhi ya maheterofilia ni wabakaji na maheterofilia wengine sio wabakaji.

Baadhi ya maheterofilia ni waasherati na wengine sio waasherati. Baadhi ya maheterofilia ni walawiti na maheterofilia wengine sio walawiti.

Na sasa, kwa kuwa ulawiti unafanywa na mahomofilia pamoja na maheterofilia pia, hebu tuogelee tabia ya "ulawiti" kwa kina.

Hii ni tabia ya kufanya ngono kwa kuingiza jenitalia ya kiume kwenye mlango wa nyuma wa mfumo wa chakula, ama katika mwili wa mwanaume au mwanamke.

Yaani, Kuna ulawiti wa aina mbili. Kuna ulawiti wa kuingiza jenitalia ya kiume kwenye rektamu ya kike, na ulawiti wa kuingiza jenitalia ya kiume kwenye rektamu ya kiume.

Kitendo cha ulawiti wa kuingiza jenitalia ya kiume kwenye rektamu ya kiume kinaweza kufanywa na mtu mwenye uhomofilia wa kiume au mtu asiye na uhomofilia wa kiume.

Kwa hiyo, neno "ulawiti" sio kisawe cha neno "ushoga," maana ushoga ni hali ya kuwa na uhomofilia wakati ulawiti ni tabia. Sio kila shoga ni mlawiti, na sio kila mlawiti ni shoga.

Kwa hiyo, kunahitajika umakini tunapojadili mambo haya, maana hali haiwezi kuwa dhambi wala jinai. Lakini, tabia inaweza kuwa dhambi au jinao, au vyote kwa pamoja.

Upotofu wa kimantiki

Sasa tunaweza kuongelea upindifu wa kimantiki, yaani logical fallacy, katika maneno ya Bagonza.

Upindifu wa kimantiki ni kosa la kimantiki ambapo mwongeaji hutunga hoja inayokiuka misingi bora ya usanifu wa hoja na uendeshaji wa mijadala.

Kwa lugha nyingine, upindifu wa kimantiki ni upotofu wa kimantiki au upotofu wa maadili ya kimatiki.

Mifano ya upotofu wa kimantiki ni tabia ya kutumia neno lenye maana nyingi bila mwongeaji kueleza maana anayoikusudia na (equivocation).

Mfano ni "Juma amekalia mbuzi". Neno mbuzi linamaanisha mnyama au kifaa cha kukunia nazi. Katika maneno ya Bagonza, neno "shoga" linamaanisha ama "mlawiti" au "homofilia."

Na neno "homofilia" lina maana nne. Linamaanisha ama homofilia basha, au homofilia chicha, au homofilia asiye chicha, au homofilia asiye basha.

Kwa hiyo, mwongeaji akitumia neno "shoga" bila kufafanua maana anayokusudia hawezi kueleweka kwa watu wanaoueleea ukweli huu wote. Bagonza hakueleweka kwa sababu hii.

Mfano mwingine wa Upindifu wa kimantiki katika kauli za Baginza ni kuongelea kitu kilicho kwenye tabaka moja, kwa kukibebesha kimakosa sifa za kitu baki kilicho kwenye tabaka jingine (category mistake).

Mfano, sauti iko katika tabaka la vitu vinavyosikika, wakati harufu iko katika tabaka la vitu vinavyonusika. Lakini, mara nyingi utasikia watu wanasema, "nasikia harufu ya chakula."

Maneno haya yanaiweka dhana ya "harufu" katika kundi moja na dhana ya "sauti." Hili ni kosa la kuchanganya pamoja kada za vitu visivyopaswa kuwekwa pamoja.

Yaani, “we say that one has committed a category mistake when she ascribes, to a certain entity, a property or properties which that entity could not have... [meaning that] one locates some entity in a category it does not belong.” (Bernard Matolino, Personhood in African Philosophy (Dorpspruit: Cluster Publications; 2014, p. 142)

Hivyo, homofilia chicha, homofilia basha, homofilia asiye chicha, na homofilia asiye basha, na mlawiti asiye homofilia ni kada tano za watu, kila kada ikiwa na sifa zake za kitabia.

Bagonza ametumia neno "ushoga" ama kumaanisha "ulawiti" au "uhomofilia." Na neno "uhomofilia" linarejea maana zaidi ya moja, kama tulivyoona hapo juu.

Tofauti hizi zinayo maana kubwa katika ulimwengu wa maadili ambapo uadilifu wa mtu unapimwa kwa kuangalia dhamira ya mtendaji, kitendo alichofanya mtendaji na mazingira ya kitendo cha mtendaji.

Kwa mujibu wa nadharia hii ya kimaadili, homofilia wa kiume asiye chicha, na homofilia wa kiume asiye basha hawana kosa lolote la kimaadili.

Vivyo hivyo, homofilia wa kike asiye msagaji, na homofilia wa kike asiye msagwaji hawana kosa lolote la kimaadili.

Ni vivyo hivyo, kwa heterofilia asiye mlawiti, asiye mbakaji, asiye mzinzi, na heterofilia asiye mwasherati.

Lakini, heterofilia aliye mlawiti, aliye mbakaji, aliye mzinzi, na heterofilia aliye mwasherati ni hatari kwa jamii.

Ni kwa sababu hii, Bagonza anayehimiza mapambano dhidi ya makundi yote mahomofilia anakosea. Napinga kauli zake kwa sababu hii.

Kwa sababu hiyo hiyo, nitampinga mtu yeyote anayetangaza vita dhidi ya maheterofilia bila kutofautisha kati ya heterofilia asiye mlawiti, heterofilia asiye mbakaji, heterofilia asiye mzinzi, heterofilia asiye mwasherati, heterofilia aliye mlawiti, heterofilia aliye mbakaji, heterofilia aliye mzinzi, na heterofilia aliye mwasherati.

Ujenzi wa imani ya jamii yenye utulivu, haki, na amani haufanyiki vizuri kama tusipokuwa makini kuchanganua fikra zetu kwa kina katika kila jambo tunaloliongelea.

Hivyo niliona kuna haja ya kujadili mawazo yake kwa kina ili kusafisha akili za watumiaji wa mitandao ya kijamii.

Maana ya kauli za Bagonza katika muktadha mpana

Kwa upande mmoja, kama Bagonza anatumia neno "ushoga" kumaanisha "uhomofilia," ambayo ni sifa ya kimaumbile, kama ulivyo ufupi na urefu, weupe na weusi, ualibino na siualibino, njia pekee ya kupambana, kama anavyopendekeza, na "ushoga" ni kuwaua "mashoga" hao.

Hivyo, Bagonza hapa anahubiri tabia hatari ya uhomofobia. Sijui kama alitafakari vema juu ya uwezekano huu.

Lakini, pia Bagonza anapswa kutoa sababu nzuri ya kupambana na mahomofilia na kuacha kupambana na mazeruzeru, watu wenye tatizo la colour blindness, na matabaka ya pembezoni kama hayo.

Wote hawa wako hivyo kwa sababu za kimaumbile. Hawakuchagua hali zao.

Bagonza anasema kuwa "imebaki kidogo [mahomofilia] wataunda umoja, watajenga nyumba zao za ibada, ... wataunda chama chao na kuwania uongozi..."

Kwa maoni haya ya Bagonza, hata "mahomofilia" ambao sio machicha wala mabasha hawana haki hizi. Kwa kiwango hiki maoni yake nayapinga.

Urefu, ufupi, sauti nene, sauti nyororo, umashoto, umakengeza, uzeruzeru, colour blindness, na ladhalika, ni sifa asilia walizo nazo watu kadhaa.

Lakini watu hawa hawapotezi haki zao za kibayolojia, kisaikosomatika, kisiasa, kiuchumi na kijamii kwa sababu hiyo pekee.

Kwa upande mwingine, kama Bagonza anatumia neno "ushoga" kumaanisha "ulawiti" kuna maswali ya kitafiti anapaswa kutusaidia kuyajibu.

Tangu tupate uhuru tumefanya sensa mara tano. Hakuna takwimu za serikali zinaonyesha idadi ya mashoga nchini.

KIla mwaka serikali kupitia jeshi la Polisi na Idara ya takwimu (NBS) wanatoa takwimu za uhalifu kupitia kitabu kiitwacho TANZANIA IN FIGURES. Huku pia idadi ya mashoga haitajwi.

Lakini takwimu za mwaka 2021 zinaonyesha kuwa yalikuwepo matukio ya ulawiti 1,296.

Taarifa hiyo haisemi kama ulawiti huu ulifanywa dhidi ya wanaume au kama lifanywa dhidi ya wanawake au kama ulifanywa na mabasha au kama ulifanywa na walawiti wasio mahomofilia.

Lakini bado Bagonza anasema hakubaliani "na wanaodhani ushoga ni tatizo la Ulaya" kwa sababu tayari "hapa kwetu ... hali inatisha."

Bagonza anasema kuwa "imebaki kidogo [walawiti] wataunda umoja, watajenga nyumba zao za ibada, ... wataunda chama chao na kuwania uongozi...Tuamke."

