Askofu Bagonza: Jakaya Kikwete hana ushawishi wowote kwenye Awamu ya Sita

Askofu Bagonza: Jakaya Kikwete hana ushawishi wowote kwenye Awamu ya Sita

Unaweza ukashangaa 2025 mgombea urais CDM akawa JK wa saigoni...na makamanda tukampigania balaa, makamanda hatuaminiki sisi..
 
Nikisikia kiongozi wa dini anajihusisha na masuala ya siasa huwa nakwazika sana.

Sana sana nafarijika napoona anahimiza waamini wajikite katika kufuata misingi yote pasipo kuvunja sheria za nchi.
Kwakuwa uwezo wako wa kufikiri ni mzigo sana.
Kazi ya kiongozi wa dini ni pamoja na kuelekeza mema na kukemea mabaya. Watawala pia ni waumini wa dini mbambali

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
Unaweza ukashangaa 2025 mgombea urais CDM akawa JK wa saigoni...na makamanda tukampigania balaa, makamanda hatuaminiki sisi..
Tz kuja kupata Raisi kama JK ambaye ni diplomat mzalendo na Raisi mstarabu itachukua mda, watu wa lijivunia kua Watanzania dimikurasia na Utawaala wa sharia kwa angalau asilimia kubwa ulionekana, Kosa la JK ambalo citakuja kumsahau ni kutuletea huyu JPM wake uncivilised man, katurudisha nyuma miaka kama 20 na chief Hangaya ameanza kumiiga huo buana.
 
Nikisikia kiongozi wa dini anajihusisha na masuala ya siasa huwa nakwazika sana.

Sana sana nafarijika napoona anahimiza waamini wajikite katika kufuata misingi yote pasipo kuvunja sheria za nchi.
Lazima wewe unaejiita Shetani ni pepo, huwezi ipenda heri ya baba Askofu…
Umelaaniwa duniani na mbinguni.
 
Hahahaha.. Bagonza si ndio huyu aliisifia sana awamu hii?
 
Vipi Gwajiboy 2025 ataamua kurejea kwenye ile kazi yake ambayo ni ya hadhi juu mno kuliko hata urais wa nchi?

Kumtumikia Mungu waweza linganisha na kutumikia watu? Thubutu!

Hiiiiii bagosha!
Gwajima 2025 tutamfanya awe mshenga wetu wa kumleta membe chamani baada ya ile ya kumleta lowasa 2015
 
Nayaheshimu maoni yako kwangu kama ninavyoyaheshimu ya akina Bagonza.....

Maoni ya mtu si lazima yawe sahihi na yenye UHALISIA...
Ndio useme unaona maoni hayo sio sahihi kwa sababu gani, tupime sababu zako vs kile alichoandika Bagonza, usizunguke zunguke tu.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Kwa hiyo sasa hivi mnakili kwamba selikali hii inaongozwa na sukuma gang tena?
 
Mie naongezea. Bagaonza na wenzako wanaojificha kwenye majoho anzisha chama badala ya kujiingiza kwenye siasa kwa mlango wa nyuma. Kikwete alikuwa bomu kuliko rais yeyote aliyewahi kuumbwa. Alikuwa rahisi na siyo rais. Alikuwa mzururaji na mtupu upstairs.
Kwani askofu kaongelea ubora wa awamu ya 4 au katoa utofauti wa awamu ya 4 na 6.Vip kichwa chako ni kidogo sana kuelewa au shida nini?
 
Huko siko kujikomba mjomba.

Kenya, Zambia, Malawi, SA hakuna uhasama kati ya vyama madarakani na vyama vya upinzani.

Uhasama baina ya vyama tawala na vyama vya upinzani nyumbani kwao ni Uganda, Burundi, Rwanda, Zimbabwe, Mozambique na Tanzania kutokea awamu ya tano.

Bado haikufikirishi?

Awamu #5 na #6 ni machukizo hata kwa Mola.

JK alikuwa Jembe. Viva JK!
Si mlikuwa mnasifu kwamba sukuma gang wamekomeshwa?

