Pre GE2025 Askofu Bagonza: Miaka mitano imepita lakini Dkt. Bashiru bado hana mpinzani

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kwani nchi hii askofu ni bagonza tuu? Hao wengine hawajui kazi yao ya uaskofu hadi hatuwaoni kwenye uanaharakati wa Chadema?
Hapa hatakiwi kujadiliwa Askofu Bagonza, bali hoja aliyoitoa.
Hata hivyo, ni muhimu kuelewa kwamba watu wenye akili ni wachache sana kwenye makundi yote, maaskofu wakiwemo.
 
CCM inatumia dola kubaki madarakani halafu Makala anakuja na ngonjera na kuushambulia mkakati wa NO REFORMS NO ELECTION.
 
Mijitu kama hili ndio mwanzo wa vita na umaskini kwa nchi nyingi za Africa
 
MIAKA 5 IMEPITA LAKINI Dr. BASHIRU BADO HANA MPINZANI!

Miaka 5 iliyopita, siku kama ya leo, Dr. Bashiru Ally, akiwa Katibu Mkuu wa CCM, alisema maneno mazito. Kwa maoni yangu, hayajajibiwa mpaka leo. Naheshimu kimya chake ambacho kina nguvu kuliko maneno yake. Ni juu yetu kudadavua uzito wa maneno yake yenye umri wa miaka 5 lakini yasiyochuja.

Katika kutafakari, niliandika hivi:

Duh!! Najua hili limegusa sana. Kila gazeti litaandika na sisi "mashabiki waandamizi" hatukosi cha kuchangia. Dr. Bashiru ni mtu makini, hawezi kukosa ufafanuzi. Anapojiandaa kufanya hivyo, ajue matamshi yake yanaweza kumaanisha moja ya haya au yote kwa pamoja:

1. Wapiga kura hawaamui mshindi, dola ndiyo inaamua ( Wananchi mpige kura, msipige, mtupatie kura au mtunyime, haisaidii lolote).

2. Tume ya Taifa ya Uchaguzi siyo huru na haina lolote. Dola ndiyo inaamua mshindi.

3. Chama tawala hakina uwezo kuliko dola na hakishiki hatamu. Dola ndiyo imeshika hatamu.

4. Dola haina uhuru wa kujiamulia, bali inaagizwa na chama tawala (inatumiwa).

5. Hata wabunge na madiwani wa upinzani walioshinda, ni kwa fadhila za dola.

6. Tunapoteza raslimali kuendesha uchaguzi uliokwishaamuliwa na dola.

7. Kwa kuwa dola ndiyo inaamua, siku ikiamua vinginevyo, hata chama tawala kitaondoka madarakani.

Naamini sivyo alivyomaanisha lakini masikioni ndivyo alivyosikika. Kuna haja ya kujisikiliza kabla hujasikilizwa.

Pimeni maneno haya kwa muktadha wa:

1. No Reform, No Election
2. Hatuondoki madarakani mpaka Yesu
arudi,
3. Hata mpigie kura kule kwingine, sisi
tutaunda serikali,
4. Atakayemtangaza mpinzani hana kazi
(Awe DED au Afisa wa umma)
5. Huwezi kumpigia mpinzani halafu ukadai uletewe maendeleo.

Kwenye kampeini tujifunze kuweka akiba ya maneno.
View attachment 3262791View attachment 3262792View attachment 3262793
Huyu Bagonza ana viini vya uhuni licha ya kuwa msomi.
Katika tafrani za matatizo KKKT mara zote yupo kundi la wahuni.
Karibuni alimtetea Askofu Mwaikali huko Dayosisi ya Konde, licha ya Askofu huyo kuwa na tabia za kihuni zisizoendana na Kanisa.
Sasa anamtetea Bashiru, pandikizi la Mwendazake, lenye uraia wenye utata.
Bagonza mwenyewe zilikuwepo tetesi za kuzaa nje.
Usituboe bwana.
 
Kwamba hamuachii madaraka kwakuwa mnahisi wengine wakiingia hawataachia?
mnaanzia wapi kuachia kwanzaa, Tindo pale ukishaonja uwaziri wa uchumi labda uletewe vifaru
 
Nenda shule uelewe maana ya dola. Usitake kupata tuition ya bure. Shule muhimu sana
Kweli kuna kuelimika na kukariri.., unadhani ukienda shule ndio utapata maana ya kitu fulani na sio kwa kuuliza aliyesema context ya alichosema huyo mtu alikuwa anamaanisha nini ?

Na kwa muktadha huo nikuulize wewe unadhani dola ni nini alafu uniambie maneno yaliyotamkwa kama sio ukweli wenyewe....; na maigizo yoyote ya vinginevyo ni katika tu kuleta peace na kujiridhisha kwamba ni vinginevyo...
 
Leta hela ya tuition. Hakuna knowledge ya bure. Mi nilisoma political science kwa mil 6

Kwahio umejibu qoute yangu kuniambia kwamba hauna jibu ? Wakati ungeweza kuokoa hio rasilimali muda ?, Kwahio na hapa tunaanza kujadili gharama uliyotumia na kisomo ulichosomea ? How has that got to do with anything Bashiru said na validity yake ?!!
 