Kwa maoni ya Bagonza, "mahomofilia" ambao ni machicha au mabasha hawana haki hizi kwa sabavu ya uhalifu wanaoufanya. Sawa. Lakini, sheria si zipo. Wanapaswa kuadhibiwa kwa kosa wanalotenda na sio zaidi ya hapo.

Lakini pia, msimamo huu haupaswi kuishia kwa wahalifu wa ulawiti pekee, kama Bagonza anavyoonekana kujielekeza.

Kwa mujibu wa taarifa ya serikali ya kila mwaka, iitwayo Tanzania in Figures, kuna makundi mengi ya uhalifu na yote yanapaswa kumulikwa na serikali.

Kauli za Bagonza zingeeleweka sana kama angesema hivi: "imebaki kidogo [wahalifu] wataunda umoja, watajenga nyumba zao za ibada, ... wataunda chama chao na kuwania uongozi... Tuamke."

Kwa kiwango hiki ningekubaliana na kauli za Bagonza. Hapa kuna wezi, wala rushwa, watu wanaotelekeza watoto mitaani, wafanya biashara ya binadamu, wateka watu, na orodha inaendelea.

Na takwimu halisi za kiserikali kupitia taarifa ya Tanzania in Figures ya kila mwaka, zinaonyesha kuwa baadhi ya watu hawa tayari wana makanisa, wengine ni wamiliki wa vyombo vya habari, wengine ni maaskofu kuanzia makanisa ya kipentekoste hadi Kanisa Katoliki, wengine ni wachungaji, na Bagonza anaujua ukweli huu fika. Hizi hapa:

View attachment 2439942

Lakini bado Bagonza kaamua kuibuka na habari ya "ushoga" isiyo na takwimu za kitafiti.

Mawazo yake yangeleweka na kukubalika zaidi kama angesema kuna "mashoga" wangapi kwenye kaya yake, ukoo wake, kijiji/mtaa wake wa Mwisho wa Lami, kata yake ya Kayanga, wilaya yake ya Karagwe, mkoa wake wa Kagera, na Tanzania kwa ujumla. Hakutoa takwimu zozote katika ngazi hizi.

Hivyo, napenda kumkumbusha kuwa, sifa tata za kimaumbile hazifuti haki za msingi za mahomofilia waadilifu, maalibino waadilifu, mashoto waadilifu, watu wenye makengeza waadilifu, nk.

Sifa hizo ni kama vile haki ya kuishi, kujumuika, kugombea nafasi za kisiasa, kupiga kura, kuabudu, kulindwa na serikali, na haki baki za kibinadamu.

Changamoto ya uhandisi wa maarifa ya kijamii (social constructionism)

Kwa maoni yangu, tamko la Bagonza linaanzia kwenye nadharia ya uhandisi wa maarifa ya kijamii (social constructionism), kama ilivyotumika kubunia "mtu hewa" aitwaye "Father Christmas."

Nadharia za uhandisi wa maarifa ya kijamii (social constructionism), hutengeneza maarifa ya kijamii kutokana na mapatano ya kibinadamu, kama asemavyo Profesa John Rogers Searle (Amerika).

View attachment 2438877
Profesa John Searle, mtalaama wa social constructionism iliyo msingi wa maadili yanayobadilika kwa sababu ya mazingira na iliyo mbadala kwa social realism iliyo msingi wa maadili yasiyobadilika kwa sababu ya mazingira

Katika maandiko yake, John Rogers Searle, kuhusu maarifa yanayotengenezwa kutokana na uhandisi wa kijamii, anataja kanuni kadhaa.

Kanuni moja inahusu "collective intentionality," nyingine inahusu "the assignment of status functions," na kanuni ya tatu inahusu "constitutive rules." Ninataka kuongelea hii kanuni ya tatu, ambayo ni kanuni ya kubuni na kutumia alama.

Kanuni hii inasema hivi: watu wanaweza kukaa wakakubaliana kwamba katika mazingira haya (X), kitu hiki (Y) kitakuwa alama inayowakilisha kitu kile (Z), na mapatano haya yatakoma pale watakapokaa tena na kukubaliana kuyabadilisha. (John R. Searle, Speech acts: An essay in the philosophy of language (Cambridge University Press; 1969, p. 34))

Mfano wake muhimu ni jumuiya ya wanampira waliokubaliana kuwa, katika mazigira ya uwanja wa mpira wa miguu (X), mchezaji akipokea mpira wakati anaelekea kufunga kwenye goli la mpizani wake wakati mbele yake hakuna mchezaji wa timu pinzani (Y), basi hilo ni kosa linaitwa offside (Z).

Kanuni hii inafaa kwenye mpira wa miguu pekee, na sio kwenye mpira wa mikono wala kwenye mpira wa kikapu.

Kwa hiyo, ikitokea siku wachezaji wa michezo yote hii wakajikuta wako pamoja kwa ajili ya mchezo mmoja, itabidi waunde kanuni mpya zinazokubalika kwa wote na kuwafaa wote. Ni vivyo hivyo kwenye maisha ya jamii mseto.

Yaani, kanuni zenye kutokana na mchakato wa mapatano ya kijamii (social constructionism) zinaweza kutumika kwenye jamii ya watu wenye imani moja, lakini sio kwenye jamii za leo ambako kuna utitiri wa kifikra (plural society).

Kwa mfano, wakati wa Papa Yohanne Paulo II, baadhi ya viongozi wa Kanisa Katoliki waliweka msimamo kwamba mahunta sio binadamu.

Mfano wa mwathirika ni Padre Selwyn Gross (jina la zamani la kiume) na baadaye Padre Sally Gross (jina jipya la kike), baada ya kubadilisha jinsia yake.

Hivyo, "Padre Sally Gross" aliyekuwa hunta (intersexual), alivuliwa upadre, kwa kuwa wanawake hawana haki ya kuwa mapadre.

Pia alifutiwa ubatizo kwa hoja kwamba mahunta sio binadamu, na hivyo hawana haki ya kubatizwa.

Mawazo kwamba "mahunta sio binadamu" ni zao la nadharia ya uhandisi wa kijamii (social constructionism) ndani ya Kanisa Katoliki kwa wakati ule wa Papa Yohanne Paul II.

Lakini, leo hii sayansi mamboleo inathibitisha kwamba mahunta wana kromozomu 46 kama watu baki walioko kwenye ukoo wa homosapiensia.

Yaani kumwondoa Padre Sally kwenye tabaka la binadamu ulikuwa ni uamuzi wenye sura ya "category mistake," na ulitokana na matumizi mabaya ya kanuni za uhandisi wa maarifa ya kijamii ndani ya Kanisa Katoliki.

Leo, Kanisa Katoliki sasa limejisahihishana halibebi tena mawazo yale potofu kuhusu hulka ya mahunta. Kanuni za maumbile zimelileta karibu na ukweli asilia.

Kwa sasa bado Kanisa Katoliki linapambana na fundisho lake tata kwamba "a copulating pair is a biological organism"

Fundisho hili ni zao la mradi wa uhandisi wa maarifa ya kijamii (social constructionism) ulioanza miaka ya 1968. Lakini, ni fundisho linalopingana na kanuni za kibayolojia na kifalsafa.

Kifalsafa, neno "organism" lina maana kuu mbili. Yaani "biological organism" kama vile binadamu na kondoo; na "social organism" kama vile familia na timu a mpira.

Ufanano wake ni kwamba, aina zote mbili ni mifumo yenye sehemu nyingi zinazofanya kazi kwa kushirikiana bila kupingana kwa ajili ya kufanikisha lengo la pamoja (organismality).

Tofauti moja kati ya "biological organism" na "social organism" ni kwamba, wakati "kanuni ya uratibu" iko ndani ya mfumo uitwao "biological organism," kanuni hiyo iko nje ya mfumo uitwao "social organism."

Tofauti nyingine kati ya "biological organism" na "social organism" ni kwamba, kiungo cha mwili wa "biological organism" kikikatwa kinakufa, lakini kiungo cha mwili wa "social organism" kikikatwa kinabaki hai, na kinaweza kuunganishwa tena na kuwa sehemu ya "social organism".

Mfano, mchezaji wa mpira wa miguu akipewa kadi nyekundi anaondoka uwanjani na anabaki hai. Akisamehewa anarejea kwenye timu.

Lakini, mkono wako ukikatawa kwa panga hadi kutenganishwa na mwili wako utaoza na baada ya hapo hauwezi kurejeshwa kuwa sehemu ya mwili wako.

Kwa upande mwingine uhai wa "social organism" unaanzia na kukomea kwenye mapatano ya wanajamii husika, kwa maana kwamba, sehemu za kitu kizima zinaanza kuwepo kabla ya kitu hicho kizima kuwepo.

Lakini uhai wa "biological organism" hautokani na mapatano ya viungo vya mwili, maana viungo hivyo huota baada ya kitu kizima kuwepo.

Kwa sababu hizi, sasa ulimwengu wa wanasayansi unakubaliana kwamba, kwa sehemu kubwa "a copulating pair is a social organism," na sio "biological organism."