Na bado
 
Viongozi wa dini ni wananchi kama wengine!
Viongozi wa dini wanaongoza wenye itikadi na wasio na itikadi za kisiasa!
Viongozi wa dini ni kimbilio kwa wanasiasa mambo yanapokuwa magumu!
Viongozi wa dini wanatakiwa kuwa wa kweli na kuwaongoza waumini wao katika ukweli!
Viongozi wa dini wanatakiwa kukemea maovu!
Viongozi wa dini wanapaswa kujihusisha kikamilifu na siasa kwa sababu siasa hutumika kufanya maamuzi ya uendashaji wa nchi!
Viongozi wa dini wanapaswa kusimama kidete ili wapatikane viongozi wa kisiasa wenye utashi na nia ya dhati kuwatumikia wananchi ambao ni waumini wao!
Viongozi wa dini wanaosapoti wanasiasa waovu, wenye hila, wanafiki na wakandamizaji ni wabaya sana kwa mustakabali wa Ustawi wa jamii!
Kama wanavyosisitiza kwa waumini wao kuwa wakamilifu na waadilifu; hawana budi kuwaambia ukweli wanasiasa!
Siasa inatakiwa ishikamane pamoja na hofu ya Mungu!
Wasipokuelewa kwa ufafanuzi huu watakua na matatizo makubwa ya kufikiri.
 
Kikwete alijitahidi sana kujikomba kwa wapinzani Hadi kuwa anawaalika kunywa chai na vitafunwa ikulu lakini malipo upinzani waliyomlipa ni matusi kutwa kuwa ni Raisi dhaifu kuwahi tokea Tanzania ni mpole mno na kazi yake kucheka cheka tu

Wakafikia hatua Hadi ya kumwita Vasco da Gama kuwa sijui kala miguu ya kuku ndio maana hatulii nchini kutwa kusafiri wakasema Raisi hatakiwi kuwa mtu mpole na wa kucheka cheka.Ok Mungu akaona na akasikia na CCM tukasikia kilio chao Cha kutaka Raisi Mkali asiyecheka cheka na asiye mpole.Naona Sasa Askofu wa Chadema Bagonza na Chadema mnamwamkia Shikamoo Kikwete baada ya kushikishwa adabu na Marehemu Magufuli.

Haya Bagonza na Chadema niwaulize swali mnataka Raisi mpole na anayecheka cheka au Bado mko msimamo ule ule mliokuwa nao kabla Magufuli kuingia kuwa mnataka Raisi serious,Mkali asiyecheka cheka?

Kikwete pokea Shikamoo kutoka kwa Askofu Bagonza na Chadema .Usisite kuwajibu marahaba walishanyooka hao.Hata ulipohutubia kuwa huyu anayekuja sio mpole walizomea na kusema kwenda zako huko Hadi humu wakaandika Siku ukiondoka watafanya sherehe Leo wanalia Lia ohh Kikwete the best!!!!

Sasa Askofu Bagonza nenda kaungame dhambi kwa Kikwete mwende na Chadema wenzio na kabla ya kuungama dhambi mwamkieni kwanza Shikamoo
Acha porojo zisizo na maana wewe.
 
Tz kuja kupata Raisi kama JK ambaye ni diplomat mzalendo na Raisi mstarabu itachukua mda, watu wa lijivunia kua Watanzania dimikurasia na Utawaala wa sharia kwa angalau asilimia kubwa ulionekana, Kosa la JK ambalo citakuja kumsahau ni kutuletea huyu JPM wake uncivilised man, katurudisha nyuma miaka kama 20 na chief Hangaya ameanza kumiiga huo buana.

JK ni aina ya Rais anayepaswa kuongoza Taifa ambalo limeshaendelea tayari na watu wake kwa zaidi ya 80% wanajielewa na wamestaarabika na mifumo iko tayari...
JK anaweza kuongoza nchi yeyote Ulaya au hata USA..

JPM anafaa na alifaa kuliongoza Taifa kama hili ambali bado haliko tayari kimifumo na zaida ya 80% ya watu wake ni wajinga na wapumbavu wasiojielewa... Watanzania bado wako kwenye stage ya kuswagwa kama punda au ng'ombe na wakishavuka hiyo stage sasa ndio wanapaswa kuongoza watu kama JK....Unafikiri hawa wapumbavu wala rushwa na wezi wa mali za umma + wauza madawa nk utawashughulikia kimama kwa kuwalealea wataacha...hizi hela za miradi bila kuwa kiongozi mkorofi unafikiri miradi itakwenda...

Bado Watanzania wako kwenye stage ya mijeledi na kuswagwa..
 
Kiongozi wa dini hasa ya Kikristo Yesu kawatuma ulimwenguni kwenda kuhubiri Injili hakuna mahali Yesu aliwatuma wakahubiri Siasa hakuna popote Agano Jipya.

Hawa ni majobless waliojiunga na dini wapate sehemu ya kupata maisha sio vio gozi waliotumwa na Yesu kuhubiri injili ndio maana waweza kuta wanahubiri katiba mpya au tume huru badala ya injili!!!

