PreGE2025 Askofu Bagonza awajia juu Mwijaku, Makalla asema 'Mnaiunga mkono No Reform, No Election bila kujua'

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
Na Askofu Kalikawe Lwakalinda Bagonza (PhD)

JUZI KUFURU; Leo HIJJA au Utalii…halafu JINAI.

Wanyambo na Wajaluo wana msemo usemao, “Give me a Break”. Wakisema hivyo wanamaanisha vituko vyako vimezidi, wape muda wapumzike kidogo.

1. Akatoka mmoja juzi. Kamlinganisha rais wetu na Mitume watakatifu wa dini mbili kuu. Tusio na kazi tukakemea na kushauri mtu ANUNE. Ile ilikuwa Kufuru. Amenuna. Si lazima aite vyombo vya habari kuonyesha mnuno wake.

2. Sasa kaja mwingine. Kapiga picha ya video akiwa Hijja, eneo takatifu la KAABA. Kafanya dua zake. Kamwombea rais wetu. Vema. Lakini kamwomba Mungu awaangamize wote wenye nia njema na wapinzani wanaosema No Reform, No Election. Hawa ni wapiga kura wa rais wetu. Mwombaji anataka waangamie. Hii ni ibada au utalii?

3. Leo kaibuka rafiki yangu Amos (Jina la Nabii mmoja mkali sana katika Biblia). Yeye ni Mwenezi wa chama Dume. Anadai chama Jike kinapanga kununua Ebola na M-Pox ili kitumie magonjwa hayo hatari kuzuia uchaguzi. Duh! Kama si Dume angeisaidia polisi. Waenezi wa vyama vingine msimuige, mtapotea au kupotezwa.

5. Nirudie kutoa shule.

a) Mungu wetu hana roho mbaya kama yetu. Ashinikizwi, haongwi na hana chama wala chawa. Anapenda HAKI na KWELI. Tuache kufuru.

b) Hata tusio Waislam tunaiheshimu sana KAABA. Hatuijui sawasawa lakini tunaogopa tukiona mizaha, kamera, na vinyongo vinapelekwa pale.

C) Hakuna mgombea rais Tanzania anayeweza kushinda uchaguzi kwa kutegemea kura za chama chake tu; dini yake tu, kabila lake tu wala jinsia yake tu. Wanasiasa jengeni ushawishi siyo mizengwe.

d) Malori ya polisi (Karandinga) hubeba watuhumiwa wa uhalifu. Tukianza kutumia magari ya polisi kusomba wapiga kura, kinachofuata ni kutumia bunduki za polisi kupigia kura na mwisho kutumia magari hayo kusombea kura. Acheni. Mnaiunga mkono No Reform, No Election bila kujua.

e) Mimi bado naamini kwa dhati, chama dume kina uwezo wa kushinda bila mizengwe wala kuleta taharuki katika jamii. Kinaweza kushinda hata kukubali maboresho ya sheria za uchaguzi zinazodaiwa na vyama jike. Kinahitaji kufuta kauli za makada wake huko nyuma na wa sasa zinazoonyesha hofu ya chama na kupandikiza hofu hiyo kwa wananchi.

e) Mizengwe ya kidola na hila binafsi za makada vimesababisha ushawishi wa kisiasa kuhamia kwa wanasiasa wenye misimamo mikali. Iwe ndani ya chama dume au vyama jike, wale wenye misimamo mikali ndio wanasikilizwa na kuheshimiwa. Tulipoteza fursa huko nyuma na sasa tuko njia panda. Wajinga wanadhani bunduki na mabomu yatasaidia. Kwa muono wangu, ubabe utaongeza kukubalika kwa wenye misimamo mikali. RUDINI MEZANI BILA HILA.
 
Bagonza ameanza kuchanganyikiwa mwinjaku ni sawa na mdude nyangali tu wote ni watu wa kubwabwaja tu!
 
Mizengwe ya kidola na hila binafsi za makada vimesababisha ushawishi wa kisiasa kuhamia kwa wanasiasa wenye misimamo mikali. Iwe ndani ya chama dume au vyama jike, wale wenye misimamo mikali ndio wanasikilizwa na kuheshimiwa. Tulipoteza fursa huko nyuma na sasa tuko njia panda. Wajinga wanadhani bunduki na mabomu yatasaidia. Kwa muono wangu, ubabe utaongeza kukubalika kwa wenye misimamo mikali. RUDINI MEZANI BILA HILA.
Mwisho wa kunukuu
 
Na Askofu Kalikawe Lwakalinda Bagonza (PhD)

JUZI KUFURU; Leo HIJJA au Utalii…halafu JINAI.

