Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 15,835
- 23,776
a Askofu Bagonza
AKILI na IMANI
Hivi kipi kinaanza? Kipi kinawezesha kingine? Imani ndiyo inakuongoza kuwa na akili au akili inakuongoza kuwa na imani na kuitegemea?
Wanaopuuza umuhimu wa kutumia akili, wawaulize wazazi ambao kwa bahati mbaya wana watoto au jamaa waliopungukiwa na akili, kwa kuzaliwa au kupata tatizo hilo ukubwani. Zawadi kubwa, ya pekee na ya thamani aliyotupa Mungu ni akili. Tunaitumia kutambua na kufanya maamuzi. Hata imani tunayoienzi na kumwamini muumba wetu, tunawezeshwa na akili aliyotupa muumba huyo huyo.
Ndiyo maana pamoja na kwamba Mungu yupo:
1. Tunajenga Nyumba na kulala ndani yake, hatulali nje ili Mungu atulinde.
2. Tunajenga uzio mkubwa kuzunguka Nyumba, hatuaiachi nyumba ili Mungu atulinde.
3. Tunafuga Mbwa wakali, licha ya kuwa na Uzio.
4. Tunaajiri walinzi wenye silaha, kana kwamba uzio na mbwa havitoshi.
5. Tunaweka na CCTV kamera licha ya kuwa tuna walinzi, uzio na mbwa wakali.
6. Tunanunua na bima kubwa kuonyesha kuwa wizi bado upo licha ya kuwa tuna yote hayo.
7. Usiku tunaamka mara tatu-tatu kuona kama walinzi wapo. Tunaajiri walinzi na wao wanatuajiri kuwachunga usiku.
Pamoja na yote hayo, Mungu aweza kutuchukua kutoka katikati ya ulinzi wote huo. Anatupa akili tuzitumie kujilinda, lakini anabaki na uwezo wa mwisho juu ya maisha yetu.
Hatuwezi kuacha kutumia akili eti kwa sababu yeye yupo. Na hatuwezi kutegemea akili tu eti kwa sababu akili katupa yeye. Imani na akili vyote ni mali ya Mungu, yeye katukabidhi tuvitumie.
Hatuwezi kuacha kuvaa Mask/Barakoa eti Mungu yupo, kwani huko VATICAN na MECCA dini zilipoanzia Mungu hayupo, yupo Tanzania pekee? UCHUMI vs MAISHA YA WATU! [MSISITIZO NI WANGU]
TUSIHUKUMIANE na TUSILAUMIANE.