Huu ni mtazamo unaopingana na mawazo ya baadhi ya makuwadi wa "metafizikia ya umoja wa kimwili," yaani, "metaphysics of bodily union"

Wataalam wa falsafa ya kibayolojia (philosophical biology) hapa wamesaidia sana kuleta mapinduzi ya kifikra yanayotakiwa kuhusiana na swali hili hapa: "what is a biological individual?"

Hitimisho na mapendekezo

Kwa hiyo, napendekeza kwamba, njia pekee ya kujenga imani ya jamii inayokubalika kwa watu wote katika jamii yenye mapokeo mseto sio kutumia kanuni za uhandisi wa maarifa ya kijamii kwa njia ya kura (social constructionism) au kwa kutumia "kanuni za taharuki ya kijamii isiyo na uhalali" (unwarranted moral panic)

Badala yake, tunapaswa kuanzia kwenye kanuni za maadili asilia yanayoweza, na yanayopaswa, kuthibitika kwa njia ya urazini huru miongoni mwa umma mpana (public reason).

Bila kukubaliana na ukweli huu, kazi ya ujenzi wa imani ya jamii yenye imani mseto itakwama, maana mwafaka wa kijamii ni ajenda ya mpito tu.

Mwisho, niseme tu kuwa, katika mradi huu wa kujenga imani ya jamii, wadau wote, yaani wanateolojia, wanasayansi asilia, wanasayansi ya jamii, wanafalsafa, wanasasiolojia, wanahistoria, wanasheria, walei, makasisi, na wanazuoni baki wanayo nafasi.

Lakini, mchango wa kila mmoja una mipaka inayokamilishwa na michango ya wenzake.

Mfano, kwenye Safina ya Nuhu tunaambiwa kuwa Nuhu aliagizwa kuweka kila kiumbe kwa kuzingatia kanuni ya ME na KE.

Lakini, leo hii sayansi inatwambia kuwa kuna viumbe havina mgawanyo huo wa ME na KE. Mfano ni minyoo. Kwa hiyo, mwandishi wa Agano la Kale hakuwa na habari ya ukweli huu wa viumbe wasio na mgawanyo wa jinsia ya ME na KE.

Na hii maana yeke ni kwamba, wanateolojia wanaofanya udadavuzi kwa kuanzia kwenye Biblia wanahitaji kuelimishwa na wanabayolojia katika suala ya asexual reporoduction. Biblia haina mamlaka katika jambo hili.

Vivyo hivyo, Biblia haina mamlaka juu ya fenomena ya "ushoga" katika ujumla wake. Biblia inaongelea "ulawiti," yaani "pedication," basi.

Kwa mfano, haitwambii kama umati wa watu wote wa Sodoma waliotaka kufanya kitendo cha ulawiti walikuwa ni mashoga au hapana.

Na hata kama ingesema hivyo, tusingeamini taarifa kwamba umati wa watu 50 na zaidi walikuwa ni mashoga.

Kwa hiyo wanateolojia wanaoongozwa na Biblia hawana mamlaka ya kutuhubiria juu ya topiki ya "ushoga" kama ilivyojadiliwa katika uzi huu.

Ukweli ni kwamba, kila wanapojaribu wanapotosha jamii. Mfano, ibara za 2357 na 2358 katika Katekisimu ya Kanisa Katoliki ya mwaka 1992 zinasema hivi kuhusu ushoga (homosexuality):

2357 Homosexuality refers to relations between men or between women who experience an exclusive or predominant sexual attraction toward persons of the same sex. It has taken a great variety of forms through the centuries and in different cultures. Its psychological genesis remains largely unexplained.
Basing itself on Sacred Scripture, which presents homosexual acts as acts of grave depravity, tradition has always declared that "homosexual acts are intrinsically disordered"... (emphasisi by underlining added)
2358 The number of men and women who have deep-seated homosexual tendencies is not negligible. This (is an ) inclination... (emphasisi by underlining added).

Katika nukuu hii, kuna makundi matatu ya maneno yafuatayo yenye kuzalisha utata wa kimantiki: "Homosexuality refers to relations," "homosexual acts," "homosexual tendencies," na "this (is an ) inclination."

Katika vishazi hivi vinne, vishazi vitatu vya mwisho vinazalisha hitimisho kwamba, "homosexuality refers to a condition."

Lakini, Katekisimu hiyo hiyo inasema kuwa "homosexuality refers to relations." Huu ni mkanganyiko wa kimantiki ndani ya Katekisimu.

Kwa sababu hii, ni wazi kuwa Kamati ya Kipapa iliyoandika Katekisimu hii, chini ya Kiranja Mkuu wa Imani wa wakati huo, Kardinali Ratzinger, hawakuwa na weledi kamilifu juu ya mada ya uhomofilia, uheterofilia, na ulawiti.

Ni kama hawakujua tofauti kati ya "hali ya ushoga" yaani "homosexual condition," "tabia ya ulawiti wa kishoga" yaani "homosexual pedication," na "tabia ya ulawiti usio wa kishoga" yaani "non-homosexual pedication,"

Tofauti hizi ndio msingi wa kanuni za kisheria zinazoangalia kitendo na dhamira ya mtendaji, yaani "actus reus (the physical element)" na "mensi rea (the mental element)."

Hii ni tofauti kati ya "the intention to commit the unlawful act " dhidi ya "the unlawful act committed ."

Kwa maana hii, "homosexuality condition" haiwezi kuwa "dhambi (sin)" wala "jinai (crime)." Lakini, "homosexual pedication" inaweza kuwa "dhambi (sin)," "jinai (crime)," au yote mawili.

Katika hili, wanasayansi, wanasheria na wanamaadili wanapaswa kushirikiana katika kujenga imani ya jamii.

Basi, kwa ujumla, sote tunakamilishana kimaarifa, na hivyo kuna haja ya kuunganisha nguvu katika kufanikisha mradi wa kujenga imani ya jamii yenye utulivu, haki na amani kkwa kuanzia kwenye misingi ya uhalisia asilia (social realism) badala ya kukimbilia kwenye unadisi wa maarifa ya kijamii kwa njia ya kura (social constructionism).

Tujenge hoja bila mihemuko wala taharuki.
Mama Amon mbona wewe unafaa kuwa mke kabisa, nilete mahari?
 
Too much

Paragraph mbili zingetosha
 
Umeelewa nini kati kati ya equivocations hizo?
Mimi ni Mfuasi wa Yesu Ambae Amefundisha!
[emoji116][emoji116]
Mark 2:17
[17]Yesu aliposikia aliwaambia, Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio hawawezi; sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi. Swali kuhusu Kufunga

Yesu Amefafanua kuhusu hilo!
[emoji116][emoji2534][emoji116][emoji2534]
Matthew 19:12
Maana wako matowashi waliozaliwa hali hiyo toka matumboni mwa mama zao; tena wako matowashi waliofanywa na watu kuwa matowashi; tena wako matowashi waliojifanya kuwa matowashi kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Awezaye kulipokea neno hili, na alipokee.

Yesu Ametuagiza!
[emoji116][emoji2534][emoji116][emoji2534]
Matthew 7:1-5
[1]Msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi.

[2]Kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa; na kipimo kile mpimiacho, ndicho mtakachopimiwa.

[3]Basi, mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe huiangalii?

[4]Au utamwambiaje nduguyo, Niache nikitoe kibanzi katika jicho lako; na kumbe! Mna boriti ndani ya jicho lako mwenyewe?

[5Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe; ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi katika jicho la ndugu yako. Kutweza Kitakatifu

Paulo Mtume wa Yesu Anakazia!
[emoji116][emoji2534][emoji116][emoji2534]
1 Corinthians 4:1,3-5
[1]Mtu na atuhesabu hivi, kuwa tu watumishi wa Kristo, na mawakili wa siri za Mungu.

[3]Lakini, kwangu mimi, si kitu kabisa nihukumiwe na ninyi, wala kwa hukumu ya kibinadamu, wala sijihukumu hata nafsi yangu.

[4] Maana sijui sababu ya kujishitaki nafsi yangu, lakini sihesabiwi haki kwa ajili hiyo; ila anihukumuye mimi ni Bwana.
[5]Basi ninyi msihukumu neno kabla ya wakati wake, hata ajapo Bwana; ambaye atayamulikisha yaliyositirika ya giza, na kuyadhihirisha mashauri ya mioyo; ndipo kila mtu atakapoipata sifa yake kwa Mungu.
 
Mkono wa kulia wa Mh.Bagonza umeshikana na mkono wa kulia wa Mh. Tundu.Lissu.
Ni ishara ya kusalimiana.
Mkono wa kushoto wa Mh.Lissu umeshika bega la kushoto la Mh.Bagonza.
Mkono ulioshika bega la kulia la Mh.Lissu ni mkono wa nani?
Mh.Bagonza ana mikono ya kulia mingapi?
 
Kwa hiyo Mungu aliumba vidole vyenye ishara ya ushoga?kwamba Mungu anaenda ushoga!je' Kwa Nini Mungu aliangamiza sodoma na gomora?
 