Wanyambo na Wajaluo wana msemo usemao, “Give me a Break”. Wakisema hivyo wanamaanisha vituko vyako vimezidi, wape muda wapumzike kidogo.

1. Akatoka mmoja juzi. Kamlinganisha rais wetu na Mitume watakatifu wa dini mbili kuu. Tusio na kazi tukakemea na kushauri mtu ANUNE. Ile ilikuwa Kufuru. Amenuna. Si lazima aite vyombo vya habari kuonyesha mnuno wake.

2. Sasa kaja mwingine. Kapiga picha ya video akiwa Hijja, eneo takatifu la KAABA. Kafanya dua zake. Kamwombea rais wetu. Vema. Lakini kamwomba Mungu awaangamize wote wenye nia njema na wapinzani wanaosema No Reform, No Election. Hawa ni wapiga kura wa rais wetu. Mwombaji anataka waangamie. Hii ni ibada au utalii?

3. Leo kaibuka rafiki yangu Amos (Jina la Nabii mmoja mkali sana katika Biblia). Yeye ni Mwenezi wa chama Dume. Anadai chama Jike kinapanga kununua Ebola na M-Pox ili kitumie magonjwa hayo hatari kuzuia uchaguzi. Duh! Kama si Dume angeisaidia polisi. Waenezi wa vyama vingine msimuige, mtapotea au kupotezwa.

5. Nirudie kutoa shule.

a) Mungu wetu hana roho mbaya kama yetu. Ashinikizwi, haongwi na hana chama wala chawa. Anapenda HAKI na KWELI. Tuache kufuru.

b) Hata tusio Waislam tunaiheshimu sana KAABA. Hatuijui sawasawa lakini tunaogopa tukiona mizaha, kamera, na vinyongo vinapelekwa pale.

C) Hakuna mgombea rais Tanzania anayeweza kushinda uchaguzi kwa kutegemea kura za chama chake tu; dini yake tu, kabila lake tu wala jinsia yake tu. Wanasiasa jengeni ushawishi siyo mizengwe.

d) Malori ya polisi (Karandinga) hubeba watuhumiwa wa uhalifu. Tukianza kutumia magari ya polisi kusomba wapiga kura, kinachofuata ni kutumia bunduki za polisi kupigia kura na mwisho kutumia magari hayo kusombea kura. Acheni. Mnaiunga mkono No Reform, No Election bila kujua.

e) Mimi bado naamini kwa dhati, chama dume kina uwezo wa kushinda bila mizengwe wala kuleta taharuki katika jamii. Kinaweza kushinda hata kukubali maboresho ya sheria za uchaguzi zinazodaiwa na vyama jike. Kinahitaji kufuta kauli za makada wake huko nyuma na wa sasa zinazoonyesha hofu ya chama na kupandikiza hofu hiyo kwa wananchi.

e) Mizengwe ya kidola na hila binafsi za makada vimesababisha ushawishi wa kisiasa kuhamia kwa wanasiasa wenye misimamo mikali. Iwe ndani ya chama dume au vyama jike, wale wenye misimamo mikali ndio wanasikilizwa na kuheshimiwa. Tulipoteza fursa huko nyuma na sasa tuko njia panda. Wajinga wanadhani bunduki na mabomu yatasaidia. Kwa muono wangu, ubabe utaongeza kukubalika kwa wenye misimamo mikali. RUDINI MEZANI BILA HILA.
Hakuna mgombea rais Tanzania anayeweza kushinda uchaguzi kwa kutegemea kura za chama chake tu; dini yake tu, kabila lake tu wala jinsia yake tu. Wanasiasa jengeni ushawishi siyo mizengwe.
FB_IMG_1742734314297.jpg
 
Nchi pekee duniani wapuuzi wengi na ndio wako na wanasiasa kuomgoza nchi masikini kifikra na kuiba pamoja wanasiasa.....ewwe jeshi nakulilia.....uadilifu wako.....polisi wamesha kengeuka....nchi haina mwenyewe?
 
Back
Top Bottom