The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
MIAKA 5 IMEPITA LAKINI Dr. BASHIRU BADO HANA MPINZANI!
Miaka 5 iliyopita, siku kama ya leo, Dr. Bashiru Ally, akiwa Katibu Mkuu wa CCM, alisema maneno mazito. Kwa maoni yangu, hayajajibiwa mpaka leo. Naheshimu kimya chake ambacho kina nguvu kuliko maneno yake. Ni juu yetu kudadavua uzito wa maneno yake yenye umri wa miaka 5 lakini yasiyochuja.
Katika kutafakari, niliandika hivi:
Duh!! Najua hili limegusa sana. Kila gazeti litaandika na sisi "mashabiki waandamizi" hatukosi cha kuchangia. Dr. Bashiru ni mtu makini, hawezi kukosa ufafanuzi. Anapojiandaa kufanya hivyo, ajue matamshi yake yanaweza kumaanisha moja ya haya au yote kwa pamoja:
1. Wapiga kura hawaamui mshindi, dola ndiyo inaamua ( Wananchi mpige kura, msipige, mtupatie kura au mtunyime, haisaidii lolote).
2. Tume ya Taifa ya Uchaguzi siyo huru na haina lolote. Dola ndiyo inaamua mshindi.
3. Chama tawala hakina uwezo kuliko dola na hakishiki hatamu. Dola ndiyo imeshika hatamu.
4. Dola haina uhuru wa kujiamulia, bali inaagizwa na chama tawala (inatumiwa).
5. Hata wabunge na madiwani wa upinzani walioshinda, ni kwa fadhila za dola.
6. Tunapoteza raslimali kuendesha uchaguzi uliokwishaamuliwa na dola.
7. Kwa kuwa dola ndiyo inaamua, siku ikiamua vinginevyo, hata chama tawala kitaondoka madarakani.
Naamini sivyo alivyomaanisha lakini masikioni ndivyo alivyosikika. Kuna haja ya kujisikiliza kabla hujasikilizwa.
Pimeni maneno haya kwa muktadha wa:
1. No Reform, No Election
2. Hatuondoki madarakani mpaka Yesu
arudi,
3. Hata mpigie kura kule kwingine, sisi
tutaunda serikali,
4. Atakayemtangaza mpinzani hana kazi
(Awe DED au Afisa wa umma)
5. Huwezi kumpigia mpinzani halafu ukadai uletewe maendeleo.
Kwenye kampeini tujifunze kuweka akiba ya maneno.