Uchaguzi 2020 Askofu Bagonza: Ujumbe kwa vyombo vya Ulinzi

Uchaguzi 2020 Askofu Bagonza: Ujumbe kwa vyombo vya Ulinzi

KWA VYOMBO VYA ULINZI

Askofu Mkuu Oscar Romero wa El-Salvador ana ujumbe kwa vyombo vya ulinzi tunapoelekea Uchaguzi Mkuu tarehe 28/10/2020. Baba Mtakatifu Papa Francis alimtangaza kuwa Mtakatifu tarehe 14/10/2018. Askofu Romero alizaliwa 15/8/1917 na kufariki 24/3/1980. Alipadrishwa kuwa Padre 4/4/1942 na kuteuliwa kuwa Askofu Mkuu 1977. Alikufa kwa kupigwa risasi akiwa altareni akiadhimisha misa ya Sakramenti ya Meza ya Bwana. Muuaji wake, kachero wa serikali, aliingia kanisani kupitia mlango wa nyuma ya Kanisa na kumlenga kwa ustadi mkubwa wakati Askofu Mkuu Romero akiwa ameinua juu kikombe (chalice) cha divai kama ishara ya damu ya Kristo.

Baba Mtakatifu Francis alimtangaza Askofu Romero kuwa mfia dini.

Siku hiyo kabla ya kifo chake, alitoa ujumbe huu kwa vyombo vya ulinzi;

"Kaka zetu na ndugu zetu, mmetoka kwetu na mtarudi kwetu. Mnawaua ndugu zenu. Amri yoyote ya kibinadamu inayoagiza kuua ni batili
maana inajiweka juu ya amri ya Mungu isemayo USIUE. Hakuna Askari aliye juu ya Mungu na Askari halazimiki kutii amri iliyo kinyume na mapenzi ya Mungu. Hakuna anayelazimika kutii amri yenye dhambi ndani yake. Imewapasa maaskari kutii dhamiri hai za kimsingi zilizo ndani yao kuliko kutii amri batili.

Kanisa haliwezi kukaa kimya likiona amri za Mungu zinavunjwa na amri za wanadamu zinaheshimiwa, USIUE au USIIBE. KWA JINA LA MUNGU na kwa Jina la watu wanaoteseka na sauti zao kusikika mbinguni, ninawaamuru na kuwasihi, ACHA UKANDAMIZAJI, ACHA MAUAJI, ACHA DHULUMA".

Askofu Oscar Romero anaongea na wote waliokabidhiwa dhamana ya kulinda uhai wetu. Uamuzi wa kumtii Mungu uko katika vidole vilivyo jirani na kitufe kinachoruhusu risasi na mabomu. MSIKILIZE MUNGU PEKE YAKE.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.
Kwa kuongezea hapo huu Ni unumbe kwa vyombo vya dola yote Tanzania , Polisi , Jeshi , usalama wa taifa na tume ya uchaguzi , simamieni haki ,sheria na katiba note Kuna amri halali na amri haramu tendeni haki hakuna hati miliki kwa mtu yoyote au chama chochote kile cha siasa uamuzi wa wananchi kupitia kura zao uheshimiwe .
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Askofu Bogonza hudumia kondoo wako, mambo ya vyombo vya ulinzi kwako ni makubwa hujui kitu

Vyombo vya ulinzi ndio vinawapa waumini wako wasaa wa kutafuta sadaka wakuletee jumapili

Bila Amani, usingepata sadaka hapo kanisani kwako
Mkuu utakua una tatizo! Mbona umejibu bila kusoma kilichoandikwa, au mbona umejibu tofauti na mada????!
 
Ni kweli kiongozi twende October 28 tumkamuadhibu msaliti wa Nchi kutoka ubeligiji
Umefanya vyema.

Yaonekana kuelekea Oct 28 na bonus imepatikana kabisa.

Punda afe Ila mzigo ufike. Kulazimisha kushinda ni sawa na ubakaji tu.
 
Jibu swali acha kujibaraguza!
Mbona nilishajibu mkuu. Au unataka nijibu majibu unayoyataka? Anzia kusoma chini kama hujaelewa uliza tena
Hakuna anayestahili kupigwa mawe. Lakini BAK niambie tuu wewe umerusha mawe mangapi?
Au umesakizia watoto wa wenzio wakati wako umewakumbatia ndani
Unadhani kwanini JWTZ hawapigwi mawe?
Hao wengi ni wangapi mkuu. Mimi najua watanzania wanawaita police
Unadhani ni kwanini wanaitwa polisiccm na siyo polisichadema au polisiact!?
Askofu Bagonza amefanya jambo jema sana kuwakumbusha vyombo vya ulinzi kuhusu umuhimu wa kulinda uhai wa watu. Abarikiwe sana Askofu

Na biblia katika 1Petro2:13-20 inatukumbusha utii.
13Kwa ajili ya Bwana, tiini kila mamlaka iliyowekwa na wanadamu: Kwa mfalme kwani ndiye aliye na mamlaka ya juu zaidi, 14au kwa maafisa aliowaweka, kwa kuwa mfalme amewatuma ili kuwaadhibu wale wanaokosa, na kuwapongeza wale watendao mema. 15Kwa maana ni mapenzi ya Mungu kwamba kwa kutenda mema mnyamazishe maneno ya kijinga ya watu wapumbavu. 16Ishini kama watu huru, lakini msitumie uhuru wenu kama kisingizio cha kutenda uovu, bali ishini kama watumishi wa Mungu. 17Mheshimuni kila mtu ipasavyo: Wapendeni jamaa ya ndugu waumini, mcheni Mungu, mpeni heshima mfalme.