Nashauri serikali iwe na special task force ya kufanya operation angamiza mashoga,viroba ufukweni vitumike
 
Nadhan ifike wakat tuache kuzungumzia haya mambo mana kuzidi kuyaongelea ni kama tunayahubiri tunawatangaza tena bila hata malipo
 
Sijaongelea jambo hili. Usipotoshe.

Hoja hapa sio mashoga wako upande wa CCM wala upande wa CHADEMA.

Bali hoja ilianzia kwenye vidole vya Lisu siku ile akiwa Kayanga, Karagwe Kagera.

Wafitini wa mambo wakasema kidole cha pili cha Lissu ni kirefu kuliko kidole cha nne cha Lissu. Yaani ukitafuta 2D:4D ratio ya vidole vyake unapata namba kubwa kuliko moja.

Kwa maoni yao, watu wente 2D:4D ratio iliyo kubwa kuliko moja ni mashoga.

Hivyo, wakabeba hoja hiyo mitandaoni. Kwa hiyo maswali yanayohitaji majibu ni mawili:

(1) Je, ni kweli kwamba 2D:4D ratio ta vidole vya Lissu ni kubwa kuliko moja?

(Yaani, ni kweli kwamba kidole cha pili cha Lissu ni kirefu kuliko kidole chake cha nne?)

(2) Na kama 2D:4D ratio ya Lissu ni kubwa kuliko moja, takwimu hiyo inamaanisha kuwa Lissu ni shoga?

(Yaani, ni kweli kwamba kama kidole cha pili cha Lissu ni kirefu kuliko kidole chake cha nne, hiyo maana yake ni kwamba Lissu ni shoga?)

View attachment 2515820
Hii hoja yako ya vidole kuwa na ratio ya 2D : 4D unaonekana hata nawe ulikuwa huijui na kuiamini, kama unaijua, jiweke miongoni mwa hao wanaoamini hayo mambo, ili nijue naezungumza nae analiamini jambo analosemea, isije kuwa unatuletea hisia za wengine halafu unalazimisha na wengine tuziamini kama nyie.

Maneno uliyotumia kama "wafitini wa mambo" "kwa maoni yao" na "wakabeba hoja hiyo mitandaoni" yanaonesha umejitenga nao, wakati nawe umeibeba toka huko ulipoiona ukaileta hapa hivyo sioni tofauti yako nao, vyema utuambie wewe msimamo wako ni upi kuhusu hili suala, sababu unaonekana hujiamini, wala hukiamini unachozungumzia.

Kwangu mimi, sababu ya tofauti za kimaumbile haiwezi kuhusianishwa moja kwa moja na tabia za mtu, wanadamu tupo wengi wenye maumbile tofauti, na tabia tofauti, hivyo, kuzungumzia hiyo ratio ya vidole sioni uzito wa hoja yenu.
 
Samahani, hebu weka vizuri swali lako ili nijibu kitu ninachokielewa.

Naona kama kuna skips katika aya yako. Naona umeandika hivi:

"Swali kwa mama amoni: Katika kueleza na (ku)bainisha hoja ya msingi katika andiko lako hili kwamba ............................................., unatumia methodolojia gani ambayo , kwanza inakubalika katika muktadha wa kifalsafa na hata dhana za kitaaluma ili kufikia hitimisho uliloweka kwamba ...........................................?"

Nitajibu baada ya wewe kukamilisha swali lako.

Karibu
Bila-samahani, sasa nauliza vizuri swali langu . Katika kueleza na (ku) bainisha hoja ya msingi katika andiko hili kwamba " Upindifu wa kimantiki ni kosa la kimantiki ambapo mwongeaji hutunga hoja inayokiuka misingi bora ya usanifu wa hoja na uendeshaji wa mijadala."

Swali : Je unatumia methodolojia gani ,ambayo kwanza inakubalika katika muktadha wa kifalsafa na hata muktadha wa dhana za kitaaluma , ili kufikia hitimisho uliloliweka kwamba " Upindifu wa kimantiki ni kosa la kimantiki ambapo mwongeaji hutunga hoja inayokiuka misingi bora ya usanifu wa hoja na uendeshaji wa mijadala.".
 
Kifalsafa, methodolojia ya udadavuzi wa kimantiki inazingatia kanuni tano:

1. Law of noncontradiction
2. Law of excluded middle
3. Law of identity
4. Law of sufficient reason
5. Law of sound inference

Bagonza alivunja kanuni namba 4 kwa sababu ya ushahidi haba

Pia alivunja kanuni namba 5 kwa sababu ya equivocations
 
Nini maana ya usanifu bora wa hoja ?! Pia katika lugha ya kiswahili au kiingereza unatumia nadharia gani inayothibitisha usanifu wa hoja kujitosheleza kimaana na kimantiki
 
Umeuliza: "Nini maana ya usanifu bora wa hoja ?!"

Jawabu: Kwanza, maneno "usanifu bora wa hoja" yasomeke "usanifu wa hoja bora." Na "usanifu wa hoja bora" yana sehemu mbili. Kwanza ni "usanifu" na pili ni "hoja bora". Kusanifu kitu ni kuunda kitu kwa kukipa umbo fulani, yaani "designing a thing."

Hivyo, "usanifu wa hoja bora" ni uundaji wa hoja bora. Na "hoja bora" ni hoja yenye muundo bora, yaani muundo unaokubaliana na anatomia ya hoja, kama tukiongozwa na nadharia mamboleo za kimawazo kuhusu usanifu wa hoja. Ziko nadharia mbili, kuna nadharia ya Aristotle na nadharia ya Toulmin. Najadili hizi shule mbili katika kujibu swali lako la pili.

Umeuliza tena: "... unatumia nadharia gani inayothibitisha usanifu wa hoja kujitosheleza kimaana na kimantiki?"

Jawabu: Nadharia ya Aristotle wa Ugriki ya Kale inasema kuwa hoja bora inapaswa kuwa na muundo wenye sehemu tatu: dokezo kuu, dokezo dogo, na hitimisho. Mfano:

(1) Cheti cha kuzaliwa cha Bagonza kinasema alizaliwa Tanzania,

(2) Wazazi wa Bagonza wanasema kuwa alizaliwa Tanzania,

(3) Hivyo, Bagonza ni Raia wa Tanzania.

Na nadharia ya Stephen Toulmin wa Uingereza, ilibuniwa miaka ya 1960, na inaboresha nadharia ya Aristotle.

Inasme akuwa hoja bora inapaswa kuwa, sio na sehemu tatu kama alivyofundisha Aristotle, bali sehemu angalau sita zifuatazo:

(1) Tamko (claim),

(2) Uthibitisho wa kuunga mkoni tamko (ground),

(3) Utetezi wa kuunga mkoni uthibitisho (warrant),

(4) Msingi wa kuimarisha utetezi (backing),

(5) Pingamizi dhidi ya tamko (objection),

(6) Majibu ya pingamizi (rebuttal), na

(7) Mipaka ya tamko linalopendekezwa (qualifier/concession).

Mfano:

(1) Bagonza ni Raia wa Tanzania.

(2) Wazazi wa Bagonza wanasema kuwa alizaliwa Tanzania.

(3) Cheti cha kuzaliwa cha Bagonza kinasema alizaliwa Tanzania.

(4) Sheria ya uraia inasema kuwa kila mtu aliyezaliwa nchini Tanzania anakuwa na sifa ya uraia wa kuzaliwa.

(5) Huenda Bagonza ameshakana uraia wa Tanzania na kuchukua uraia wa nchi nyingine au ameshakufa.

(6) Hakuna ushahidi wowote wa kuthibitisho pingamizi hilo.

(7) Kama Bagonza hajakana uraia wa Tanzania na kuchukua uraia wa nchi nyingine na hajafa, basi tamko kuu hapo juu linasimama. Lakini, litaanguka kama ameshakana uraia wa Tanzania na kuchukua uraia wa nchi nyingine au ameshakufa.

Katika uwasilishaji wa mawazo kupitia maongezi ya kawaida pointi hizi saba zitaunganishwa hivi:

Kuna uwezekano mkubwa kwamba, (1) Bagonza ni Raia wa Tanzania, kwa sababu (2) Wazazi wa Bagonza wanasema kuwa alizaliwa Tanzania; na kwa kuzingatia kwamba, (3) Cheti cha kuzaliwa cha Bagonza kinasema alizaliwa Tanzania; na kutokana na ukweli kuwa, (4) Sheria ya uraia inasema kuwa kila mtu aliyezaliwa nchini Tanzania anakuwa na sifa ya uraia wa kuzaliwa; isipokuwa kama itathibitika kwamba, Bagonza ameshakana uraia wa Tanzania na kuchukua uraia wa nchi nyingine au ameshakufa, mapingamizi ambayo hayana ushahidi wa kuyaunga mkono kwa sasa.

Nawasilisha.

Kuna swali jingine?
 
