Ameandika Askofu Bagonza
Kuna mambo ukiyakalia kimya yanaisha yenyewe kwa sababu hayakusaidii wala hayakuumizi.
Kuna mambo ukiyakalia kimya hayaondoki yenyewe na ni ya hatari.
Hili la Askari wa Kukodi (Mamluki au Mercenaries), LISIKALIWE kimya. Kama ni kweli wapo, WAONDOLEWE mara moja kimya kimya. Kwa nini?
1. Wakati wa vita ya Uganda, Iddi Amin alileta Askari wa Libya kumsaidia. Tukawateka. Hatukuwaua. Baada ya vita tuliwarudisha Libya kutokea DSM. Ilikuwa aibu kubwa kwa Libya na Uganda. Tulionekana waungwana. Kutumia mamluki kwa migogoro yetu ya ndani kunafuta heshima yetu ya wakati ule.
2. Ni kejeli na matusi kwa vyombo vyetu vya ulinzi. Vyombo vyetu ni fahari yetu na ni nyeti kama makalio yetu. Eneo nyeti si za kuguswaguswa na wageni. Vyaweza kuwa kimya kwa heshima ya wakuu lakini vinajisikia kuaibika.
3. Afisa wetu mmoja mkubwa wa Polisi, alikamatwa na Idd Amin hapa mpakani Mtukula. Alikuwa chotara, marehemu Hans Pope kutoka Iringa. Idd Amin akadai Tanzania inatumia mamluki. Akamuua na kumhifadhi kwenye jokofu kama ushahidi kwa miaka mingi. Umamluki una gharama chungu. Tusipuuze.
4. Pamoja na kuwa katika giza la mawasiliano, lakini malalamiko yanayosikika yana mashiko kwa sababu watuhumiwa wameacha “DNA” katika shughuli zao. Watu wetu wako tayari kuuawa na watanzania wenzao. Tusipuuze, tutapuuzwa.
5. Tumekuwa wakali na makini katika vyombo vyetu kutoingiza watu wenye uraia tata. Tunaanzaje kuleta majeshi ya kigeni kuchangamana na majeshi yetu? Miaka ya karibuni zilisikika habari za Afisa wa jeshi kutoroka na kuhamia nchi ya kigeni akiwa na siri zetu. Hawa kama wapo wataondoka na siri ngapi? Natamani isiwe kweli!
6. Tumewahi kuwa na wataalam wa vyombo vyetu kwa ajili ya mafunzo katika vyote tangu tupate uhuru. Lakini haikuwa siri na yalikuwa ni mafunzo. Kutumia mamluki katika mambo ya kisiasa ni hatari kwa sababu inachochea tuanze kutazamana maeneo tutokapo.
Si kila suala la kisiasa ni la kiusalama. Naelewa kuna bangi ya siasa imemwagwa kwenye vyombo vyetu lakini isitufikishe kwenye mamluki.
Kama hamuelewani huko ndani jengeni madaraja, bomoeni kuta, au waiteni makamisaa wazalendo wawakumbushe tulikotoka.
HILI SI LA KURUDI MEZANI.