Askofu Bagonza: ATCL imekosa aibu, basi iwe na huruma

Askofu Bagonza: ATCL imekosa aibu, basi iwe na huruma

Wamejitetea kindezi
Msemaji wa ATCL ndugu Josephat Mwingira amesema pamekuwepo na mabadiliko ya mara kwa mara ya ratiba za ndege zao takribani wiki mbili sasa kwa sababu ndege nyingi zilikuwa kwenye matengenezo makubwa.

Mwingira amesema nyingi ya ndege zao zilinunuliwa kwa wakati mmoja ndio maana hata matengenezo yake hufanyika pamoja na kamwe ATCL haiwezi kurusha ndege yenye hitilafu.

Mwingira amewataka mawakala wa kuuza tiketi kuweka namba zao za simu na kuchukua namba za wateja ili wawe wanapewa taarifa ya mapema pindi yanapotokea matatizo.

Source: Star tv habari!
Hata kama ndege zote zilinunuliwa kwa wakati mmoja , the fact ni kuwa hazifanyi safari ya aina moja , maana yake ni kuwa zina milage tofauti tofauti, inawezekana ndege ya mwisho ikadai matengenezo mapema kuliko ile ya mwanzo.
 
Kwanini waliifutia leseni fastjet ndege yetu wanyonge?
Hakuna mechi isiyo na watazamaji.
Leo ATCL imewaomba radhi wasafiri kwa usumbufu walioupata! Kuna siku waliwalaumu wasafiri kwa kutoacha namba zao za simu ili wajulishwe endapo ndege itakuwa na mafua makali.
 
Kumbe tunazihitaji hizi ndege
Zipo tayari, na zimenunuliwa kwa pesa za walipa kodi hivyo ni jambo la kawaida tu kuhoji chochote juu ya shirika hili la Umma, ama sivyo lisingekuwepo hakuna ambaye angehoji kulihusu.
 
ATCL Imekosa Aibu basi Iwe na Huruma

Ndani ya miezi miwili nikisafiri na ndege za ATCL nimeona haya:

1. Nilishindwa kuhudhuria mazishi ya ndugu na kukaa airport siku nzima

2. Nilishinda uwanjani Dar na kuondoka usiku wa manane siku ya pili.

3. Nilikosa connection ya ndege Dar baada ya ndege kutoka Mwanza kuchelewa kufika

4.Leo nimekesha uwanjani Mwanza (tangu saa Moja jioni Hadi saa 9 alfajiri).

Nashauri kirefu cha ATC kiwe:
"Any Time Cancellation" (ATC).

Tunatia aibu mbele ya wageni.

Pia soma: ATCL yatoa ufafanuzi kuvurugika kwa ratiba za ndege zake, yasema nyingi zilikuwa kwenye matengenezo makubwa!
View attachment 1899014
Any Time Cancellation & Liabilities (ATCL) [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Bongo bado sana tuna watu ambao hawastahili kuwa hata wajumbe wa shina mtaani leo hii wanakabidhiwa Ikulu na kuongeza madudu kila kukicha
Any Time Cancellation & Liabilities (ATCL) [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Shirika linaendeshwa kienyeji, no professionalism at all.

Sababu kuu ya cancellations zisizo na kichwa wala miguu, ni kwamba, fleet zilizopo zipo busy na kuwazungusha watawala badala ya kuwahudumia wananchi.

Rais, Makamo wake, Rais wa Zanzibar, Waziri Mkuu na Makamo wa Rais Zanzibar watumie ndege za serikali, ndege za ATCL za abiria zitumike kubebea abiria.

Viongozi Kama wanapenda sana ndege, nawashauri wafuge kuku, bata, kanga na hata bundi iwapo wataweza
Kumbe
 
Wewe unadhani kwa watu wote duniani si waaminifu kama wewe. Kampuni ya ndege kama Boeing au Airbus haiwezi kufanya biashara za kipuuzi hivyo, mzee. Mimi nilitembelea Boeing Seattle nikaikuta ATCL iko kwenye production line pamoja na ndege nyingine za United Airlines. Ujenzi wa ndege ni project ya muda mrefus, siyo kama unakwenda sokoni na kukuta iko yadi na kujichagulia tu. Katika ndege hizi mpya za ATCL kuna ushahidi wa kutosha kuwa zilianza kujengwa baada ya oda, siyo kuwa zilichukuliwa kwenye yadi na kupakwa rangi kama unavyojiaminisha.