Maneno uliyotumia kama "wafitini wa mambo" "kwa maoni yao" na "wakabeba hoja hiyo mitandaoni" yanaonesha umejitenga nao, wakati nawe umeibeba toka huko ulipoiona ukaileta hapa hivyo sioni tofauti yako nao, vyema utuambie wewe msimamo wako ni upi kuhusu hili suala, sababu unaonekana hujiamini, wala hukiamini unachozungumzia.
Kanuni za usanifu wa hoja zinatutaka kutofautisha hoja na mleta hoja. Tujielekeze kwenye hoja. Nimesema kuwa, ni jukumu la Lissu na Bagonza kujitetea kuhusu tuhuma hizo mbili. Hakuna mtu mwingine anayeweza kuwatetea vizuri. Sababu ni mbili.

Mosi, mosi, Lissu ndiye anavijua vidole vyake vizuri. Anapaswa kutokea mbele ya kamera ya TV na kuweka bayana anatomia yake ili watu tuone vidole vyake vina muundo gani. Mojawapo ya picha hizi mbili, hapa chini, itajitokeza, nasi tutapata ushahidi wa awali kuhusu tuhuma hizo:

1676447094289.png

Pili, uwiano wa urefu wa kidole cha pili na cha nne (2D:4D ratio) sio confirmatory test ya ushoga wala kinyume chake.

Kuna tafiti zinaonyesha mashoga wenye vidole vyenye 2D:4D ratio ya kike, wapo mashoga wenye vidole vyenye 2D:4D ratio ya kiume, wapo wanaume wa kawaida wenye vidole vyenye 2D:4D ratio ya kike, wapo wanawake wa kawaida wenye vidole vyenye 2D:4D ratio ya kiume.

Ni kama ambavyo wako wanaume wenye sura za kike, na wanawake wenye sura za kiume, na maisha yanasonga mbele.

Confirmatory tests za ushoga ni mbili: hormone test pamoja na sexual orientation test. Kuhusu hili la pili, hakuna mtu mwingine anayeweza kutupa taarifa sahihi isipokuwa mtuhumiwa mwenyewe.

Maana yeye pekee ndiye anayeweza kujichunguza na kujifahamu vizuri kuanzia kwenye mtazamo wa nafsi ya kwanza, yaani from the first person perspective (introspection).

Mbali na hapo sisi watazamaji wa nje tutatambua mbetuko wa kimapenzi wa mtu kwa kuangalia tabia yake, yaani anapenda kutiana na kina nani.
 
View attachment 2515878
Bagonza akiwa amemkumbatia Lissu Kwenye Uwanja wa Kayanga, Karagwe, 2020. Kuhusu sababu mojawapo ya uzushi angalia tofauti kati ya urefu wa kidole cha pili na kidole cha nne, ambapo duara A ni vidole vya Bagonza (kidole cha pili kifupi kuliko kidole cha nne) na duara B ni vidole vya Lissu (kidole cha pili kirefu kuliko kidole cha nne).

Mwaka 2020 Bagonza alizushiwa zengwe kwamba ni rafki wa mashoga kwa sababu mbili.

Kwanzani ni kutokana na kujitokeza hadharani kwenye uwanja wa Kayanga, Karagwe, na kumsalimia Tundu Lissu, kwa kumkumbatia kama wafanyavyo wanyarwanda (kuhobherana).

Na pili, ni kutokana na tofauti za urefu wa vidole vya Lissu na Bagonza kwenye picha yao.

Vidole vya Bagonza (duara A) vinaonyesha kuwa kidole cha pili ni kifupi kuliko kidole cha nne.

Yaani, ukitafuta uwiano wa urefu wa kidole cha pili dhidi ya urefu wa kidole cha nne (2D:4D ratio) utapata namba iliyo ndogo kuliko moja.

Lakini, vidole vya Lissu (duara B) vinaonyesha kuwa kidole cha pili ni kirefu kuliko kidole cha nne.

Yaani, ukitafuta uwiano wa urefu wa kidole cha pili dhidi ya urefu wa kidole cha nne (2D:4D ratio) utapata namba iliyo kubwa kuliko moja.

Kwa mujibu wa maoni ya watu kwenye mitandao ya kijamii, wakati huo, kama mtu anakuwa na kidole cha pili ambacho ni kirefu kuliko kidole cha nne anakuwa na vidole vya kishoga, na hivyo ishara inayozalisha kwamba yeye ni shoga. Tazama picha ifuatazo ili kuelewa vema msingi wa tuhuma.
View attachment 2518121

Hivyo, watu hao walitumia mitandao ya kijamii kumvisha Lissu joho la ushoga kwa sababu hizi mbili.

Picha hiyo hapo juu, Bagonza anapoonekana kumkumbatia Lissu ilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii ikiwa na bandiko "acheni ushoga."

Lissu alimaliza kampeni na kuondoka nchini bila kujibu tuhuma hizi. Na bagonza amekuwepo nchini muda wote bila kujibu tuhuma hizi pia.

Yaani, mpaka naandika uzi huu, hakuna majibu ya kukanusha ama tuhuma kwamba Lissu ni shoga au tuhuma kwamba ana vidole vya kishoga.

Lakini, mimi kama mwanasayansi, mtafiti na mwanafalsafa makini, ninao msimamo kwamba, "nadharia ya vidole vya kishoga" ni sayansi-koko, yaani "pseudo-science."

Ukweli ninaoufahamu ni kwamba wapo mashoga wana kidole cha pili kirefu kuliko cha nne, na wapo mashoga wenye kidole cha pili kifupi kuliko kidole cha nne.

Hivyo, takwimu za uwiano wa urefu wa vidole ni ushahidi wa awali katika kuthibitisha tuhuma za ushoga. Kuna ushahidi mwingie wa kisayansi unahitajika ili kuthibitisha au kukanusha tuhuma.

Linabaki ni jukumu la Bagonza na Tundu Lissu kujibu tuhuma mbili zinazoelekezwa kwao.

Bagonza ni mwanazuoni ngazi ya uzamivu. Hivyo, naamini kwamba anapaswa kuwa na mawazo kama yangu kuhusu utata juu ya "nadharia ya vidole vya kishoga."

Hivyo, binafsi nilitarajia kwamba, Bagonza atakuwa miongoni mwa watu watakaopinga tabia ya watu kuvishwa "joho la ushoga" pasipo ushahidi unaokubalika kisayansi. Lakini, naona anafanya kinyume.

Leo, kupitia mitandai ya kijamii, Benson Bagonza ameripotiwa kutamka kauli zifuatazo:

"Sikubaliani na wanaodhani ushoga ni tatizo la Ulaya. Hapa kwetu [Tanzania] tayari hali inatisha. Imebaki kidogo mashoga wataunda umoja, watajenga nyumba zao za ibada, na serikali itaufyata. Wataunda chama chao na kuwania uongozi ... Tuamke."

Napendekeza kwamba maneno haya yanaambatana na utata mkubwa unaotokana na upindifu wa kimantiki na uhaba wa kimisamiati kwenye fikra za mwongeaji, kama nitakavyoonyesha.

Uhaba wa misamiati sahihi

Bagonza ametumia neno "ushoga" lenye maana angalu mbili, yaani "ulawiti" au "uhomofilia," bila kuzitofautisha maana hizi. Nataka kuonyesha tofauti zake kwa kina, na kisha kuonyesha kuwa neno uhomofilia lina maana nyingi pia.

Kwa upande mmoja, uhomofilia (homophilia) ni hali ya mtu kuvutiwa kimapenzi na watu wa jinsia yake.

Kuna aina mbili za uhomofilia . Kwa upande mmoja, hali ya mtu kuvutiwa kimapenzi na mwanamume inaitwa "uandrofilia," (androphilia), na uandrofilia kati ya wanaume wawili unazaa uhomofilia wa kiume (androphilia-androphilia attraction).

Homofilia wa kiume anayelawiti wenzake anaitwa basha, yaani "pedicon" kwa Kiingereza. Sio kila homofilia wa kiume ni basha.

Na homofilia wa kiume anayelawitiwa na wenzake anaitwa chicha, yaani "effeminate" kwa kimombo. Sio kila homofilia wa kiume ni chicha.

Kwa hiyo, kauli mwamba "mtu fulani anahusika na vitendo vya ulawiti wa kishoga" ni "questions begging," yaani inazalisha maswali kadhaa, yakiwemo yafuatayo: mtu huyo ni basha au chicha? kama ni chicha, basha wake nani? kama ni basha chicha wake nani?

Ni vivyo hivyo kwa tuhuma kwamba, "mtu fulani ni mwizi, mwongo, mzinzi, au mbakaji." Mwizi huiba kitu cha mtu baki, hivyo kitu na mmiliki wake lazima watajwe; mwongo hutoa tamko la uwongo dhidi ya mtu baki, hivyo tamko la uwongo na mtu aliyedanganywa lazima vitajwe; mzinzi hujamiiana na mke wa mtu baki, hivyo mke na mume wake lazima watajwe; na orodha inaendelea.

Bila kufanya hivyo, tunakuwa tunaongelea majungu, jambo ambalo ni kosa kubwa kufanywa na mwanazuoni. Kila mwanazuoni anapaswa kuheshimu kanuni ya "5W's and 1H".

Yaani, "what was done, where was it done, when was it done, who was the subject and who are the objects of the action, why was it done, and how was it done?"

