Pre GE2025 Askofu Bagonza: Kanisa likijenga Shule ama Hospitali halihojiwi na Serikali, lakini likihoji mbona dawa hakuna linaambiwa lisichanganye dini na siasa

Pre GE2025 Askofu Bagonza: Kanisa likijenga Shule ama Hospitali halihojiwi na Serikali, lakini likihoji mbona dawa hakuna linaambiwa lisichanganye dini na siasa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Jibu hoja yake hata hilo fungu ulilotumia inaonekana hujui maana yake.
Usipindishe. Ninamaanisha yeye aendelee na kazi yake ya uongozi wa kiroho na kazi za kisiasa awaachie wanasiasa.
 
Labda Askofu Bagonza anatamani sana majukwaa ya kisiasa kuliko kutumikia wanakondoo wake. Aamue moja tu kama Padre wa zamani Dr Wilbroad Slaa, atoke madhabahuni aje apambane na akina Nape na Iddi Nondo.

Bagonza anajuwa kabisa kuwa Biblia imeandika:-
Mathayo 22:21 BHN
Wakamjibu, “Ni ya Kaisari.” Hapo Yesu akawaambia, “Basi, ya Kaisari mpeni Kaisari, na ya Mungu mpeni Mungu.”
Oooh kumbe siasa na wanasiasa si vya MUNGU??
Huoni kwamba kwa mantiki hiyo ndo maana hawakanyiki wala hawana aibu na hofu ya MUNGU ndani yao??
Je, waendelee hivyo??
 
Umesoma ila hujaelewa,rudia kusoma mara nyingi zaidi utamuelewa Askofu Bagonza, otherwise shuleni ulienda kusomea ujinga
Bagonza ana kitu gani anachojuwa? Uongozi wa kanisa tu waluteri wanamuona takataka? Ndiyo atathubutu kuleta ushawishi wa kisiasa?

Kwanza mwambieni apeleke matunzo kwa mwanaye aliyemzaa na kimada wa Arusha!! Eti naye ni Askofu???!!!
 
Wakiambiwa ukweli unao wapiga kwenye mbavu ndio wanaanza kulalamika na kuleta madai ya dini na siasa
 
Mpotoshaji mkubwa, si umuulize Katekista maana ya fungu Hilo kuliko kubwabwaja?
Wewe ndiye mpotoshaji. Sihitaji kateskista kuelewa mstari huo. Na hakuna maana moja kwenye tafsiri. Acha kuishi kwa KUKARIRI
 
Rwakatare alikuwa kiongozi wa kanisa na aligombea ubunge viti maalum ccm na alipata na hakujivua uongozi wa kanisa lake. Dini na Siasa
Mwamposa alipewa ubunge wa Kawe akiwa kiongozi wa kanisa, na hakujivua uongozi wa kanisa lake. Dini na Siasa.
Hii imekaaje?
Siasa ni ya watu wote wa MUNGU!
Siasa ni lazima!
Siasa ni maisha!
Dini zinahitaji kukidhi kanuni, sheria na mahitaji ya kisiasa ili ziwe rasmi!
Hivyo siasa ni kama maji!
 
Mbona Gwajima mpo naye huko CCM lakini hamsemi aache madhabahu? Au akiwa anaiunga mkono CCM hana haja ya kutoka nje ya madhabahu lakini akihoji Serikali anatakiwa aachane na madhabahu Kwa sababu ni kuchanganya Dini na siasa? Hivi hamwonagi aibu kutetea ujinga?
Two wrongs do not make one right. Gwajima ahukumiwe kama Gwajima, mimi na deal na huyu Bagonza askofu aliyetelekeza mwanaye aliyezaa na kimafa
 
Sio kwamba Askofu anatamani siasa, bali wewe na watu wa namna yako, ama ni watu wanafiki au mmekosa uelewa wa maana ya siasa.
Anatamani sana, na ndiyo maana kila mara yuko na statements tu zenye utata.
 
Labda Askofu Bagonza anatamani sana majukwaa ya kisiasa kuliko kutumikia wanakondoo wake. Aamue moja tu kama Padre wa zamani Dr Wilbroad Slaa, atoke madhabahuni aje apambane na akina Nape na Iddi Nondo.

