Pre GE2025 Askofu Bagonza: KKKT ina Mkuu wa Kanisa mmoja tu, Dereva wawili hawawezi kuendesha gari moja kwa wakati mmoja

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kama Askofu Shoo akigombea ubunge kupitia CCM, hata mimi ntampigia kampeni. Chadema wamemlia hela zake kwa muda mrefu, bora amegundua uongo wao.
 
Nje ya mada kidogo kuna mapadri waliuawa na kutupwa kwenye matenk ya maji tena kanisani, mbona sisikii kanisa likishinikiza polisi wafanye uchunguzi haraka? Au tuamini ni INSIDE JOB?
 
Askofu Dr Bagonza wa KKKT Dayosisi ya Karagwe amesema Kwa sasa Taifa limefika Mahali pagumu sana sana

" Kuna watu wanatumia Dini Kueneza Siasa na kuna watu wanatumia Siasa Kueneza Dini Mimi natumia Ujinga Kueneza Dini na Siasa"

Source: Jambo TV

Aliyemuelewa baba askofu naomba Ufafanuzi tafadhali nisije kuchuma Dhambi Bure 🐼
 
Hahaa.......wewe unatumia nini? Siasa kueneza uchawa.
 
Mnara wa babeli. Sijawahi kuona clip ya Bagonza na Mwamakula wakihubiri kanisani, wao ni siasa tu
 
Pameanza kuchangamka kweli lakini ni kwa maneno tu !
Unadhani Watanzania wanapenda mabadiliko yoyote, chief? Ufahari wa Bongo ni kutunishiana misuli twitani, Insta, FB na kwenye mitandao mingine ya kijamii.

Baada ya hapo, watu wanasalimiana kwa furaha, wenye kununa nao walee; tunalala halafu kesho yake inatukuta mzigoni tukiganga yaliyopo na yajayo.

Ndiyo maana haishangazi kuwakuta watu kiduchu kwenye mikutano, mijadala na maamuzi nyeti kabisa kitaifa.
 
nadhan hakuna jambo au wazo jipya wala fikra mbdala ambalo Baba Askofu Bagonza amelieleza zaidi ya kupingana kisiasa na Askofu mwenzie kitu ambacho ni kawaida kabisa.

Hata baada ya Askofu Malasusa kuchaguliwa tena kwenye wadhifa wa kanisa alionao hivi sasa, huyu Askofu wa Karagwe Dr.Bagonza aling"aka sana na kuandika kwamba kwenye uchaguzi wao wa kumchagua mkuu wa kanisa hilo huwa hawachagui wao bali kiongozi wa kanisa hilo huchaguliwa kutoka mahali Fulani ambako hakuweka wazi ni wapi.

Kiufupi Askofu Bagonza hua ana chuki binafsi sana dhidi ya maoni na mitazamo ya maaskofu wa kanisa hilo, lakini pia anatamani sana kua kiongozi mkuu wa kanisa hilo Tanzania.

Lakini ujuaji wake mwingi umemfanya akose ushawishi kabisa ndani ya kanisa hilo ispokua ana ushawishi kiasi nje ya kanisa hilo, ambao hata hivyo hauna athari zozote kisiasa nchini , kwasababu ana hulka ya kupinga mawazo na mitazamo huru ya wengine bila kueleza wazo na mtazamo mbadala na bora bora zaidi ya wengine 🐒
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…