Haya ni mswali kuhusu "Usita wa Herufi ya 'U' katika Ripoti Kamilifu", yaani "6U's" zifuatazo: "unani, ulini, unini, uwapi, uvipi, usababu na utaratibu wa tukio au kitendo." Bagonza amekiuka kanuni hii ya
"Usita wa Herufi ya 'U' katika Ripoti Kamilifu."

Kwa upande mwingine, hali ya mtu kuvutiwa kimapenzi na mwanamke inaitwa "ugainefilia," (gynephilia), na ugainefilia kati ya wanawake wawili unazaa uhomofilia wa kike (gynephilia-gynephilia attraction).

Homofilia wa kike anayetumia jenitalia yake kuchua jenitalia ya mwanamke mwenzake anaitwa msagaji. Sio kila homofilia wa kike ni msagaji.

Na homofilia wa kike ambaye jenitalia yake ya kike inafanyiwa uchuaji kwa kutumia jenitalia ya mwanamke mwenzake anaitwa msagwaji. Sio kila homofilia wa kike ni msagwaji.

Kitendo cha wanawake wawili kusagana kinaitwa "tribadism" au "tribbing" au "scissooring" au "grinding," kwa Kiingereza. Msagaji anaitwa "tribber" na msagwaji anaitwa "tribbee"

Kinyume cha "uhomofilia" ni "uheterofilia" (heterophilia), yaani hali ya mtu kuvutiwa kimapenzi na watu wa jinsia tofauti na jinsia yake.

Yaani, uheterofilia hutokea pale ambapo mtu mwenye hali ya uandrofilia anapovutana kimapenzi na mtu mwenye ugainefilia (androphilia-gynephilia attraction).

Kuna maheterofilia wa aina tofauti kulingana na tabia zao.

Baadhi ya maheterofilia ni wazinzi na maheterofilia wengine sio wazinzi. Baadhi ya maheterofilia ni wabakaji na maheterofilia wengine sio wabakaji.

Baadhi ya maheterofilia ni waasherati na wengine sio waasherati. Baadhi ya maheterofilia ni walawiti na maheterofilia wengine sio walawiti.

Na sasa, kwa kuwa ulawiti unafanywa na mahomofilia pamoja na maheterofilia pia, hebu tuogelee tabia ya "ulawiti" kwa kina.

Hii ni tabia ya kufanya ngono kwa kuingiza jenitalia ya kiume kwenye mlango wa nyuma wa mfumo wa chakula, ama katika mwili wa mwanaume au mwanamke.

Yaani, Kuna ulawiti wa aina mbili. Kuna ulawiti wa kuingiza jenitalia ya kiume kwenye rektamu ya kike, na ulawiti wa kuingiza jenitalia ya kiume kwenye rektamu ya kiume.

Kitendo cha ulawiti wa kuingiza jenitalia ya kiume kwenye rektamu ya kiume kinaweza kufanywa na mtu mwenye uhomofilia wa kiume au mtu asiye na uhomofilia wa kiume.

Kwa hiyo, neno "ulawiti" sio kisawe cha neno "ushoga," maana ushoga ni hali ya kuwa na uhomofilia wakati ulawiti ni tabia. Sio kila shoga ni mlawiti, na sio kila mlawiti ni shoga.

Kwa hiyo, kunahitajika umakini tunapojadili mambo haya, maana hali haiwezi kuwa dhambi wala jinai. Lakini, tabia inaweza kuwa dhambi au jinao, au vyote kwa pamoja.

Upotofu wa kimantiki

Sasa tunaweza kuongelea upindifu wa kimantiki, yaani logical fallacy, katika maneno ya Bagonza.

Upindifu wa kimantiki ni kosa la kimantiki ambapo mwongeaji hutunga hoja inayokiuka misingi bora ya usanifu wa hoja na uendeshaji wa mijadala.

Kwa lugha nyingine, upindifu wa kimantiki ni upotofu wa kimantiki au upotofu wa maadili ya kimatiki.

Mifano ya upotofu wa kimantiki ni tabia ya kutumia neno lenye maana nyingi bila mwongeaji kueleza maana anayoikusudia na (equivocation).

Mfano ni "Juma amekalia mbuzi". Neno mbuzi linamaanisha mnyama au kifaa cha kukunia nazi. Katika maneno ya Bagonza, neno "shoga" linamaanisha ama "mlawiti" au "homofilia."

Na neno "homofilia" lina maana nne. Linamaanisha ama homofilia basha, au homofilia chicha, au homofilia asiye chicha, au homofilia asiye basha.

Kwa hiyo, mwongeaji akitumia neno "shoga" bila kufafanua maana anayokusudia hawezi kueleweka kwa watu wanaoueleea ukweli huu wote. Bagonza hakueleweka kwa sababu hii.

Mfano mwingine wa Upindifu wa kimantiki katika kauli za Baginza ni kuongelea kitu kilicho kwenye tabaka moja, kwa kukibebesha kimakosa sifa za kitu baki kilicho kwenye tabaka jingine (category mistake).

Mfano, sauti iko katika tabaka la vitu vinavyosikika, wakati harufu iko katika tabaka la vitu vinavyonusika. Lakini, mara nyingi utasikia watu wanasema, "nasikia harufu ya chakula."

Maneno haya yanaiweka dhana ya "harufu" katika kundi moja na dhana ya "sauti." Hili ni kosa la kuchanganya pamoja kada za vitu visivyopaswa kuwekwa pamoja.

Yaani, “we say that one has committed a category mistake when she ascribes, to a certain entity, a property or properties which that entity could not have... [meaning that] one locates some entity in a category it does not belong.” (Bernard Matolino, Personhood in African Philosophy (Dorpspruit: Cluster Publications; 2014, p. 142)

Hivyo, homofilia chicha, homofilia basha, homofilia asiye chicha, na homofilia asiye basha, na mlawiti asiye homofilia ni kada tano za watu, kila kada ikiwa na sifa zake za kitabia.

Bagonza ametumia neno "ushoga" ama kumaanisha "ulawiti" au "uhomofilia." Na neno "uhomofilia" linarejea maana zaidi ya moja, kama tulivyoona hapo juu.

Tofauti hizi zinayo maana kubwa katika ulimwengu wa maadili ambapo uadilifu wa mtu unapimwa kwa kuangalia dhamira ya mtendaji, kitendo alichofanya mtendaji na mazingira ya kitendo cha mtendaji.

Kwa mujibu wa nadharia hii ya kimaadili, homofilia wa kiume asiye chicha, na homofilia wa kiume asiye basha hawana kosa lolote la kimaadili.

Vivyo hivyo, homofilia wa kike asiye msagaji, na homofilia wa kike asiye msagwaji hawana kosa lolote la kimaadili.

Ni vivyo hivyo, kwa heterofilia asiye mlawiti, asiye mbakaji, asiye mzinzi, na heterofilia asiye mwasherati.

Lakini, heterofilia aliye mlawiti, aliye mbakaji, aliye mzinzi, na heterofilia aliye mwasherati ni hatari kwa jamii.

Ni kwa sababu hii, Bagonza anayehimiza mapambano dhidi ya makundi yote mahomofilia anakosea. Napinga kauli zake kwa sababu hii.

Kwa sababu hiyo hiyo, nitampinga mtu yeyote anayetangaza vita dhidi ya maheterofilia bila kutofautisha kati ya heterofilia asiye mlawiti, heterofilia asiye mbakaji, heterofilia asiye mzinzi, heterofilia asiye mwasherati, heterofilia aliye mlawiti, heterofilia aliye mbakaji, heterofilia aliye mzinzi, na heterofilia aliye mwasherati.

Ujenzi wa imani ya jamii yenye utulivu, haki, na amani haufanyiki vizuri kama tusipokuwa makini kuchanganua fikra zetu kwa kina katika kila jambo tunaloliongelea.

Hivyo niliona kuna haja ya kujadili mawazo yake kwa kina ili kusafisha akili za watumiaji wa mitandao ya kijamii.

Maana ya kauli za Bagonza katika muktadha mpana

Kwa upande mmoja, kama Bagonza anatumia neno "ushoga" kumaanisha "uhomofilia," ambayo ni sifa ya kimaumbile, kama ulivyo ufupi na urefu, weupe na weusi, ualibino na siualibino, njia pekee ya kupambana, kama anavyopendekeza, na "ushoga" ni kuwaua "mashoga" hao.

Hivyo, Bagonza hapa anahubiri tabia hatari ya uhomofobia. Sijui kama alitafakari vema juu ya uwezekano huu.

Lakini, pia Bagonza anapswa kutoa sababu nzuri ya kupambana na mahomofilia na kuacha kupambana na mazeruzeru, watu wenye tatizo la colour blindness, na matabaka ya pembezoni kama hayo.

Wote hawa wako hivyo kwa sababu za kimaumbile. Hawakuchagua hali zao.

Bagonza anasema kuwa "imebaki kidogo [mahomofilia] wataunda umoja, watajenga nyumba zao za ibada, ... wataunda chama chao na kuwania uongozi..."

Kwa maoni haya ya Bagonza, hata "mahomofilia" ambao sio machicha wala mabasha hawana haki hizi. Kwa kiwango hiki maoni yake nayapinga.