Kama watumiaji wenyewe ni wa aina yako si ajabu ni wewe uliyharibu kutasa hivho kusudi utoe lawama. Watanzania tulivunja viti uwanja wa Taifa hatushindwi kuvuja vitasa hasa kwa vile kuna watu wanachukia ndege hizo; walitaka pesa iliyotumika kuzinunua igawiwe mitaani kama njugu.
Pole mheshimiwa. Uliikuta kwenye production au kwenye ukarabati. Kumbuka ndege zimetoka Canada siyo US. Wewe ulipataje kibali kuingia huko kama unataka uonekane unaishi marekani. Sisi wasafishaji wa ndege ambao hatujawahi ruka nayo bali kusafisha ndo tunaongea.
 
Ukitafuta hapa JF miaka kadhaa hata kabla ya ndege Boeing ya kwanza kuletwa nilipost nilivyoikuta katika hatua za mwisho za matengezo nilipokwenda field trip na wanafunzi wangu kutembelea kiwa cha Boeing. Ndege za Boeing zinatoka Seattle; hizo za Bombardier na Airbus ndizo zilziotoka Canada. Halafu kiwanda cha ndege huwa kinajenga ndege kuanzia hatua za mwanzo, huwa hakifanyi ukarabati. Ndege ikishajengwa na kukamilika, haiwezi kurudi tena kwenye proudction line kwa sababu ya nafasi.
 
Wamejitetea kindezi
Msemaji wa ATCL ndugu Josephat Mwingira amesema pamekuwepo na mabadiliko ya mara kwa mara ya ratiba za ndege zao takribani wiki mbili sasa kwa sababu ndege nyingi zilikuwa kwenye matengenezo makubwa.

Mwingira amesema nyingi ya ndege zao zilinunuliwa kwa wakati mmoja ndio maana hata matengenezo yake hufanyika pamoja na kamwe ATCL haiwezi kurusha ndege yenye hitilafu.

Mwingira amewataka mawakala wa kuuza tiketi kuweka namba zao za simu na kuchukua namba za wateja ili wawe wanapewa taarifa ya mapema pindi yanapotokea matatizo.

Source: Star tv habari!

Mwingira muongo tu! Tunakumbuka kusheherekea ujio wa hizi ndege pale JNIA. Hakuna kipindi tulipokea ndege zaidi ya moja na hakuna ndege ilifika ndani ya miezi mitatu ya nyingine!!

Watanzania tunachukuliwa na watawala kama watu wasahaulifu na ndio maana tunasikia habari za “nitajenga barabara, shule, zahanati. Nitaleta maji na kuongeza ajira” kutoka kwa watu walewale kufikia hata miaka 15-20!! Ni kwa sababu kila kitu kikitajwa - kinasikika kama kipya.

Ukweli ni kuwa idadi ya domestic sorties ninkubwa kuliko mahitaji na hivo hakuna mapato ya kutosha. Hizi cancellations ni kujaribu kuungalisha abiria wa sorties tofauti ili kuendesha ndege chache zaidi!! Kwa ujumla swala la ndege liliamliwa kisiasa zaidi kuliko kiuchumi na kiuendeshaji!!
 
Shirika linaendeshwa kienyeji, no professionalism at all.

Sababu kuu ya cancellations zisizo na kichwa wala miguu, ni kwamba, fleet zilizopo zipo busy na kuwazungusha watawala badala ya kuwahudumia wananchi.

Rais, Makamo wake, Rais wa Zanzibar, Waziri Mkuu na Makamo wa Rais Zanzibar watumie ndege za serikali, ndege za ATCL za abiria zitumike kubebea abiria.