Unataka somo la semister nzima ufundishwe siku moja. Dont take things easier
Kwahio umejibu qoute yangu kuniambia kwamba hauna jibu ? Wakati ungeweza kuokoa hio rasilimali muda ?, Kwahio na hapa tunaanza kujadili gharama uliyotumia na kisomo ulichosomea ? How has that got to do with anything Bashiru said na validity yake ?!!
 
Unataka somo la semister nzima ufundishwa siku moja. Dont take things easier
Kwahio watu waliosoma semester nzima ndio wanatambua kuhusu Dola ? Na yule mama ntilie kijiweni akiongelea Dola anakuwa amesoma Semester ngapi au akiongelea kitu ambacho unaweza ukakiona ni controversial itabidi umuulize anamaanisha nini kwanza kwa alichokisema ?

Ukizingatia hapa the main issue sio DOLA bali ni kuhusisha hilo DOLA na kinachoendelea na ukidadavua ndio unaweza kupata ukweli wa hali halisi na huenda wala sio hapa au pale bali ndio the Nature of the Game.... Hence anamaanisha nini kuhusu Dola; Mbili anaitumia vipi kwa faida yake; Tatu anafanya hayo within the legal boundaries hapo ndio Nne tunaweza kuongelea rectification ili the above if possible can be rectified....
 
Askofu Bagonza, saa ngapi unasoma biblia? Mbona uko busy na siasa? Si uvue majoho ya uaskofu uingie uwanja wa siasa, tunajua ww ni CHADEMA, si uchukue fomu gombea nafasi yoyote ya kisiasa alafu utakuwa umeingia uwanjani kucheza ngoma yenyewe.

Askofu, huoni unapata shida sana uko katika wito wa uaskofu, ila mawazo yako yapo siasani, njoo huku ucheze siasa, unachanganya mafaili askofu huoni, acha kuisema CCM, njoo uwanjani upambane na CCM uione ilivyo, maandishi tu hayasaidii kitu chochote.
Dini na siasa kipi kimetangulia?
 
Hata dini ni siasa pia
 
MIAKA 5 IMEPITA LAKINI Dr. BASHIRU BADO HANA MPINZANI!

Miaka 5 iliyopita, siku kama ya leo, Dr. Bashiru Ally, akiwa Katibu Mkuu wa CCM, alisema maneno mazito. Kwa maoni yangu, hayajajibiwa mpaka leo. Naheshimu kimya chake ambacho kina nguvu kuliko maneno yake. Ni juu yetu kudadavua uzito wa maneno yake yenye umri wa miaka 5 lakini yasiyochuja.

Katika kutafakari, niliandika hivi:

Duh!! Najua hili limegusa sana. Kila gazeti litaandika na sisi "mashabiki waandamizi" hatukosi cha kuchangia. Dr. Bashiru ni mtu makini, hawezi kukosa ufafanuzi. Anapojiandaa kufanya hivyo, ajue matamshi yake yanaweza kumaanisha moja ya haya au yote kwa pamoja:

1. Wapiga kura hawaamui mshindi, dola ndiyo inaamua ( Wananchi mpige kura, msipige, mtupatie kura au mtunyime, haisaidii lolote).

2. Tume ya Taifa ya Uchaguzi siyo huru na haina lolote. Dola ndiyo inaamua mshindi.

3. Chama tawala hakina uwezo kuliko dola na hakishiki hatamu. Dola ndiyo imeshika hatamu.

4. Dola haina uhuru wa kujiamulia, bali inaagizwa na chama tawala (inatumiwa).

5. Hata wabunge na madiwani wa upinzani walioshinda, ni kwa fadhila za dola.

6. Tunapoteza raslimali kuendesha uchaguzi uliokwishaamuliwa na dola.

7. Kwa kuwa dola ndiyo inaamua, siku ikiamua vinginevyo, hata chama tawala kitaondoka madarakani.

Naamini sivyo alivyomaanisha lakini masikioni ndivyo alivyosikika. Kuna haja ya kujisikiliza kabla hujasikilizwa.

Pimeni maneno haya kwa muktadha wa:

1. No Reform, No Election
2. Hatuondoki madarakani mpaka Yesu
arudi,
3. Hata mpigie kura kule kwingine, sisi
tutaunda serikali,
4. Atakayemtangaza mpinzani hana kazi
(Awe DED au Afisa wa umma)
5. Huwezi kumpigia mpinzani halafu ukadai uletewe maendeleo.

Kwenye kampeini tujifunze kuweka akiba ya maneno.
View attachment 3262791View attachment 3262792View attachment 3262793
Maandishi hayafutiki
 
Kipindi hicho Bashiru hakamatiki
 
Dola ni nini ?
Labda tuanzie hapo kwanza...
Kwa maoni yangu tu na sio lazima yawe ni kweli !
Mtu anaposema Dola mara nyingi ana refer kwenye maguvu ya Dola mahali yalipo !
Na hapo zaidi zaidi anamaanisha ni vyombo vya Usalama !
Yaani ni Armed Forces !
Kwa sababu tumesikia sehemu nyingi tu Vyombo hivyo vikiingia mitini kwa sababu yeyote ile Government huwa haina namna isipokuwa inaanguka kirahisi sana !
Recently ilitokea huko Syria !
Bashar al Asaad akabwaga manyanga !
 
Back
Top Bottom