Urefu, ufupi, sauti nene, sauti nyororo, umashoto, umakengeza, uzeruzeru, colour blindness, na ladhalika, ni sifa asilia walizo nazo watu kadhaa.

Lakini watu hawa hawapotezi haki zao za kibayolojia, kisaikosomatika, kisiasa, kiuchumi na kijamii kwa sababu hiyo pekee.

Kwa upande mwingine, kama Bagonza anatumia neno "ushoga" kumaanisha "ulawiti" kuna maswali ya kitafiti anapaswa kutusaidia kuyajibu.

Tangu tupate uhuru tumefanya sensa mara tano. Hakuna takwimu za serikali zinaonyesha idadi ya mashoga nchini.

KIla mwaka serikali kupitia jeshi la Polisi na Idara ya takwimu (NBS) wanatoa takwimu za uhalifu kupitia kitabu kiitwacho TANZANIA IN FIGURES. Huku pia idadi ya mashoga haitajwi.

Lakini takwimu za mwaka 2021 zinaonyesha kuwa yalikuwepo matukio ya ulawiti 1,296.

Taarifa hiyo haisemi kama ulawiti huu ulifanywa dhidi ya wanaume au kama lifanywa dhidi ya wanawake au kama ulifanywa na mabasha au kama ulifanywa na walawiti wasio mahomofilia.

Lakini bado Bagonza anasema hakubaliani "na wanaodhani ushoga ni tatizo la Ulaya" kwa sababu tayari "hapa kwetu ... hali inatisha."

Bagonza anasema kuwa "imebaki kidogo [walawiti] wataunda umoja, watajenga nyumba zao za ibada, ... wataunda chama chao na kuwania uongozi...Tuamke."

Kwa maoni ya Bagonza, "mahomofilia" ambao ni machicha au mabasha hawana haki hizi kwa sabavu ya uhalifu wanaoufanya. Sawa. Lakini, sheria si zipo. Wanapaswa kuadhibiwa kwa kosa wanalotenda na sio zaidi ya hapo.

Lakini pia, msimamo huu haupaswi kuishia kwa wahalifu wa ulawiti pekee, kama Bagonza anavyoonekana kujielekeza.

Kwa mujibu wa taarifa ya serikali ya kila mwaka, iitwayo Tanzania in Figures, kuna makundi mengi ya uhalifu na yote yanapaswa kumulikwa na serikali.

Kauli za Bagonza zingeeleweka sana kama angesema hivi: "imebaki kidogo [wahalifu] wataunda umoja, watajenga nyumba zao za ibada, ... wataunda chama chao na kuwania uongozi... Tuamke."

Kwa kiwango hiki ningekubaliana na kauli za Bagonza. Hapa kuna wezi, wala rushwa, watu wanaotelekeza watoto mitaani, wafanya biashara ya binadamu, wateka watu, na orodha inaendelea.

Na takwimu halisi za kiserikali kupitia taarifa ya Tanzania in Figures ya kila mwaka, zinaonyesha kuwa baadhi ya watu hawa tayari wana makanisa, wengine ni wamiliki wa vyombo vya habari, wengine ni maaskofu kuanzia makanisa ya kipentekoste hadi Kanisa Katoliki, wengine ni wachungaji, na Bagonza anaujua ukweli huu fika. Hizi hapa:

View attachment 2439942

Lakini bado Bagonza kaamua kuibuka na habari ya "ushoga" isiyo na takwimu za kitafiti.

Mawazo yake yangeleweka na kukubalika zaidi kama angesema kuna "mashoga" wangapi kwenye kaya yake, ukoo wake, kijiji/mtaa wake wa Mwisho wa Lami, kata yake ya Kayanga, wilaya yake ya Karagwe, mkoa wake wa Kagera, na Tanzania kwa ujumla. Hakutoa takwimu zozote katika ngazi hizi.

Hivyo, napenda kumkumbusha kuwa, sifa tata za kimaumbile hazifuti haki za msingi za mahomofilia waadilifu, maalibino waadilifu, mashoto waadilifu, watu wenye makengeza waadilifu, nk.

Sifa hizo ni kama vile haki ya kuishi, kujumuika, kugombea nafasi za kisiasa, kupiga kura, kuabudu, kulindwa na serikali, na haki baki za kibinadamu.

Changamoto ya uhandisi wa maarifa ya kijamii (social constructionism)

Kwa maoni yangu, tamko la Bagonza linaanzia kwenye nadharia ya uhandisi wa maarifa ya kijamii (social constructionism), kama ilivyotumika kubunia "mtu hewa" aitwaye "Father Christmas."

Nadharia za uhandisi wa maarifa ya kijamii (social constructionism), hutengeneza maarifa ya kijamii kutokana na mapatano ya kibinadamu, kama asemavyo Profesa John Rogers Searle (Amerika).

View attachment 2438877
Profesa John Searle, mtalaama wa social constructionism iliyo msingi wa maadili yanayobadilika kwa sababu ya mazingira na iliyo mbadala kwa social realism iliyo msingi wa maadili yasiyobadilika kwa sababu ya mazingira

Katika maandiko yake, John Rogers Searle, kuhusu maarifa yanayotengenezwa kutokana na uhandisi wa kijamii, anataja kanuni kadhaa.

Kanuni moja inahusu "collective intentionality," nyingine inahusu "the assignment of status functions," na kanuni ya tatu inahusu "constitutive rules." Ninataka kuongelea hii kanuni ya tatu, ambayo ni kanuni ya kubuni na kutumia alama.

Kanuni hii inasema hivi: watu wanaweza kukaa wakakubaliana kwamba katika mazingira haya (X), kitu hiki (Y) kitakuwa alama inayowakilisha kitu kile (Z), na mapatano haya yatakoma pale watakapokaa tena na kukubaliana kuyabadilisha. (John R. Searle, Speech acts: An essay in the philosophy of language (Cambridge University Press; 1969, p. 34))

Mfano wake muhimu ni jumuiya ya wanampira waliokubaliana kuwa, katika mazigira ya uwanja wa mpira wa miguu (X), mchezaji akipokea mpira wakati anaelekea kufunga kwenye goli la mpizani wake wakati mbele yake hakuna mchezaji wa timu pinzani (Y), basi hilo ni kosa linaitwa offside (Z).

Kanuni hii inafaa kwenye mpira wa miguu pekee, na sio kwenye mpira wa mikono wala kwenye mpira wa kikapu.

Kwa hiyo, ikitokea siku wachezaji wa michezo yote hii wakajikuta wako pamoja kwa ajili ya mchezo mmoja, itabidi waunde kanuni mpya zinazokubalika kwa wote na kuwafaa wote. Ni vivyo hivyo kwenye maisha ya jamii mseto.

Yaani, kanuni zenye kutokana na mchakato wa mapatano ya kijamii (social constructionism) zinaweza kutumika kwenye jamii ya watu wenye imani moja, lakini sio kwenye jamii za leo ambako kuna utitiri wa kifikra (plural society).

Kwa mfano, wakati wa Papa Yohanne Paulo II, baadhi ya viongozi wa Kanisa Katoliki waliweka msimamo kwamba mahunta sio binadamu.

Mfano wa mwathirika ni Padre Selwyn Gross (jina la zamani la kiume) na baadaye Padre Sally Gross (jina jipya la kike), baada ya kubadilisha jinsia yake.

Hivyo, "Padre Sally Gross" aliyekuwa hunta (intersexual), alivuliwa upadre, kwa kuwa wanawake hawana haki ya kuwa mapadre.

Pia alifutiwa ubatizo kwa hoja kwamba mahunta sio binadamu, na hivyo hawana haki ya kubatizwa.

Mawazo kwamba "mahunta sio binadamu" ni zao la nadharia ya uhandisi wa kijamii (social constructionism) ndani ya Kanisa Katoliki kwa wakati ule wa Papa Yohanne Paul II.

Lakini, leo hii sayansi mamboleo inathibitisha kwamba mahunta wana kromozomu 46 kama watu baki walioko kwenye ukoo wa homosapiensia.

Yaani kumwondoa Padre Sally kwenye tabaka la binadamu ulikuwa ni uamuzi wenye sura ya "category mistake," na ulitokana na matumizi mabaya ya kanuni za uhandisi wa maarifa ya kijamii ndani ya Kanisa Katoliki.

Leo, Kanisa Katoliki sasa limejisahihishana halibebi tena mawazo yale potofu kuhusu hulka ya mahunta. Kanuni za maumbile zimelileta karibu na ukweli asilia.

Kwa sasa bado Kanisa Katoliki linapambana na fundisho lake tata kwamba "a copulating pair is a biological organism"

Fundisho hili ni zao la mradi wa uhandisi wa maarifa ya kijamii (social constructionism) ulioanza miaka ya 1968. Lakini, ni fundisho linalopingana na kanuni za kibayolojia na kifalsafa.

Kifalsafa, neno "organism" lina maana kuu mbili. Yaani "biological organism" kama vile binadamu na kondoo; na "social organism" kama vile familia na timu a mpira.

