Pre GE2025 Askofu Bagonza: Miaka mitano imepita lakini Dkt. Bashiru bado hana mpinzani

Pre GE2025 Askofu Bagonza: Miaka mitano imepita lakini Dkt. Bashiru bado hana mpinzani

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Askofu Bagonza, saa ngapi unasoma biblia? Mbona uko busy na siasa? Si uvue majoho ya uaskofu uingie uwanja wa siasa, tunajua ww ni CHADEMA, si uchukue fomu gombea nafasi yoyote ya kisiasa alafu utakuwa umeingia uwanjani kucheza ngoma yenyewe.

Askofu, huoni unapata shida sana uko katika wito wa uaskofu, ila mawazo yako yapo siasani, njoo huku ucheze siasa, unachanganya mafaili askofu huoni, acha kuisema CCM, njoo uwanjani upambane na CCM uione ilivyo, maandishi tu hayasaidii kitu chochote.
Pole sana Dada!
Tafuta kivuli kizuri hapo nje angalau upate upepo mzuuuri na mwanana itakusaidia sana
 
Unampangia muda wa kusoma biblia? akiwa chadema au Tlp inakuuma nini? Mbona mnashawishi viongozi wa dini kuiombea nchi hata kama kuna mambo ya wazi ambayo mnayakiuka kwa makusudi? Hoja zake ni za uongo au ni za kweli? Unadhani ni sahihi kila mtu kuiunga mkono CCM hata kama hataki?
 
Pole sana Dada!
Tafuta kivuli kizuri hapo nje angalau upate upepo mzuuuri na mwanana itakusaidia sana

Mimi ni mume wa mama yako, muulize Jay One ni nani atakuambia, huna adabu, pumbaf
 
MIAKA 5 IMEPITA LAKINI Dr. BASHIRU BADO HANA MPINZANI!

Miaka 5 iliyopita, siku kama ya leo, Dr. Bashiru Ally, akiwa Katibu Mkuu wa CCM, alisema maneno mazito. Kwa maoni yangu, hayajajibiwa mpaka leo. Naheshimu kimya chake ambacho kina nguvu kuliko maneno yake. Ni juu yetu kudadavua uzito wa maneno yake yenye umri wa miaka 5 lakini yasiyochuja.

Katika kutafakari, niliandika hivi:

Duh!! Najua hili limegusa sana. Kila gazeti litaandika na sisi "mashabiki waandamizi" hatukosi cha kuchangia. Dr. Bashiru ni mtu makini, hawezi kukosa ufafanuzi. Anapojiandaa kufanya hivyo, ajue matamshi yake yanaweza kumaanisha moja ya haya au yote kwa pamoja:

1. Wapiga kura hawaamui mshindi, dola ndiyo inaamua ( Wananchi mpige kura, msipige, mtupatie kura au mtunyime, haisaidii lolote).

2. Tume ya Taifa ya Uchaguzi siyo huru na haina lolote. Dola ndiyo inaamua mshindi.

3. Chama tawala hakina uwezo kuliko dola na hakishiki hatamu. Dola ndiyo imeshika hatamu.

4. Dola haina uhuru wa kujiamulia, bali inaagizwa na chama tawala (inatumiwa).

5. Hata wabunge na madiwani wa upinzani walioshinda, ni kwa fadhila za dola.

6. Tunapoteza raslimali kuendesha uchaguzi uliokwishaamuliwa na dola.

7. Kwa kuwa dola ndiyo inaamua, siku ikiamua vinginevyo, hata chama tawala kitaondoka madarakani.

Naamini sivyo alivyomaanisha lakini masikioni ndivyo alivyosikika. Kuna haja ya kujisikiliza kabla hujasikilizwa.

Pimeni maneno haya kwa muktadha wa:

1. No Reform, No Election
2. Hatuondoki madarakani mpaka Yesu
arudi,
3. Hata mpigie kura kule kwingine, sisi
tutaunda serikali,
4. Atakayemtangaza mpinzani hana kazi
(Awe DED au Afisa wa umma)
5. Huwezi kumpigia mpinzani halafu ukadai uletewe maendeleo.

Kwenye kampeini tujifunze kuweka akiba ya maneno.
View attachment 3262791View attachment 3262792View attachment 3262793
Upotoshaji wa kile aliongea na kumaanisha. Huyu msomi na mwanamapinduzi inahitaji akili kutoweza kupotoshwa na wapinga maendeleo kama watumishi wa matumbo yao kina Bagonza huku wakijidai ni watumishi wa mungu.
 
Kwani nchi hii askofu ni bagonza tuu? Hao wengine hawajui kazi yao ya uaskofu hadi hatuwaoni kwenye uanaharakati wa Chadema?
Hawaja jua wajibu wao ipasavyo?Lakini pia nchi yenye wajenga wengi wanaoamua kwenye kutekana na kuana kisa kukosoa serikali,wengi wanaona na heri kukaa kimya.ASKOFU BAGONZA AMECHAGUA FUNGU LILO JEMA
 
1. Wapiga kura hawaamui mshindi, dola ndiyo inaamua ( Wananchi mpige kura, msipige, mtupatie kura au mtunyime, haisaidii lolote).

2. Tume ya Taifa ya Uchaguzi siyo huru na haina lolote. Dola ndiyo inaamua mshindi.

3. Chama tawala hakina uwezo kuliko dola na hakishiki hatamu. Dola ndiyo imeshika hatamu.
Duuh
 
Back
Top Bottom