Badala ya kufungua Biblia kuhubiri Injili unawakuta wameshika katiba wanasema tufungue katiba kifungu Cha ngapi huko!!!

Tatizo la Tanzania kutoendelea ni kuwa watu hawajiliti kwenye fani zao kuepuka mwingiliano.Kiongozi wa dini ana nafasi kubwa akisimama eneo lake kuleta mageuzi makubwa hata ya kiuchumi kupitia eneo lake tu mfano tulikuwa na yule mzee mchungaji Mwasapile mzee wa kikombe Cha Babu Hakuwa mwanasiasa akaema Mungu kamuonyesha kitu dawa.Akaanza kutumia kikombe chake kule
porini kabisa .Mamilioni ya watu walienda kutoka ndani na nje ya nchi na kwa kuwa lile eneo ni la hifadhi walilipa viingilio .Halmashauri kwa mwezi kwenye eneo Hilo kwa mwezi mapato yalikuwa milioni 15 Mwasapile akayapaisha kufikia bilioni moja kwa mwezi kwa wageni walioingia simu zilikuwa hazidaki kule makampuni ya simu yakaweka minara kuhudumia Mamilioni ya watu waenda kule, barabara ilikuwa mbaya ikatengenezwa, kampuni za kubeba abiria zikapata pesa hasa,hoteli zikafurika wageni nk lakini alisimama eneo lake tu

Hawa akina Bagonza ni weupe ndio maana hawajui wafanye Nini ndani ya wito wait
TB Joshua kule Nigeria alitunukiwa Hadi Nishani na serikali kwa kuiza religious tourist wengi walioingizia mapato serikali ya Nigeria kupitia Visa kuliko sekta yeyote na kuchangamsha uchumi wa Nigeria na image kupitia wageni wake na huduma yake.Watu kutoka mataifa mengi duniani walienda kwa TB Joshua!!! Bagonza watu toka taifa gani wanaenda kwake wageni wake labda Askofu mwamakula asiye na waumini akitokea kimara kwenda kumtembelea Bagonza ,!!!
Kwahiyo wakifanya hayo ya kiuchumi ni sawa ila wakikosoa serikali haitakiwi?.acha kutangatanga ndugu.dini ni kazi kama kazi nyingine.kama ambavyo kiongozi wa kisiasa anaweza akawa mhumini wa dini ndivyo ambavyo mkulima anaweza kua mwalimu na mchungaji kua mwanasiasa.zaidi ya hapo ni porojo tu kwasababu hatutaki kukosolewa.hao viongozi wa dini wangekua wanasifia tu kamwe usingesikia hizi porojo za kwamba kiongozi wa dini asihubiri mambo ya kisiasa ila kwavile wanakemea maovu ambayo watawala hawapendi kusikia ndipo zinakuja hizi hoja mfu.
 
JK ni aina ya Rais anayepaswa kuongoza Taifa ambalo limeshaendelea tayari na watu wake kwa zaidi ya 80% wanajielewa na wamestaarabika na mifumo iko tayari...
JK anaweza kuongoza nchi yeyote Ulaya au hata USA..

JPM anafaa na alifaa kuliongoza Taifa kama hili ambali bado haliko tayari kimifumo na zaida ya 80% ya watu wake ni wajinga na wapumbavu wasiojielewa... Watanzania bado wako kwenye stage ya kuswagwa kama punda au ng'ombe na wakishavuka hiyo stage sasa ndio wanapaswa kuongoza watu kama JK....Unafikiri hawa wapumbavu wala rushwa na wezi wa mali za umma + wauza madawa nk utawashughulikia kimama kwa kuwalealea wataacha...hizi hela za miradi bila kuwa kiongozi mkorofi unafikiri miradi itakwenda...

Bado Watanzania wako kwenye stage ya mijeledi na kuswagwa..
Huyo mtu wakutuswaga hivyo atapatikana vip?.Ndo maana wenye akili wanataka katiba mpya yenye ubora utakao weka mifumo thabiti yakuongoza nchi kwenye kila nyanja badala yakutegemea mtu ambaye ata akipatikana bado atapita uku nchi ikiendelea kuwepo.
 
Ndio useme unaona maoni hayo sio sahihi kwa sababu gani, tupime sababu zako vs kile alichoandika Bagonza, usizunguke zunguke tu.

Huyo chawa akitoa sababu hata moja usiache kutustua mkuu 😁😁
 
Back
Top Bottom