LGE2024 Askofu Bagonza: Nawaomba radhi niliowahamasisha ili waende wakajiandikishe kupiga kura

LGE2024 Askofu Bagonza: Nawaomba radhi niliowahamasisha ili waende wakajiandikishe kupiga kura

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Mkuu na kuonya kama mkristo acha tabia kushabiki a maovu na dhambi kisa vyeo vya CCM utapata laana wewe na watoto wako ,utapata laana wewe na wazazi wako.

Wewe unakuja unacho kifanya ni UCHAWA ili upate cheo serikalini.
Kumbuka huna ajira tangu tumalize chuo kikuu na ukaenda kugombea ubunge na ukokosa
nani akakosa ubunge gentleman?🤣

Gentleman,
unapotosha na kuwafunga kamba wadau mchana kweupe hivyo, halafu eti unakuja kunitishia na laana zako za kishirikiana, kweli? 🤣

unanitisha mimi mtumishi mwandamizi wa wananchi wa kata zaidi ya 20 nchini? halafu kabisaaaa nitishike na hawa wananchi wote zaidi ya laki3.5 wanatizama tu 🤣

Gentleman,
hapa nilipo ni kwa Neema na Baraka za Mungu. Sitikisiki wala sibabaiki na cheo au nafasi ya uongozi ndrugu wadau.

Itakua ni tamaa ya kiwango cha juu mno kuacha jukumu hili zito na muhimu zaidi la kutumikia wananchi na kubabaika na mihemko au makasiriko ya waliopoteza uelekeo 🐒

Mungu Ibarki Tanzania
 

Attachments

  • IMG_20230730_055342.jpg
    IMG_20230730_055342.jpg
    52.7 KB · Views: 9
Askofu Bagonza ameandika hayo kupitia ukurasa wake wa Facebook;


Mwaka 2019 tulitangaziwa kuna uchaguzi. Likawa shindano la kujaza fomu. CCM wakashinda. Wapinzani wakarudi darasani kujifunza kujaza fomu.

Mwaka huu tukatangaziwa, safari hii ni UCHAGUZI KWELI. Tukainuka kuhamasisha watu wajiandikishe. Wakaandikwa hata watakaofikisha miaka 18 miaka 5 ijayo. Idadi ya waliojiandikisha ikazidi ya wapiga kura. Tanzania tuna miujiza kweli.

Ghafla, uchaguzi “ukahairishwa” tukarudi tena kwenye mashindano ya kujaza fomu. CCM wameshinda tena. Wapeni maua yao. Lakini:

1. Nduguyo akikukosea muonye mkiwa wawili. Akikataa, chukua shahidi ukaonye tena. Akikataa liambie kanisa. Akikatalia kanisa, achana naye. Mwone kama mmataifa na mtoza ushuru (Mathayo 18:16-18). CCT, TEC na Bakwata wamesema tayari. Hata wasioomba wanaomba!

2. Wanyambo wana hekima isemayo; “Ukimwonya nduguyo ili afunike uchi wake akakataa, jiunge na wanaomcheka”. Nipo nacheka utadhani mazuri!

3. Tumemaliza ibada Musoma. Tumempata Mkurya mmoja akawa Askofu. Kofia ilitaka kugoma kuingia kichwani tukatamani tutafute ya jeshi. Yesu “aliyemteka” Mkurya akatii, kuna siku atawateka wanaokaidi maonyo ya kanisa lake kuhusu taifa.

4. Mgeni rasmi Prof John Kabudi, katupiga darasa ibadani. Ilani nzima ya chama chake imefunika mpaka wengine tukaondoka bila kula mchele. Katujulisha habari za BWAWA la umeme. Ahsante Prof LAKINI..

5. Watanzania hawa wanatamani Bwawa kubwa la kuzalisha Demokrasia. Bwawa hilo litalinda Bwawa la Umeme. Bila demokrasia wanaohujumu SGR watahamia kwenye umeme.

6. Najiuliza: Waweza kuwa na taifa huru lisilo na watu huru? Na je waweza kuwa na watu huru katika taifa lisilo huru? Niliwahi jibu swali nikiwa darasa la sita, lisemalo “Afrika ni Bara Tajiri lenye watu maskini: Jadili kwa kutoa mifano. Majibu yangu yalisababisha nifukuzwe shule mwaka mzima. Apumzike kwa amani Mwalimu aliyenifukuza.

7. Nimalize tafakuri yangu kwa kutoa pole kwa wahanga wa Kariakoo. Nitoe pole kwa familia Mama Kibiki. Waliomuua “wameishakufa” hata kama wanatembea. Nitoe pole kwa wote walioenda kwenye uchaguzi wakaambulia mashindano ya kujaza fomu. Nitoe pole kwa wote wanaolazimika kucheka wakati moyoni wanatamani kulia.

Nawaomba radhi wote niliowahamasisha kwenda kujiandikisha ili wapige kura. Nilidanganywa nami nikawadanganya. Sitarudia tena.

Mungu wetu ana kazi kweli kweli. Mwizi wa Kura anamuomba afanikiwe kuiba. Mlinzi wa kura naye anakanyaga mafuta ili alinde kura zisiibiwe. Lakini HADHIAKIWI.

Naipenda nchi yangu hata kama kuna wanaonilazimisha niichukie. Hata mkiniteka, SIICHUKII NCHI YANGU.
Wala hata asituombe radhi. Tarehe 27/11 tunaenda kupiga kura za HAPANA dhidi ya wagombea wa CCM waliopita bila kupingwa.
 
Huyu Askofu ndiye pekee anae haribugi kura kwa makusudi kwenye chaguzi za mkuu wa kanisa la KKKT nchini. Huwa anatamani awe yeye ila ndiyo hivyo tena hakubaliki ni moshi mweusi tu [emoji1787]

Huwa anakasirika sana, na hua anahisi anadhulumiwa na huwa anatamani sana uchaguzi wa Askofu mkuu wa kanisa la KKKT Tanzania usimamiwe na BAKWATA au Tume Huru ya Uchaguzi Tanzania. Huwa hawaamini kabisa wasimamizi wa kanisa. Sifahamu kama kweli anamuamini hata Mungu [emoji1787]

Baadhi ya Maaskofu wenzake humpamba kweli, kwamba yeye ndie anastahili kua Askofu mkuu wa KKKT Tanzania, Lakini wakifika kwenye uchaguzi wala hakuna alie na habari nae.

Mara nyingine husingizia ana safari ya ghafla mara tu baada ya kupiga kura ambayo huiandika madudu anayojua yeye ili tu kura hiyo iharibike.

Ana gubu na viongozi wa kuu wa kanisa lake, Lakini pia ana gubu na jinsi ambavyo serikali sikivu ya CCM inavyopeleka Maendeleo kwa wananchi kwa kasi ya ajabu...

Actually,
Anakubalika sana Karagwe na kwenye baadhi ya mitandaoni ya kijamii. Nje na hapo ni useless tu [emoji1787]
Jipige kifua huku ukisema ww ni kubwa jinga
 
Back
Top Bottom