Sidhani, kama Tanzania imefika huko. Tutafahamu.Hili la wajeshi wa kigeni ni kweli japo watapinga. Tumewaona huku mitaani hawajui kiswahili
Ukimpata daktari ukaongea naye kwa siri atakuelezea alivyowahoji majeruhi au ndugu wa majeruhi. Iwe kwa siri maana nao wanaogopaSidhani, kama Tanzania imefika huko. Tutafahamu.
Na wanaongozana na polisi wenyewe.Hili la wajeshi wa kigeni ni kweli japo watapinga. Tumewaona huku mitaani hawajui kiswahili
Hans pope wasimba??huyo askofu nae kaanza chai. Afisa wetu mmoja mkubwa wa Polisi, alikamatwa na Idd Amin hapa mpakani Mtukula. Alikuwa chotara, marehemu Hans Pope kutoka Iringa. Idd Amin akadai Tanzania inatumia mamluki. Akamuua na kumhifadhi kwenye jokofu kama ushahidi kwa miaka mingi. Umamluki una gharama chungu. Tusipuuze.
mmmmm mbona ni Chai hapo kwa Hans Pope ?
Mkuu walikuepo walikua wanatumia Alphard nyeusi wakishuka sehemu wanapiga risasi watu wawili au watatu then wanaondokaSidhani, kama Tanzania imefika huko. Tutafahamu.
Kama ni hivyo Chief, haikuwa sahihi. Hilo tulikemee wote kwa umoja wetu.Mkuu walikuepo walikua wanatumia Alphard nyeusi wakishuka sehemu wanapiga risasi watu wawili au watatu then wanaondoka
Kama wewe ni mzaliwa wa juzi tu, usibishi wanachokueleza waliokuwepo wakati huo. Mimi mwenyewe nilikuwepo. Ngoja nikupashe japo kwa ufupi ilivyokuwa.Hans pope wasimba??huyo askofu nae kaanza chai
Asante mkuu kwa historia na elimu nzuri,Sasa huyu hans pope wa Simba nae c wanasema alipigana vita ya Kagera?Kama wewe ni mzaliwa wa juzi tu, usibishi wanachokueleza waliokuwepo wakati huo. Mimi mwenyewe nilikuwepo. Ngoja nikupashe japo kwa ufupi ilivyokuwa.
Hans Pope alikuwa Regional Police Commander wa Mkoa wa Ziwa Magharibi, ambao siku hizi unaitwa Mkoa wa Kagera. Intelijensia ilipata habari kwamba Idd Amin atashambulia Tanzania. Kwa hiyo Tanzania itume jeshi Bukoba kwa tahadhari. Kwa sababu ya vita baridi vilivyokuwa vikiendelea kati ya nchi za Magharibi na Mashariki, Nyerere alikataa kufanya hivyo kwa kuogopa kuambiwa anachochea vita.
