Askofu Benson Bagonza adai kuna wanaotaka kumdhuru, wamefika Karagwe

Askofu Benson Bagonza adai kuna wanaotaka kumdhuru, wamefika Karagwe

Hii ndio Taarifa aliyoisambaza mitandaoni siku ya leo , kwamba kuna watu wabaya wamefika Karagwe kwa lengo la kummaliza , bali amejiapiza kwamba hatokimbia na anasubiri watekeleze Unyama wao .

Binafsi siwezi kupuuza taarifa hii ya kiharamia kutokana na ukweli kwamba sasa tuko kwenye Tanzania mpya ambayo wote waliotoa taarifa za kuwindwa hawakulindwa hadi wakaumia ama kupotea , Lissu na Ben Saa Nane ni mifano halisi , mpaka leo Polisi hawana maelezo yaliyonyooka zaidi ya kumung'unya maneno tu .

Mungu mbariki Baba Askofu Bagonza
Ninavyojua Watu wakikuamulia hasa Kukumaliza huwezi kamwe kujua na hata wa karibu yako hakuna ambaye atajua. Sasa huyu Askofu anatuboa!
 
Duuu askofu wetu wanataka kumfanya nini hawa TISS

maana tushazoea hatukawii kusikia kapotea katekwa kwashambuliwa kauwawa na watu wasiojulikana

wanaotekeleza na wanapanga na wanao toa maelekezo Mungu wa haki awaumbue na awahukumu upesi
 
Jiwe ni mtu hatari sana! Alafu watu wakikimbia nchi, MATAGA wanaona kama ni kutafuta umaarufu na kuchafua nchi wakati mambo wenyewe ndio haya.
Kwahiyo Bagonza naye yuko mbioni kukimbia nchi!!!
 
Sababu kubwa ya kutaka kumuua ni kusema ukweli kuhusu hali mbaya ya haki za binadamu, udhalimu Nchini na kukosa kama demokrasi ya kweli. Msikilizeni Warioba hapa chini bila ya shaka huyo anayejiita mwendawazimu ataanza kutishia uhai wake.


Mwambie atueleze na ile pesa ya Mwananchi Gold ilikoyeyukia.
 
Askofu anastukia kivuli chake!!
kama kuna usaliti wowote kafanya, afanye toba mapema.

Saa inakuja ambayo kila mtu atalipwa kulingana na matendo yake.
Kofia ya uaskofu haitasaidia wakati ukiwadia.
TISS mnaua watanzania wenzenu kwa maslahi ya mtu mmoja. Kwanini msimuue yeye aliyemuweka mtoto wa dada yake HAZINA ili aibe vizuri????
 
Back
Top Bottom