Viongozi Kama wanapenda sana ndege, nawashauri wafuge kuku, bata, kanga na hata bundi iwapo wataweza
"Viongozi Kama wanapenda sana ndege, nawashauri wafuge kuku, bata, kanga na hata bundi iwapo wataweza"

Upo kwenye ubora wako mpwa. Hahahaha
 
Yaani ni vituko. Hizi ndege si ni mpya? Sasa hayo matengenezo makubwa kipindi hiki kifupi tangu kununuliwa? Soon hili shirika litakufa. Sitashangaa. Wanaliendesha kwa big loss. eventually serikali itashindwa kuwa-bail out. Labda wazidishe ongezeko zaidi kwenye tozo za miamala ili kulibeba shirika hili pia. Otherwise, I see the death of ATCL very soon
Tena life mapema turudi tulikozoea. Watz hatupendi kumiliki vitu vizuri tuna kasumba ya kujitweza kujiona dhaifu na duni. Tuko proud kuonesha jinsi wengine walivofanikiwa zile cheki KQ cheki EthiopianAirways.. Hata wish ya opportunistic politicians (ccm na upinzani) ni kuona Atc inakufa (wanajua wanavofaidika likiwa mfu) ndio maana vita ya kupinga atcl isifufuliwe ilikuwa kubwa kweli kwa kila sura na mbinu. R. I. P JPM
 
ATCL Imekosa Aibu basi Iwe na Huruma

Ndani ya miezi miwili nikisafiri na ndege za ATCL nimeona haya:

1. Nilishindwa kuhudhuria mazishi ya ndugu na kukaa airport siku nzima

2. Nilishinda uwanjani Dar na kuondoka usiku wa manane siku ya pili.

3. Nilikosa connection ya ndege Dar baada ya ndege kutoka Mwanza kuchelewa kufika

4.Leo nimekesha uwanjani Mwanza (tangu saa Moja jioni Hadi saa 9 alfajiri).

Nashauri kirefu cha ATC kiwe:
"Any Time Cancellation" (ATC).

Tunatia aibu mbele ya wageni.

Pia soma: ATCL yatoa ufafanuzi kuvurugika kwa ratiba za ndege zake, yasema nyingi zilikuwa kwenye matengenezo makubwa!
View attachment 1899014
Bishop tulia atcl ife wish yenu haikuwa kuona Tz inasimama imara kwenye nyanja hii na zinginezo kiuchumi. Mlimpinga JPM kwa kila namna mlivoweza. Hii ndo inaitwa back to normalcy unalalamika nini wakati haya ndo yalikuwa maisha kabla ya 2015
 
Shirika linaendeshwa kienyeji, no professionalism at all.

Sababu kuu ya cancellations zisizo na kichwa wala miguu, ni kwamba, fleet zilizopo zipo busy na kuwazungusha watawala badala ya kuwahudumia wananchi.

Rais, Makamo wake, Rais wa Zanzibar, Waziri Mkuu na Makamo wa Rais Zanzibar watumie ndege za serikali, ndege za ATCL za abiria zitumike kubebea abiria.

Viongozi Kama wanapenda sana ndege, nawashauri wafuge kuku, bata, kanga na hata bundi iwapo wataweza
Hii ndo shida kubwa.. habari ya eti ndege zilikuwa zinafanyiwa matengenezo makubwa ni geresha tu!!
 
Ni mwenye ufinyu wa akili tu ndiye anaweza kuandika upuuzi kama huu. Kweli Tanzania upumbavu UMETAMALAKI labda kuliko nchi yoyote ile duniani.
Bishop tulia atcl ife wish yenu haikuwa kuona Tz inasimama imara kwenye nyanja hii na zinginezo kiuchumi. Mlimpinga JPM kwa kila namna mlivoweza. Hii ndo inaitwa back to normalcy unalalamika nini wakati haya ndo yalikuwa maisha kabla ya 2015
 
Kumbe tunazihitaji hizi ndege
Ni zetu, japo zimenunuliwa bila mpangilio, lakini pesa ni yetu. Hatutaki tuzidi kupata hasara juu ya hasara. Shida wengine mlifikiri ile hela Magu katoa mfukoni.
 
Back
Top Bottom