Kweli Amin akashambulia, na kwa kuwa hakukuwa na jeshi upande wetu, polisi ndio wakajitokeza kupambana naye, wakiongozwa na RPC Hans Pope. Polisi wetu wakazidiwa nguvu na wanajeshi wa Amin. Hans Pope akauawa, na hapo ndipo Amin akasema Tanzania wanasaidiwa na Wachina, akitaja sura ya mchotara Hans Pope kama mfano. Sehemu ya Tanzania iliyopo upande wa pili wa Mto Kagera, akaiteka na kuvunja daraja walilokuwa wakivukia Watanzania wa pande mbili hizo za Mto Kagera. Amin akaomba aingizwe kwenye Guiness Book of Records kwamba ameteka sehemu ya nchi ndani ya dakika 15 tu. Nyerere alikaa kimya kwa siku tatu akisubiri matamko ya nchi zingine kulaani kitendo hicho cha Amin, na kila siku alikuwa anakwenda kanisani. Sana sana matamko yalitolewa na nchi za Magharibi ni kuiomba Tanzania 'to act with restraint'. Siku ya tatu, ndipo Nyerere akatumia uwezo wake mkubwa wa kuhamasisha. Akalihutubia Taifa kwa kusema kwamba joka limeingia nyumbani mwetu. Tuna kazi moja tu ya kulitoa nje. Sababu tunayo; nia tunayo; na uwezo tunao. Bahati nzuri Amin mwenyewe ametusaidia kwa kuutangazia ulimwengu kwamba ameteka sehemu ya nchi yetu. Hivyo, hakuna mtu wa kutulaumu kwamba tunaenda vitani. Hapo ndipo jeshi letu likaingia mzigoni. Wakawa wakipiga risasi kutoka upande wetu wa mto huku mainjinia wakilikarabati daraja, mpaka lilipotengemaa ya kutosha kuweza kupitisha silaha. Baada ya kuikomboa hiyo sehemu iliyokuwa imetekwa, ndipo Museveni akakazana na askari wake, akisaidiwa na jeshi letu, mpaka Kampala ilipotekwa na Amin kuikimbia nchi. Baada ya vita Nyerere akatangaza kubadili jina la mkoa kutoka Ziwa Magharibi kuwa Kagera. Mkoa wa Mara ulikuwa ukiitwa Ziwa Mashariki. Nao ukabadilishwa jina kuwa Mara.
Kwa hiyo, maelezo ya Askofu Bagonza ni ya kweli kabisa.
Mtawala anayeingiza mercenaries ili waue raia wake wanaompinga hatufai hata kwa sekunde moja zaidi. Ni msaliti wa taifa asiyesameheka!Ameandika Askofu Bagonza
Kuna mambo ukiyakalia kimya yanaisha yenyewe kwa sababu hayakusaidii wala hayakuumizi.
Kuna mambo ukiyakalia kimya hayaondoki yenyewe na ni ya hatari.
Hili la Askari wa Kukodi (Mamluki au Mercenaries), LISIKALIWE kimya. Kama ni kweli wapo, WAONDOLEWE mara moja kimya kimya. Kwa nini?
1. Wakati wa vita ya Uganda, Iddi Amin alileta Askari wa Libya kumsaidia. Tukawateka. Hatukuwaua. Baada ya vita tuliwarudisha Libya kutokea DSM. Ilikuwa aibu kubwa kwa Libya na Uganda. Tulionekana waungwana. Kutumia mamluki kwa migogoro yetu ya ndani kunafuta heshima yetu ya wakati ule.
2. Ni kejeli na matusi kwa vyombo vyetu vya ulinzi. Vyombo vyetu ni fahari yetu na ni nyeti kama makalio yetu. Eneo nyeti si za kuguswaguswa na wageni. Vyaweza kuwa kimya kwa heshima ya wakuu lakini vinajisikia kuaibika.
3. Afisa wetu mmoja mkubwa wa Polisi, alikamatwa na Idd Amin hapa mpakani Mtukula. Alikuwa chotara, marehemu Hans Pope kutoka Iringa. Idd Amin akadai Tanzania inatumia mamluki. Akamuua na kumhifadhi kwenye jokofu kama ushahidi kwa miaka mingi. Umamluki una gharama chungu. Tusipuuze.
4. Pamoja na kuwa katika giza la mawasiliano, lakini malalamiko yanayosikika yana mashiko kwa sababu watuhumiwa wameacha “DNA” katika shughuli zao. Watu wetu wako tayari kuuawa na watanzania wenzao. Tusipuuze, tutapuuzwa.
5. Tumekuwa wakali na makini katika vyombo vyetu kutoingiza watu wenye uraia tata. Tunaanzaje kuleta majeshi ya kigeni kuchangamana na majeshi yetu? Miaka ya karibuni zilisikika habari za Afisa wa jeshi kutoroka na kuhamia nchi ya kigeni akiwa na siri zetu. Hawa kama wapo wataondoka na siri ngapi? Natamani isiwe kweli!