Ufanano wake ni kwamba, aina zote mbili ni mifumo yenye sehemu nyingi zinazofanya kazi kwa kushirikiana bila kupingana kwa ajili ya kufanikisha lengo la pamoja (organismality).

Tofauti moja kati ya "biological organism" na "social organism" ni kwamba, wakati "kanuni ya uratibu" iko ndani ya mfumo uitwao "biological organism," kanuni hiyo iko nje ya mfumo uitwao "social organism."

Tofauti nyingine kati ya "biological organism" na "social organism" ni kwamba, kiungo cha mwili wa "biological organism" kikikatwa kinakufa, lakini kiungo cha mwili wa "social organism" kikikatwa kinabaki hai, na kinaweza kuunganishwa tena na kuwa sehemu ya "social organism".

Mfano, mchezaji wa mpira wa miguu akipewa kadi nyekundi anaondoka uwanjani na anabaki hai. Akisamehewa anarejea kwenye timu.

Lakini, mkono wako ukikatawa kwa panga hadi kutenganishwa na mwili wako utaoza na baada ya hapo hauwezi kurejeshwa kuwa sehemu ya mwili wako.

Kwa upande mwingine uhai wa "social organism" unaanzia na kukomea kwenye mapatano ya wanajamii husika, kwa maana kwamba, sehemu za kitu kizima zinaanza kuwepo kabla ya kitu hicho kizima kuwepo.

Lakini uhai wa "biological organism" hautokani na mapatano ya viungo vya mwili, maana viungo hivyo huota baada ya kitu kizima kuwepo.

Kwa sababu hizi, sasa ulimwengu wa wanasayansi unakubaliana kwamba, kwa sehemu kubwa "a copulating pair is a social organism," na sio "biological organism."

Huu ni mtazamo unaopingana na mawazo ya baadhi ya makuwadi wa "metafizikia ya umoja wa kimwili," yaani, "metaphysics of bodily union"

Wataalam wa falsafa ya kibayolojia (philosophical biology) hapa wamesaidia sana kuleta mapinduzi ya kifikra yanayotakiwa kuhusiana na swali hili hapa: "what is a biological individual?"

Hitimisho na mapendekezo

Kwa hiyo, napendekeza kwamba, njia pekee ya kujenga imani ya jamii inayokubalika kwa watu wote katika jamii yenye mapokeo mseto sio kutumia kanuni za uhandisi wa maarifa ya kijamii kwa njia ya kura (social constructionism) au kwa kutumia "kanuni za taharuki ya kijamii isiyo na uhalali" (unwarranted moral panic)

Badala yake, tunapaswa kuanzia kwenye kanuni za maadili asilia yanayoweza, na yanayopaswa, kuthibitika kwa njia ya urazini huru miongoni mwa umma mpana (public reason).

Bila kukubaliana na ukweli huu, kazi ya ujenzi wa imani ya jamii yenye imani mseto itakwama, maana mwafaka wa kijamii ni ajenda ya mpito tu.

Mwisho, niseme tu kuwa, katika mradi huu wa kujenga imani ya jamii, wadau wote, yaani wanateolojia, wanasayansi asilia, wanasayansi ya jamii, wanafalsafa, wanasasiolojia, wanahistoria, wanasheria, walei, makasisi, na wanazuoni baki wanayo nafasi.

Lakini, mchango wa kila mmoja una mipaka inayokamilishwa na michango ya wenzake.

Mfano, kwenye Safina ya Nuhu tunaambiwa kuwa Nuhu aliagizwa kuweka kila kiumbe kwa kuzingatia kanuni ya ME na KE.

Lakini, leo hii sayansi inatwambia kuwa kuna viumbe havina mgawanyo huo wa ME na KE. Mfano ni minyoo. Kwa hiyo, mwandishi wa Agano la Kale hakuwa na habari ya ukweli huu wa viumbe wasio na mgawanyo wa jinsia ya ME na KE.

Na hii maana yeke ni kwamba, wanateolojia wanaofanya udadavuzi kwa kuanzia kwenye Biblia wanahitaji kuelimishwa na wanabayolojia katika suala ya asexual reporoduction. Biblia haina mamlaka katika jambo hili.

Vivyo hivyo, Biblia haina mamlaka juu ya fenomena ya "ushoga" katika ujumla wake. Biblia inaongelea "ulawiti," yaani "pedication," basi.

Kwa mfano, haitwambii kama umati wa watu wote wa Sodoma waliotaka kufanya kitendo cha ulawiti walikuwa ni mashoga au hapana.

Na hata kama ingesema hivyo, tusingeamini taarifa kwamba umati wa watu 50 na zaidi walikuwa ni mashoga.

Kwa hiyo wanateolojia wanaoongozwa na Biblia hawana mamlaka ya kutuhubiria juu ya topiki ya "ushoga" kama ilivyojadiliwa katika uzi huu.

Ukweli ni kwamba, kila wanapojaribu wanapotosha jamii. Mfano, ibara za 2357 na 2358 katika Katekisimu ya Kanisa Katoliki ya mwaka 1992 zinasema hivi kuhusu ushoga (homosexuality):

2357 Homosexuality refers to relations between men or between women who experience an exclusive or predominant sexual attraction toward persons of the same sex. It has taken a great variety of forms through the centuries and in different cultures. Its psychological genesis remains largely unexplained.
Basing itself on Sacred Scripture, which presents homosexual acts as acts of grave depravity, tradition has always declared that "homosexual acts are intrinsically disordered"... (emphasisi by underlining added)
2358 The number of men and women who have deep-seated homosexual tendencies is not negligible. This (is an ) inclination... (emphasisi by underlining added).

Katika nukuu hii, kuna makundi matatu ya maneno yafuatayo yenye kuzalisha utata wa kimantiki: "Homosexuality refers to relations," "homosexual acts," "homosexual tendencies," na "this (is an ) inclination."

Katika vishazi hivi vinne, vishazi vitatu vya mwisho vinazalisha hitimisho kwamba, "homosexuality refers to a condition."

Lakini, Katekisimu hiyo hiyo inasema kuwa "homosexuality refers to relations." Huu ni mkanganyiko wa kimantiki ndani ya Katekisimu.

Kwa sababu hii, ni wazi kuwa Kamati ya Kipapa iliyoandika Katekisimu hii, chini ya Kiranja Mkuu wa Imani wa wakati huo, Kardinali Ratzinger, hawakuwa na weledi kamilifu juu ya mada ya uhomofilia, uheterofilia, na ulawiti.

Ni kama hawakujua tofauti kati ya "hali ya ushoga" yaani "homosexual condition," "tabia ya ulawiti wa kishoga" yaani "homosexual pedication," na "tabia ya ulawiti usio wa kishoga" yaani "non-homosexual pedication,"

Tofauti hizi ndio msingi wa kanuni za kisheria zinazoangalia kitendo na dhamira ya mtendaji, yaani "actus reus (the physical element)" na "mensi rea (the mental element)."

Hii ni tofauti kati ya "the intention to commit the unlawful act " dhidi ya "the unlawful act committed ."

Kwa maana hii, "homosexuality condition" haiwezi kuwa "dhambi (sin)" wala "jinai (crime)." Lakini, "homosexual pedication" inaweza kuwa "dhambi (sin)," "jinai (crime)," au yote mawili.

Katika hili, wanasayansi, wanasheria na wanamaadili wanapaswa kushirikiana katika kujenga imani ya jamii.

Basi, kwa ujumla, sote tunakamilishana kimaarifa, na hivyo kuna haja ya kuunganisha nguvu katika kufanikisha mradi wa kujenga imani ya jamii yenye utulivu, haki na amani kkwa kuanzia kwenye misingi ya uhalisia asilia (social realism) badala ya kukimbilia kwenye unadisi wa maarifa ya kijamii kwa njia ya kura (social constructionism).

Tujenge hoja bila mihemuko wala taharuki.
Mleta hoja kusema ukweli ebu mtake radhi Mh.Lissu na Askofu Bagonza. Yaani umechukua vidole vya mkono wa mlinzi na msaidizi wa Mh.Lissu na kusema ni mkona wa Mh.Askofu Bagonza. Ili ni kosa kubwa sana,unataka kusema Askofu Bagonza ana mikono mitatu? Moderators ebu mkue makini na watu kama huyu
 
Ndugu, huwa sifanyi ujinga huo. Picha hiyo ipo kwenye ukurasa wa wanachadema wenyewe. Tazama hapa: Chadema in Blood. Ilibandikwa hapo 15 Desemba 2020. Naiposti tena hapa chini bila labels zangu, lakini kwa kuonyesha context ya mtandaoni ...

1676449403230.png

Picha zingine zilizo kwenye ukurasa wao hizi hapa:

1676449521447.png

Na hii....
1676449591127.png

Na hii....
1676452442886.png

Na hii....
1676452690107.png

Kwa ajili ya kukuondolea shaka kuhusu anatomia ya vidole vya Lissu, picha hii hapa inamaliza utata (iangalie vizuri):

1.jpg

Hii nayo nimeichakachua?
 
Back
Top Bottom