Hii ndio Taarifa aliyoisambaza mitandaoni siku ya leo , kwamba kuna watu wabaya wamefika Karagwe kwa lengo la kummaliza , bali amejiapiza kwamba hatokimbia na anasubiri watekeleze Unyama wao .
Binafsi siwezi kupuuza taarifa hii ya kiharamia kutokana na ukweli kwamba sasa tuko kwenye Tanzania mpya ambayo wote waliotoa taarifa za kuwindwa hawakulindwa hadi wakaumia ama kupotea , Lissu na Ben Saa Nane ni mifano halisi , mpaka leo Polisi hawana maelezo yaliyonyooka zaidi ya kumung'unya maneno tu .
Mungu mbariki Baba Askofu Bagonza
Siungi mkono Vitisho ,mauaji na utekaji lakini pia kwa sasa siwaungi mkono wakosoaji au wapinzani mana sijui wanataka nini?
Magufuli anataka maendeleo kwa wananchi wanyonge. Hapo kosa la Magufuli ni nini?
Kwa nini tusimuunge mkono kwenye suala la Maendeleo.?
Kuna watu wameliibia taifa hili kwa miaka mingi kupitia Siasa na masaraka.
Viongozi wa kisiasa walifanya siasa kuwa mchezo wa kujipatia mapesa mengi ya kodi za wananchi huku maendeleo yakirudi nyuma. Hapo kwa nini tusijitokeze kumshauri Magufuli namba ya kuwabana na hata kuwafunga Majizi yanayoliingizia taifa hili hasara huku familia zao zikineemeka?
Nchi hii ina watu zaidi ya mil.60 lakini watu wasiozidi 2000 wanamaliza kodi za wananchi na kulisababishia Taifa hili kuwa ombaomba na madeni huku wao na familia zao wakipiga hatua kwa Kasi inayolingana na Rocket ili kuvuka anga za juu, yaani Escaping Velocity. Hili hakuna Mwanaharakati wala Askafu wala Nabii ,wala mtume ,wala kiongozi wa dini ,wala kiongozi wa kisiasa ,wala shekhe, wala ustadhi wala Imamu ,wala mufti ,wala Kadinali anayeliongelea na kuitaka serikali ichukue hatu kuahakikisha kuwa Pato la nchi hii lisiishie kwenye mikono ya watu wasiozidi elfu mbili huku wengine wote wakilitumikia taifa hili kwa machozi na jasho kubwa.
Nilitegemea sasa Maaskofu nao wajitokeze wataje mishahara yao hadharani na walinganishe na ile ya Wateuliwa ,wabunge,majaji n.k.. Wajipime waone kuwa ni sawa kukaa kimya huku kundi dogo kabisa linalogonga meza tu na kuzunguka kufokea fokea watu tu bila mikakati mipana ya kuondoa umaskini kwa wanyonge wanavyolipwa mapesa karibu yote ya pato la serikali.
Je, askofu amewahi kutafakari kwa sauti kuwa ikitokea siku moja Waziri au mwanasiasa au mbunge mmoja kulipwa maslahi yenye kumjengea huyo mwanasiasa au mbunge au waziri au mteuliwa au Jaji au mstaafu uwezo wa kuajiri maaskofu watatu mpaka wanne na kuwalipa kwa mwezi kutokana na utofauti wa vipato uliopo kwa watanzania kwenye nchi moja ,tena nchi maskini ya kijamaa atalisemea hili na kulipigia kelele au naye atatamani kutafuna Vipato vya maskini?
Hivi bado tu askofu hajabaini kuwa kuna kundi la wanasiasa ndani ya vyama vyote vya siasa ikiwemo CCM wanaotumia nafasi zao kutaka kumjengea Rais taswira mbaya ili waendelee kuitafuna nchi mana wameshafahamu wazi kuwa kwa sasa kinachofuata ni kuwanyoosha wezi waliokuwa wamejihalalishia kula na kuvimbiwa na kumwaga kupitia madaraka kwenye siasa na serikali?
Ni wakati sasa wa kupaza sauti kupigania maslahi ya watanzania yanayotumiwa vibaya na wanasiasa kwa mgongo wa sheria na kanuni ziliowekwa na watu waliokuwa na dhamira ya kulifilisi taifa huku wao wakineemeka.
Uchaguzi umekwisha tumuunge mkono Rais ili tusonge mbele. Vita ya kiuchumi ihamie ndani mana kuna mabeberu waliopo kwenye mgongo wa siasa za ndani na hawa ndio tatizo kubwa. Wanajifanya kumuunga mkono Rais lakini mioyo yao yote inalenge kujinufaisha tuu na sio vinginevyo.
Hivi ni kweli wenyeviti wa vyama vyote vya upinzani wanawaza kujenga Demokrasia au wanawaza kujinufaisha kupitia nafsia hizo.?
Kuna mambo watanzania tukizubaa yasipofanyika awamu hii hayatakuja kufanyika tena ? Na nchi itakua ni shamba la bibi la wanasiasa.
Pole sana Baba askofu kwa matishio ya watu waovu .
Hii nchi itakua salama zaidi tukiamua kumiunga mkono Rais ili uteuzi wa wanasiasa usiwe ndio uteuzi wa kula nchi iloyojaa maskini!
Wanaojiona kuwa wananeemeka kutokana na madaraka Mara nyingi ndio wanaowachukia wakosoaji mana wanaona kama watu wanaowazibia utajiri haraka . Ni lazima uongozi uwe ni mzigo ili waliochaguliwa na Mungu ndio wawe tayari kuwatumikia wananchi maskini wanaolipa kodi .