6. Tumewahi kuwa na wataalam wa vyombo vyetu kwa ajili ya mafunzo katika vyote tangu tupate uhuru. Lakini haikuwa siri na yalikuwa ni mafunzo. Kutumia mamluki katika mambo ya kisiasa ni hatari kwa sababu inachochea tuanze kutazamana maeneo tutokapo.
Si kila suala la kisiasa ni la kiusalama. Naelewa kuna bangi ya siasa imemwagwa kwenye vyombo vyetu lakini isitufikishe kwenye mamluki.
Kama hamuelewani huko ndani jengeni madaraja, bomoeni kuta, au waiteni makamisaa wazalendo wawakumbushe tulikotoka.
HILI SI LA KURUDI MEZANI.
. Afisa wetu mmoja mkubwa wa Polisi, alikamatwa na Idd Amin hapa mpakani Mtukula. Alikuwa chotara, marehemu Hans Pope kutoka Iringa. Idd Amin akadai Tanzania inatumia mamluki. Akamuua na kumhifadhi kwenye jokofu kama ushahidi kwa miaka mingi. Umamluki una gharama chungu. Tusipuuze.
mmmmm mbona ni Chai hapo kwa Hans Pope ?
Asante mkuu kwa historia na elimu nzuri,Sasa huyu hans pope wa Simba nae c wanasema alipigana vita ya Kagera?
Kuna mambo mawili, moja ni ukweli wa uwepo wao ndani ya nchi, pili ni nani alikuwa nyuma yao? La pili ni muhimu zaidi.Mkuu walikuepo walikua wanatumia Alphard nyeusi wakishuka sehemu wanapiga risasi watu wawili au watatu then wanaondoka
Kwangu sioni logic hata kidogo ya mtawala kuingiza mamluki ili kudhbiti raia, wakati huo huo wewe ndio Amiri jesh mkuu. Hao ulio agiza pengine si hata platoon moja ya jeshi watafanya nini? na utawagawa ktk mikoa ipi? Maana kama ni rais logic ni kuwa anapingwa nchi nzima! Sasa Hao mamluki kwanini wakae mwanza na dar tu kwa mfano? wale walio pinga urais/uchaguzi Arusha watadhbitiwa na nani?Mtawala anayeingiza mercenaries ili waue raia wake wanaompinga hatufai hata kwa sekunde moja zaidi. Ni msaliti wa taifa asiyesameheka!
Maybe to deploy a more ruthless force kwenye maeneo fulani tukutu. In general, ukitaka kupata logic ya moves za huyo fazafaka (hata kwa kutumia tochi) utahangaika sana.Kwangu sioni logic hata kidogo ya mtawala kuingiza mamluki ili kudhbiti raia, wakati huo huo wewe ndio Amiri jesh mkuu. Hao ulio agiza pengine si hata platoon moja ya jeshi watafanya nini? na utawagawa ktk mikoa ipi? Maana kama ni rais logic ni kuwa anapingwa nchi nzima! Sasa Hao mamluki kwanini wakae mwanza na dar tu kwa mfano? wale walio pinga urais/uchaguzi Arusha watadhbitiwa na nani?
Kuna dalili gani ya kuwa vyombo viliasi au havikuwa karibu na rais kiasi cha yeye kuagiza mamluki?
Okay, swali la pili ni nani kawaleta? Umenifurahisha hapo ktk kupata logic.Maybe to deploy a more ruthless force kwenye maeneo fulani tukutu. In general, ukitaka kupata logic kwa moves za huyo fazafaka (hata kwa kutumia tochi) utahangaika sana.
Mashuhuda wanasema wamekutano na hao mercenaries, ambao hawajui hata Kiswahili.
Kama ni kweli, hiyo ni decision nzito na sensitive sana. Mtu pekee anayeweza kuidhinisha ni Rais. Anyone else atakuwa anatafuta punishment kali sana!Okay, swali la pili ni nani kawaleta? Umenifurahisha hapo ktk kupata logic.
Ni jambo sensitive twende nalo kwa umakini sana.