Bagonza anajuwa kabisa kuwa Biblia imeandika:-
Mathayo 22:21 BHN
Wakamjibu, “Ni ya Kaisari.” Hapo Yesu akawaambia, “Basi, ya Kaisari mpeni Kaisari, na ya Mungu mpeni Mungu.”
Na hiyo ndo siasa yenyewe sasa! Bravo Yesu🙏🙏
 
Kuelewa maandiko matakatifu ni kazi sana ndugu yangu.hoja imekaa vzr sana kutoka kwa Askofu Bagonza isipokuwa watu Wana uwezo mdogo sana wa kuelewa.
Ni kazi kubwa kuelewa maandiko matakatifu kwa ma- pimbi kama wewe
 
Sio kwamba Askofu anatamani siasa, bali wewe na watu wa namna yako, ama ni watu wanafiki au mmekosa uelewa wa maana ya siasa.
Siasa inaratibu vingi kuanzia unavyojiongoza, maendeleo yako, fursa ulizo nazo, matarajio yako na unavoishi na watu!
Hivyo sijui unachora vipi mpaka kati ya siasa na mambo mengine!
Anyways; Askofu Gwajima mtamvua lini uanasiasa??
Au mchanganyo hutokea pindi mnapokosolewa??
 
Rwakatare alikuwa kiongozi wa kanisa na aligombea ubunge viti maalum ccm na alipata na hakujivua uongozi wa kanisa lake. Dini na Siasa
Mwamposa alipewa ubunge wa Kawe akiwa kiongozi wa kanisa, na hakujivua uongozi wa kanisa lake. Dini na Siasa.
Hii imekaaje?
Mwamposa kapewa ubunge wa kawe mwaka gani?
 
Dkt.Benson Bagonza Askofu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe alikuwa akihojiwa na Mwanahabari nguli Jenerali Ulimwengu ambaye alimuuliza " Baba Askofu ningependa nikuulize, wewe umekuwa ukitoa mawazo yako hadharani juu ya masuala ya kisiasa huwa hakuna 'contradiction' kwamba unaingiza labda Siasa ndani ya Dini?..."

Askofu Dkt. Bagonza. “Mimi nadhani siasa ni uwanja wa watu wote lakini Dini ni uchaguzi wa mtu binafsi, Siasa ni yetu wote kwakuwa tunapiga kura, tunalipa kodi, ni yetu wote na sioni sababu ya mtu kumuwekea mtu mwenzake mipaka..." -

Aliongeza kusema, "Kwanini mnahoji kwamba nachanganya Dini na Siasa?, nikijenga Shule mbona hamsemi nachanganya Elimu na Dini?, nikijenga Hospitali mbona sihojiwi kwamba nachanganya Afya na Dini?, nikichimba kisima cha maji kwa wananchi mbona hawasemi kwamba unaingilia idara ya maji?..." -Askofu Dkt. Bagonza

"... nikimkuta mgonjwa pale nikampa dawa siulizwi kwanini unachanganya Dini na Siasa na hata sihojiwi kwanini unachanganya Afya na Dini lakini nikihoji kwanini mgonjwa huyu hana dawa?, kwanini serikali haileti dawa kwaajili ya mgonjwa wanasema aaah.., anachanganya Dini na Siasa, sasa huoni hapo kwamba kuna shida ya kimantiki?” -Askofu Dkt. Bagonza.
Nilimuelewa sana magu alipoamua kuhangaikia hospitals za serikali

Hizi huduma za kijamii kama
Hospitals za mission pamoja na faida kubwa kwa wananchi, zimekua zikitumika kama fimbo

Ufujaji wa miaka ile elct Kwa kupitia afya na elimu ulikua mkubwa

Serikali ikaze sana kwenye kusimamia huduma inazolipia kwa mission hospitals
 
Mathayo
Wakamjibu, “Ni ya Kaisari.” Hapo Yesu akawaambia, “Basi, ya Kaisari mpeni Kaisari, na ya Mungu mpeni Mungu.”[/QUOTE]
 
Back
Top Bottom