Uchaguzi 2020 Askofu Benson Bagonza: Wote Hawaamini

Uchaguzi 2020 Askofu Benson Bagonza: Wote Hawaamini

Sikia nikwambie, ni ujinga kusema mmeibiwa.

Na hata kama ni kuibiwa basi mnaibiwa kuanzia madiwani, ubunge mpaka Urais tena nchi nzima kila kata?

Na kama ni kweli mmeibiwa basi nyinyi ni wapuuzi, kwanini mnaibiwa kila uchaguzi ilhali mawakala wenu wapo na wanafatilia kila hatua ya upigaji kura?

Kama kweli kila mwaka mnaibiwa na mnakubali kushiriki uchaguzi wa wizi, viongozi wenu wanaakili timamu kwenye vichwa vyao, kukubali kushiriki kwenye uwizi?

Kama kweli mnaibiwa basi mnaibiwa kizembe sana hata mkipewa nchi rasilimali za nchi pamoja na hazina ya nchi itaibiwa kizembe sana kwakuwa hamko makini.

CHADEMA piteni kushoto mtupishe.
CCM tuna jambo letu la kuapishwa kwa Rais JPM.
 
Furaha alipotea na hajarudi tena. Na sasa Imani ametekwa mazima.. Nakuelewa sana baba Askofu, M/Mungu akutangulie.
 
Askofu anatoa maneno matupu ya misamiati, CCM ishashinda kwa kishindooo, askofu endelea kutoa maneno zaidi na zaidi, CCM INATOA VITENDO ZAIDI
Haijashinda imejishindisha kwa mtutu wa bunduki na vifaru. Kubwa lilajo
 
Si vizuri kwenda matokeo kwenye mpira au kwenye sanduku la kupigia kura. Mioyo ya watu ina siri nyingi.
 
WOTE HAWAAMINI...

Na Askofu Benson Bagonza, KKKT Dayosisi ya Karagwe

Waliopiga kura hawaamini,
Waliogoma kupiga kura hawaamini,
"Walioshinda" hawaamini,
"Walioshindwa" hawaamini,
Walioshuhudia hawaamini,
Waliohesabu kura hawaamini,
Wasimamizi hawaamini,
Waangalizi wa ndani na nje hawaamini,
Walinzi wa amani hawaamini,

Kwa nini lakini?

KWA sababu mwaka 2019 baada ya Uchaguzi wa serikali za mitaa,

"Walioshinda" hawakuwa na furaha,
"Walioshindwa" hawakuwa na furaha,
Waliopiga kura, ambao hawakupiga kura, waliohesabu, waliotangaza na waliosikia, WOTE hawakuwa na furaha. FURAHA alipotea, hajarudi. Sasa na IMANI ametoweka.

Usinibishie kwa sababu ubishi ni hulka ya watu waliopoteza furaha na Imani.

Nani anafuata kuwafuata FURAHA na IMANI?
Hehehee kila mtu haamini
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] Katika watu wanaumia katika haya matokeo ni huyu Askofu wangu! Maana yeye alishajichagulia upande toka siku nyingi sana.
Kweli mkuu, yeye alishajichagulia upande long time ago, sasa anaugulia ndani kwa ndani. Sitashangaa next time akiamua kujitosa ulingoni 😂😂😂
 
WOTE HAWAAMINI...

Na Askofu Benson Bagonza, KKKT Dayosisi ya Karagwe

Waliopiga kura hawaamini,
Waliogoma kupiga kura hawaamini,
"Walioshinda" hawaamini,
"Walioshindwa" hawaamini,
Walioshuhudia hawaamini,
Waliohesabu kura hawaamini,
Wasimamizi hawaamini,
Waangalizi wa ndani na nje hawaamini,
Walinzi wa amani hawaamini,

Kwa nini lakini?

KWA sababu mwaka 2019 baada ya Uchaguzi wa serikali za mitaa,

"Walioshinda" hawakuwa na furaha,
"Walioshindwa" hawakuwa na furaha,
Waliopiga kura, ambao hawakupiga kura, waliohesabu, waliotangaza na waliosikia, WOTE hawakuwa na furaha. FURAHA alipotea, hajarudi. Sasa na IMANI ametoweka.

Usinibishie kwa sababu ubishi ni hulka ya watu waliopoteza furaha na Imani.

Nani anafuata kuwafuata FURAHA na IMANI?
Utapata taabu sanaaaa.
 
Back
Top Bottom