18Ninyi watumwa, watiini mabwana zenu kwa heshima yote, si wale mabwana walio wema na wapole peke yao, bali pia wale walio wakali. 19Kwa maana ni jambo la sifa kama mtu akivumilia anapoteswa kwa uonevu kwa ajili ya Mungu. 20Kwani ni faida gani kwa mtu kustahimili anapopigwa kwa sababu ya makosa yake? Lakini kama mkiteswa kwa sababu ya kutenda mema, nanyi mkastahimili, hili ni jambo la kusifiwa mbele za Mungu.

Tufate sheria na taratibu za tume na mwombe Mungu atujalie uchaguzi wenye amani
 
Narudia tena acha kujibaraguza na longo longo zako! Polisiccm wanapigwa mawe na Watanzania nikakuuliza unadhani ni kwanini JWTZ hawapigwi mawe!? 😳
Mbona nilishajibu mkuu. Au unataka nijibu majibu unayoyataka? Anzia kusoma chini kama hujaelewa uliza tena
 
KWA VYOMBO VYA ULINZI

Askofu Mkuu Oscar Romero wa El-Salvador ana ujumbe kwa vyombo vya ulinzi tunapoelekea Uchaguzi Mkuu tarehe 28/10/2020. Baba Mtakatifu Papa Francis alimtangaza kuwa Mtakatifu tarehe 14/10/2018. Askofu Romero alizaliwa 15/8/1917 na kufariki 24/3/1980. Alipadrishwa kuwa Padre 4/4/1942 na kuteuliwa kuwa Askofu Mkuu 1977. Alikufa kwa kupigwa risasi akiwa altareni akiadhimisha misa ya Sakramenti ya Meza ya Bwana. Muuaji wake, kachero wa serikali, aliingia kanisani kupitia mlango wa nyuma ya Kanisa na kumlenga kwa ustadi mkubwa wakati Askofu Mkuu Romero akiwa ameinua juu kikombe (chalice) cha divai kama ishara ya damu ya Kristo.

Baba Mtakatifu Francis alimtangaza Askofu Romero kuwa mfia dini.

Siku hiyo kabla ya kifo chake, alitoa ujumbe huu kwa vyombo vya ulinzi;

"Kaka zetu na ndugu zetu, mmetoka kwetu na mtarudi kwetu. Mnawaua ndugu zenu. Amri yoyote ya kibinadamu inayoagiza kuua ni batili
maana inajiweka juu ya amri ya Mungu isemayo USIUE. Hakuna Askari aliye juu ya Mungu na Askari halazimiki kutii amri iliyo kinyume na mapenzi ya Mungu. Hakuna anayelazimika kutii amri yenye dhambi ndani yake. Imewapasa maaskari kutii dhamiri hai za kimsingi zilizo ndani yao kuliko kutii amri batili.

Kanisa haliwezi kukaa kimya likiona amri za Mungu zinavunjwa na amri za wanadamu zinaheshimiwa, USIUE au USIIBE. KWA JINA LA MUNGU na kwa Jina la watu wanaoteseka na sauti zao kusikika mbinguni, ninawaamuru na kuwasihi, ACHA UKANDAMIZAJI, ACHA MAUAJI, ACHA DHULUMA".

Askofu Oscar Romero anaongea na wote waliokabidhiwa dhamana ya kulinda uhai wetu. Uamuzi wa kumtii Mungu uko katika vidole vilivyo jirani na kitufe kinachoruhusu risasi na mabomu. MSIKILIZE MUNGU PEKE YAKE.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.
Safisana
 
But Askofu kama kweli Wewe ni mshauri Kwanini unapenda kuegemea Chadema tu?

Unamaanisha Chadema ndio hawakosei ?

Mbona hukemei ushoga ambaye mgombea wa chadema Aliwatetea ?
Kama.nyinyi.ndiomnaokemea.ushoga.mbona.mlimuachia.makonda.sakalaushoga
 
Narudia tena acha kujibaraguza na longo longo zako! Polisiccm wanapigwa mawe na Watanzania nikakuuliza unadhani ni kwanini JWTZ hawapigwi mawe!? 😳
Sijui chochote, niambie kwanini
 
Ni kweli kiongozi twende October 28 tumkamuadhibu msaliti wa Nchi kutoka ubeligiji

Kwangu na kwetu wengi, Lissu na Maalim Seif ni wakombozi wetu.

Huyu wa Chatto aka mkoloni mweusi atatutambua. Hatuna mzaha. Hatucheki na nyani tena.

1. Tunajihimu vituoni.
2. Tunakikisha mawakala wetu wapo gado.
3. Tunapiga kura.
4. Tunabaki vituoni, hatuondoki.
5. Tutatangaziwa matokeo ya vituoni hapo hapo.

NB tutaelewana tu. JKNIA busara ilitumika. Hapa msipime!

Wengine Buriani tayari tulishatoa.
 
Back
Top Bottom