implicit memory
JF-Expert Member
- Nov 14, 2024
- 2,109
- 2,157
Uongozi wa Saudi Arabia ungefanya jambo hapo,usikae kimya,upande mwingine ameifanyia dini mzaha
Hivi huyu anayejiita Askofu Bagonza hana kazi ya Uaskofu? Au kazi ya Uaskofu ni ndogo na nyepesi sana? Hivi ikitokea na wanasiasa wakianza kupatimba huko makanisani, kitaeleweka kweli?Na Askofu Kalikawe Lwakalinda Bagonza (PhD)
JUZI KUFURU; Leo HIJJA au Utalii…halafu JINAI.
Wanyambo na Wajaluo wana msemo usemao, “Give me a Break”. Wakisema hivyo wanamaanisha vituko vyako vimezidi, wape muda wapumzike kidogo.
1. Akatoka mmoja juzi. Kamlinganisha rais wetu na Mitume watakatifu wa dini mbili kuu. Tusio na kazi tukakemea na kushauri mtu ANUNE. Ile ilikuwa Kufuru. Amenuna. Si lazima aite vyombo vya habari kuonyesha mnuno wake.
2. Sasa kaja mwingine. Kapiga picha ya video akiwa Hijja, eneo takatifu la KAABA. Kafanya dua zake. Kamwombea rais wetu. Vema. Lakini kamwomba Mungu awaangamize wote wenye nia njema na wapinzani wanaosema No Reform, No Election. Hawa ni wapiga kura wa rais wetu. Mwombaji anataka waangamie. Hii ni ibada au utalii?
3. Leo kaibuka rafiki yangu Amos (Jina la Nabii mmoja mkali sana katika Biblia). Yeye ni Mwenezi wa chama Dume. Anadai chama Jike kinapanga kununua Ebola na M-Pox ili kitumie magonjwa hayo hatari kuzuia uchaguzi. Duh! Kama si Dume angeisaidia polisi. Waenezi wa vyama vingine msimuige, mtapotea au kupotezwa.
5. Nirudie kutoa shule.
a) Mungu wetu hana roho mbaya kama yetu. Ashinikizwi, haongwi na hana chama wala chawa. Anapenda HAKI na KWELI. Tuache kufuru.
b) Hata tusio Waislam tunaiheshimu sana KAABA. Hatuijui sawasawa lakini tunaogopa tukiona mizaha, kamera, na vinyongo vinapelekwa pale.
C) Hakuna mgombea rais Tanzania anayeweza kushinda uchaguzi kwa kutegemea kura za chama chake tu; dini yake tu, kabila lake tu wala jinsia yake tu. Wanasiasa jengeni ushawishi siyo mizengwe.
d) Malori ya polisi (Karandinga) hubeba watuhumiwa wa uhalifu. Tukianza kutumia magari ya polisi kusomba wapiga kura, kinachofuata ni kutumia bunduki za polisi kupigia kura na mwisho kutumia magari hayo kusombea kura. Acheni. Mnaiunga mkono No Reform, No Election bila kujua.
e) Mimi bado naamini kwa dhati, chama dume kina uwezo wa kushinda bila mizengwe wala kuleta taharuki katika jamii. Kinaweza kushinda hata kukubali maboresho ya sheria za uchaguzi zinazodaiwa na vyama jike. Kinahitaji kufuta kauli za makada wake huko nyuma na wa sasa zinazoonyesha hofu ya chama na kupandikiza hofu hiyo kwa wananchi.
e) Mizengwe ya kidola na hila binafsi za makada vimesababisha ushawishi wa kisiasa kuhamia kwa wanasiasa wenye misimamo mikali. Iwe ndani ya chama dume au vyama jike, wale wenye misimamo mikali ndio wanasikilizwa na kuheshimiwa. Tulipoteza fursa huko nyuma na sasa tuko njia panda. Wajinga wanadhani bunduki na mabomu yatasaidia. Kwa muono wangu, ubabe utaongeza kukubalika kwa wenye misimamo mikali. RUDINI MEZANI BILA HILA.
Kila asemaye ukweli mbele ya waovu na wasio na akili huwa amechanganyikiwa,mambo yakiharibika waovu hupata Akili mwishoni kwa sababu wao ni slow learners.Bagonza ameanza kuchanganyikiwa mwinjaku ni sawa na mdude nyangali tu wote ni watu wa kubwabwaja tu!
Ivi skuiz pale KAABA naona Kuna watu wanapanajisi sana cjajua ni Kwa sababu ya teknolojia au vipiNchi hii wauza unga wapo salama sn sababu wanaipigia debe CCM
Bagonza mwenyewe anasemaje nafikiri amekataa mawakili kitambo!Kila asemaye ukweli mbele ya waovu na wasio na akili huwa amechanganyikiwa,mambo yakiharibika waovu hupata Akili mwishoni kwa sababu wao ni slow learners.
Ndiyo ujue umejaa usheteni tupuIvi skuiz pale KAABA naona Kuna watu wanapanajisi sana cjajua ni Kwa sababu ya teknolojia au vipi
Umemuacha wapi na Makala?Bagonza ameanza kuchanganyikiwa mwinjaku ni sawa na mdude nyangali tu wote ni watu wa kubwabwaja tu!
Bagonza nae ni mtu wa udaku mwinjaku huwa siangalii nini anafanya!
kumbe ndio wewe kiziwi , Sawa oktoba inakujaHakuna mgombea rais Tanzania anayeweza kushinda uchaguzi kwa kutegemea kura za chama chake tu; dini yake tu, kabila lake tu wala jinsia yake tu. Wanasiasa jengeni ushawishi siyo mizengwe.View attachment 3280862
Zile dawa zinafunga masikio au ile raha inawasababisha wasisikie kitu kingineWauza unga hawawezi kusikia
YapZile dawa zinafunga masikio au ile raha inawasababisha wasisikie kitu kingine
Hao wala sembe hawawezi kuelewaMaandiko ya Askofu Bagonza yanalenga watu wenye akili timamu, siyo mtu kama wewe!!
Bagonza ameanza kuchanganyikiwa mwinjaku ni sawa na mdude nyangali tu wote ni watu wa kubwabwaja tu!
Tofauti yao ni nini wote ni waropokaji!Pamoha na kumdharau, Mdude ana akili sana. Huwezi kumlinganisha na Mwijaku. Ni kama kulinganisha maji na mafuta
Pole sana mkuu!Maandiko ya Askofu Bagonza yanalenga watu wenye akili timamu, siyo mtu kama wewe!!
Wacha nikupe namba ya simu uongee nae maana si kwa kuwanyoosha!Umemuacha wapi na Makala?
Bagonza yuko sawa,lbd ww uchanganyikiwe mwijaku na mdude kuwa sawa Kwa kubwabwaja bila kuona tofauti ya wanayoongea ni tatizo jingine.Bagonza ameanza kuchanganyikiwa mwinjaku ni sawa na mdude nyangali tu wote ni watu wa kubwabwaja tu!
mtajuwa wenyewe wapenda udaku!Bagonza yuko sawa,lbd ww uchanganyikiwe mwijaku na mdude kuwa sawa Kwa kubwabwaja bila kuona tofauti ya wanayoongea ni tatizo jingine.
kipara tuheshimianemtajuwa wenyewe wapenda udaku!