Nimestuka sana. Tafakari uiombee nafsi yako radhi kwa Mungu pamoja na mwenzio aliyemuita Askofu na Mtumishi wa MUNGU mpumbavu. Vinginevyo laana itakuwa juu yenu kuanzia leo hii.
Pili, Askofu Bagonza na wengine wengi wa jinsi yake ndio haswa wanaujua wito wao mkuu walioitiwa wa kupigania haki, utu na ukweli bila kuogopa. Kwa maneno mengine kupiga vita dhuluma, uonevu na hata ujangili wa kisiasa. Ni ajabu kwamba siku hizi ukipigania haki, usawa na uhuru unaitwa CHADEMA. Tafsiri yangu ni kwamba watawala wa sasa wahahusishwa na kuwa kinyume na hayo. Ni hatari kweli kweli. Askofu na Maaskofu na Masheikh ipiganieni haki msikae kimya na wala msiwaachie wachache. Ndio wito mkuu wa Kanisa, Misikiti na hata wasio na dini rasmi. Endelea Baba Bagonza nchi ipone.